Godoro la kioo
JF-Expert Member
- Aug 2, 2025
- 364
- 727
Wakuu poleni na matatizo yanayoikumba nchi yetu. Poleni kwenu mliopoteza ndugu, jamaa, na marafiki kutokana na yaliyojiri oct29
Bila kuwachosha. Kuna msemo maarufu usemao """Wajinga ndiyo waliwao"""'
Ilikuwa tarehe 20 mwezi wa 11 mwaka 2025 ndo siku ambayo kwa mara ya kwanza nilihisi kuchanganyikiwa na kutembea barabarani nikiongea pekee yangu hii ni baada ya kutapeliwa kiasi Cha laki Moja na elfu kumi.
Mkasa mzima ulikuwa hivi
Siku Moja katika pitapita zangu mtandaon nikakutana na tangazo la mtu anaedai kuwa anauza simu used kutoka dubai
Kwa kuwa nilikuwa na shida na simu wakati huo basi nikachukua namba zake kama inavyoonekana hapo chino.
Nikawasiliana nae vizuri akanipa utaratibu wote unavyokuwa, maskin wa Mungu nikamwamini (kosa kubwa sana)
Akanielekeza kuwa Simu zipo ukifka dukani ni sh laki Moja ila kwa mkoani unalipia nauli elfu kumi akasema kuwa unatuma Hela Kisha ndo mzigo wako unapelekwa kwenye basi tayari kwa kusafirishwa
Basi akanitumia namba yake ya M-pesa Hela nikatuma Jina likaja Jaffari Yusuph
Baada ya muda kidogo akanipigia na kuniambia Hela nimeiona Kisha akaniuliza nikuchagulie ya rangi gani
Mimi nikamwambia nyeusi akaniambia nimtumie taarifa zangu nikamtumia
Hela nilituma saa nne asubuhi kwa makubaliano kuwa muda huo huo anawapelekea hao wanaosafirisha kuja huku mkoani (ilitakiwa ije kahama)
Na alisema kuwa akiwakabidhi atanipigia Ili kunijulisha mzigo umekuja na bus la aina gani ,nikasema sawa
Imefika Saa nane mchana mtu Yuko kimya saa tisa kimya
Ilipofika saa kumi na Moja nikampigia kumuuliza je simu inakuja na kampuni gani . muda huo akili imeshaanza kuvurugika
Akaniambia simu imepelekwa stendi na aloipeleka bado hajarudi, akirudi atanijuza kwa hiyo nivute subira
Saa Moja usiku kimya akili ndo ikanirudi nikajua nishatapeliwa kupiga simu ikawa haipokelewi mwisho akaizima
Nikiri wazi nilitamani kujiua hiyo siku kutokana na kwamba nimeweza kumtumia kiasi chote hicho mtu Ambae simjui
Nilijilaumu mno nilihisi kuchanganyikiwa kiasi kwamba nilijiona Mimi ni mjinga wa mwisho
Hii itabaki kwenye historia ya maisha yangu yote
Tangazo ndo kama lilivyo hapo chini
Jaffari Yusuph, Jaffari Yusuph popote ulipo Mungu anakuona
N.B:Nisamehen kwa uandishi mbovu