Jinsi nilivyookoa ndoa ya watu

Jinsi nilivyookoa ndoa ya watu

nilishasema kwamba katika mahusiano yangu na mwanamke yeyote sitakaa nimshirikishe mtu wa tatu hata kiwe nini, kama tulikutana wawili tukatamaniana wawili tukatongozana na kukubaliana bila mtu wa tatu basi ni jambo gani litaloshindikana baina yetu?! tukishindwa kabisa kuyajenga mimi na yeye basi mtu wa tatu utakuwa ni unafki tu. mleta mada haukutakiwa kupeleka habari za ndani za jirani yako kwenye mitandao ya kijamii! kuna jamaa yangu alienda na mkewe mtarajiwa kutubu kabla ya kufunga ndoa, alipotoka kwenye kale kachumba akawa anacheka huku anatingisha kichwa, jamaa kamuuliza "vipi?"..dada wa watu kasema alivomaliza kutubu eti faza kaanza kuchombeza "leo umepeneza", kwenye mahusiano usimwamini nyang'au yeyote wa tatu.
 
Jumapili iliyopita nikiwa nimejipumzisha nyumbani kwangu mara akatokea rafiki yangu ambaye ni jirani yangu, akaniomba niende kwake nikamsaidie kusuluhisha kwani kuna kasheshe limetokea kati yake na mke wake.

Pia huyu mkewe ana undugu na mimi kwa mbali hivyo tunaheshimiana kama kaka na dada. Sikukataa wito nikaondoka naye, nilipofika nyumbani kutaka kujua kulikoni..yule dada akaanza kunisimulia kuwa mumewe ana tabia ya kumchungulia housegirl kila anapokwenda kuoga, mara nyingi eti housegirl anapoingia bafuni kuoga mume naye atatafuta mbinu yoyote ya kutoka nje ili aweze kumchungulia.

Bafu lenyewe lipo kwenye nyumba yao kubwa lakini unaweza kumchungulia kwa nje kama utapanda kwenye ngazi au stuli.

Huyu dada akaendelea kusema kuwa alikuwa hajui kitu anachokifanya mumewe kwa muda mrefu kidogo kama miezi miwili iliyopita, lakini siku hiyo ya Jumapili alisikia kishindo kwa nje akatoka haraka kwenda kuangalia nini kimetokea..akamkuta mumewe akiugulia maumivu chini na ndoo aliyokuwa ameitumia kusimamia ili amchungulie housegirl ikiwa imepasuka.

Hivyo akaunganisha tukio la ndoo na kinachofanyika bafuni na akakumbuka mumewe huwa anatoka nje karibu kila siku kwa wakati ambaye h/girl anaoga basi akajua kuwa moja kwa moja alikuwa na tabia ya kumchungulia housegirl.

Dada alikuja juu kama simba aliyenyang'anywa watoto wake anataka talaka yake aanze zake kuliko kuendelea kuaibika namana hiyo. Huyu mume alikana kuwa alikuwa afanyi hivyo bali ndoo ilimtega wakati akizunguka nyuma ya nyumba kuangalia usalama wa nyumba yao. Wakagombana sana..mwisho wa siku wakakubaliana waniite mimi kama rafiki yao wa karibu na walijua nitatoa maamuzi ya busara yatakayowasaidia wote wawili. (kumbuka mimi siyo mshenga wao wala msimamizi wao).

Basi niliposikiliza maelezo ya pande zote mbili nikawaomba tuende eneo la tukio, kweli nikakuta ndoo imetoboka katikati, haiitaji kuwa na degree kujua chanzo cha kutoboka kwa hiyo ndoo, kwani ilitoboka kwa sababu ya kitu kizito kilichowekwa juu yake au mtu kusimama juu yake.

Nikatumia akili yangu ya kuzaliwa nikawaambia kwanza mmefanya vizuri kuja kuniambia ili msijiaibishe kwa watu. Pili nikamwambia mwanamke mumeo anakupenda sana kwani kama kweli unamfikiria kitendo alichokifanya kuwa ni kweli basi angeweza si tu kumchungulia bali kumfanya mke kabisa au nyumba ndogo iliyoko kwenye nyumba kubwa.

Huyu jamaa ana uwezo wote angeweza hata kumwachisha kazi akampangia sehemu nyingine ili aendeleze uharamia wake huo ambao unaufikiria.

Sasa kwa muda huo aliokaa dada (miezi 6) na ajafanya hivyo basi unayodhania siyo kweli kama hayana kithibitisho.

Ni kamwambia mume wako anakupenda ndiyo maana anawahi kuja nyumbani kama siyo hivyo angekuwa anakuja saa nane za usiku kama wanaume wengine, niliongea mengi mwisho wa siku mke akamuomba mumewe msamaha wakapeana mikono yakaisha.

Basi nikaendelea kukaa pale kupima upepo ni kweli yaliisha. mwisho wa siku wakanisindikiza wote wawili nyumbani. Kesho yake yule jamaa akanifuata mapema akanipa 50,000 eti nikanye wine kwani nimeokoa ndoa yake, nikajaribu kumuuliza madai ya mkewe yalikuwa ya ukweli? akasema ni kweli kabisa.

Huyu dada anafanya kazi serikalini na mumewe anafanya kazi kwenye NGO.

Hivyo ndivyo nilivyo okoa ndoa ya watu.

Yaani siamini kama umeamua kunisema jf !
Mimi nlikupa hela ili unitunzie siri halafu umekuja kuharibu!
 
nilishasema kwamba katika mahusiano yangu na mwanamke yeyote sitakaa nimshirikishe mtu wa tatu hata kiwe nini, kama tulikutana wawili tukatamaniana wawili tukatongozana na kukubaliana bila mtu wa tatu basi ni jambo gani litaloshindikana baina yetu?! tukishindwa kabisa kuyajenga mimi na yeye basi mtu wa tatu utakuwa ni unafki tu. mleta mada haukutakiwa kupeleka habari za ndani za jirani yako kwenye mitandao ya kijamii! kuna jamaa yangu alienda na mkewe mtarajiwa kutubu kabla ya kufunga ndoa, alipotoka kwenye kale kachumba akawa anacheka huku anatingisha kichwa, jamaa kamuuliza "vipi?"..dada wa watu kasema alivomaliza kutubu eti faza kaanza kuchombeza "leo umepeneza", kwenye mahusiano usimwamini nyang'au yeyote wa tatu.
Unajua elimu ingekuwa inafungiwa chumbani tusingeipata, Hapa JF nimeleta kama ushuda wa kujifunza na wala siyo umbeya kama unavyodhani. Kumbuka kuwa sijamtaja mtu yoyote kwa jina, unadhani tutajifunzia wapi kama siyo kupata experince za wengine? unavyojua maisha ya ndoa hayana formula hivyo tunajifunza kupitia uzoefu wa mwingine. Kwa hiyo ndugu yangu na declare kwamba sikuwa na nia ya kumsema mtu vibaya bali watu wajifunze kupitia kwake. Kwani unapoambiwa kwamba JF inaelimisha ulidhani kuna mwalimu anakuja huku na chaki au projector kutoa lecture? but anyway hayo ni mawazo yako.

 
hongera pia kwa kutumia busara na hekima kuwapatanisha
ubarikiwe kwa hlo
Biblia imeandika heri wapatanishi kwa kuwa wataitwa wana wa Mungu...
Unajua kwenye usuluishi wa ndoa usijaribu hata siku moja kuwaachanisha, ukiona hauwezi achia ngazi mapema kwani walivyokutana haukuwepo wakielewana utaiweka wapi sura yako? hapa unatumia hekima tu ya kawaida.

 
Inaonesha jamaa anamwogopa mother house kuliko kingine chochote. Shida yote nini mpaka mtu uvunjike guu kisa kuchungulia? Tena hapo sio kuchungulia bali kutazama, ukiwa mbali na kumeza mate mpaka akimaliza kuoga na weye umeshashiba mimate?? Jamani, mijitu mingine ni hasara tu.
Mihele yote alokupa si angempa h/g anejilambia kiulainiiii au apewe ruksa ya kumwogesha?? Akili nyingine, tope tupu.
Binadamu wako tofauti sana, na ndiyo maana kuna sheria mbalimbali za kuadabisha tabia zisizofaa ndani ya jamii.

 
ha ha ha ha stori tamu sana sasa mzee ungekatupia basi hata kapicha ka hiyo ndoo ilivyotoboka
kutumia tena kapicha mkuu nitawadhalilisha na mimi sitajisikia amani rohoni, ila kikubwa hapa ni elimu ya ndoa kupitia uzoefu wao. Nadhani kuna kitu tutajifunza hapa.

 
Yaani siamini kama umeamua kunisema jf !
Mimi nlikupa hela ili unitunzie siri halafu umekuja kuharibu!
Matukio yanaweza kufanana, lakini hata hivyo jamaa nimeshamwambia aangalie kile kisa chake hapa JF, kafurahi kaniambia watu wengi watajifunza kwani yeye ni shetani tu alimpitia hivyo hatarajii kurudia kitu kama hicho maishani mwake.

 
yaaa hili domo zege...hakuna cha timing miezi 3 anachungulia tuuu.it seems h/gal ana kijungu.
siyo kijungu tu bali hata chuchu zimesimama sana....ana miaka kama 18 au 19 hivi, sasa sikumuuliza jamaa interest yake ilikuwa nini kwani ni mambo ya aibu kuyachambua zaidi. Ila nilimwambia mama mwenye nyumba asimfukuze huyo house girl kwani hata hajui kilichokuwa kinaendelea huko nje. Siunajua tena wamama wakishaona hivyo wanamtimua house girl

 
Duh,Ukistaajabu ya Mussa.Huyo jamaa bila shaka hata kazini anawachungulia wafanyakazi wenzie.Huyo House girl anajua kuhusu huo mzozo?.Mwanamke ameamua kupotezea ila ana yake moyoni,siku wakikosana jamaa asishangae kuambiwa ndio maana ulimchungulia House girl.
yaa inawezekana kwani wanawake wengi hawafuti makosa moyoni moja kwa moja...hivyo ni kazi ya jamaa kuchukua hatua mpya za kinidhamu

 
mmmmh ndoa zingine jamani, ila kwa jinsi mimi nilivyo hiyo kesi isingeisha kirahisi hivyo mshukuru huyo mwanamke ni mwepesi wa kuachilia
Maisha ya kusameheana kwa makosa mbalimbali ndiyo maisha ya afya dada yangu Mrsleo, usikubali kukaa na kitu rohoni...

 
utakuwa umefanya nini kama huyu mke akasoma habari hizo humu ndani ya jamiii forum kwmba ilikuwa kweli na kujua kuwa wewe ulikuwa unalimda rafiki yako na unamfichia sirik?umbuka kwamba huu ni mtana wa kijamii sidhani kama ni vema ku expose mambo binafsi hasa ya watu/mtu wngine.
Hapana huyo mama hayupo huku JF lakini mumewe yupo na nimeshamwambia. Nia ya hii kama nilivyosema ni kutoa elimu kupitia experience za watu wengine, ndiyo maana MMU lipo

 
ha ha ha ha haa jamani duh mumeo mzee wa chabo uwiii..... kunywa wine tu aisee... mkuu house girl ni chombo?
Housegirl ni kama wananwake wengine tu, Tafsiri ya yeye kuwa chombo sijui nitaliwekaje hapa, ila ana makalio kiasi na chuchu saa sita umri ni kati 18 au 19 hivi. Ninachojua kidogo kuhusu tabia yake ni kwamba anaheshima sana mpaka nadhani kapitiliza.
 
Housegirl ni kama wananwake wengine tu, Tafsiri ya yeye kuwa chombo sijui nitaliwekaje hapa, ila ana makalio kiasi na chuchu saa sita umri ni kati 18 au 19 hivi. Ninachojua kidogo kuhusu tabia yake ni kwamba anaheshima sana mpaka nadhani kapitiliza.

nawe ushaanza kumtamani huyo hgl
 
Housegirl ni kama wananwake wengine tu, Tafsiri ya yeye kuwa chombo sijui nitaliwekaje hapa, ila ana makalio kiasi na chuchu saa sita umri ni kati 18 au 19 hivi. Ninachojua kidogo kuhusu tabia yake ni kwamba anaheshima sana mpaka nadhani kapitiliza.

nikisema ni chombo na maanisha ni mzuri mkuu ..... hapo hata kama ni mimi ningepiga chabo
 
Hahaha dah nimecheka hapo kwenye ndoo.ila ndoa hizi jamani.!! ningekuwa ni mimi ningemtia bakora huyo mume augulie vizuri.
Ila Hongera kwa kusovu tatizo.
 
Back
Top Bottom