SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,615
- 929
Jumapili iliyopita nikiwa nimejipumzisha nyumbani kwangu mara akatokea rafiki yangu ambaye ni jirani yangu, akaniomba niende kwake nikamsaidie kusuluhisha kwani kuna kasheshe limetokea kati yake na mke wake.
Pia huyu mkewe ana undugu na mimi kwa mbali hivyo tunaheshimiana kama kaka na dada. Sikukataa wito nikaondoka naye, nilipofika nyumbani kutaka kujua kulikoni..yule dada akaanza kunisimulia kuwa mumewe ana tabia ya kumchungulia housegirl kila anapokwenda kuoga, mara nyingi eti housegirl anapoingia bafuni kuoga mume naye atatafuta mbinu yoyote ya kutoka nje ili aweze kumchungulia.
Bafu lenyewe lipo kwenye nyumba yao kubwa lakini unaweza kumchungulia kwa nje kama utapanda kwenye ngazi au stuli.
Huyu dada akaendelea kusema kuwa alikuwa hajui kitu anachokifanya mumewe kwa muda mrefu kidogo kama miezi miwili iliyopita, lakini siku hiyo ya Jumapili alisikia kishindo kwa nje akatoka haraka kwenda kuangalia nini kimetokea..akamkuta mumewe akiugulia maumivu chini na ndoo aliyokuwa ameitumia kusimamia ili amchungulie housegirl ikiwa imepasuka.
Hivyo akaunganisha tukio la ndoo na kinachofanyika bafuni na akakumbuka mumewe huwa anatoka nje karibu kila siku kwa wakati ambaye h/girl anaoga basi akajua kuwa moja kwa moja alikuwa na tabia ya kumchungulia housegirl.
Dada alikuja juu kama simba aliyenyang'anywa watoto wake anataka talaka yake aanze zake kuliko kuendelea kuaibika namana hiyo. Huyu mume alikana kuwa alikuwa afanyi hivyo bali ndoo ilimtega wakati akizunguka nyuma ya nyumba kuangalia usalama wa nyumba yao. Wakagombana sana..mwisho wa siku wakakubaliana waniite mimi kama rafiki yao wa karibu na walijua nitatoa maamuzi ya busara yatakayowasaidia wote wawili. (kumbuka mimi siyo mshenga wao wala msimamizi wao).
Basi niliposikiliza maelezo ya pande zote mbili nikawaomba tuende eneo la tukio, kweli nikakuta ndoo imetoboka katikati, haiitaji kuwa na degree kujua chanzo cha kutoboka kwa hiyo ndoo, kwani ilitoboka kwa sababu ya kitu kizito kilichowekwa juu yake au mtu kusimama juu yake.
Nikatumia akili yangu ya kuzaliwa nikawaambia kwanza mmefanya vizuri kuja kuniambia ili msijiaibishe kwa watu. Pili nikamwambia mwanamke mumeo anakupenda sana kwani kama kweli unamfikiria kitendo alichokifanya kuwa ni kweli basi angeweza si tu kumchungulia bali kumfanya mke kabisa au nyumba ndogo iliyoko kwenye nyumba kubwa.
Huyu jamaa ana uwezo wote angeweza hata kumwachisha kazi akampangia sehemu nyingine ili aendeleze uharamia wake huo ambao unaufikiria.
Sasa kwa muda huo aliokaa dada (miezi 6) na ajafanya hivyo basi unayodhania siyo kweli kama hayana kithibitisho.
Ni kamwambia mume wako anakupenda ndiyo maana anawahi kuja nyumbani kama siyo hivyo angekuwa anakuja saa nane za usiku kama wanaume wengine, niliongea mengi mwisho wa siku mke akamuomba mumewe msamaha wakapeana mikono yakaisha.
Basi nikaendelea kukaa pale kupima upepo ni kweli yaliisha. mwisho wa siku wakanisindikiza wote wawili nyumbani. Kesho yake yule jamaa akanifuata mapema akanipa 50,000 eti nikanye wine kwani nimeokoa ndoa yake, nikajaribu kumuuliza madai ya mkewe yalikuwa ya ukweli? akasema ni kweli kabisa.
Huyu dada anafanya kazi serikalini na mumewe anafanya kazi kwenye NGO.
Hivyo ndivyo nilivyo okoa ndoa ya watu.