macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,223
- 60,290
Utapeli wowote una kanuni moja muhimu: mtu anakuvutia kuwa utapata pato nono kwa kufanya kazi ndogo sana! Ukiishaijua hii kanuni wala hutakaa utapeliwe kirahisi namna hii. Halafu hii aina ya utapeli anayoiongelea mwanzisha thread ni ya siku nyingi mno mno ila version zinabadilika tu! Nakumbuka zamani sana nilishasikia bibi yangu anahadithia babu yangu akiwa kijana alienda mjini akakutana na wale waangusha pochi. Mbele anatangulia mtu anaangusha pochi halafu nyuma anakuja mwenzake ambaye humjui na kukushawishi muichukue mkagawane kilichopo. Matokeo yake ukienda wanakuchenjia uchochoroni na kukunyanganya kila kitu. Sasa mwanzisha thread alifanya kosa kubwa sana kukubali kufuatana nao kwani wangeweza kutumia nguvu kuzichukua zile fedha.Da! Nilikutana na hii kitu mwaka 2013.hawa jamaa wananusa Sana hela.
Hata kuchukua ujira usio sahihi kwa sababu anayekulipa ni mshamba bado ni kosa.Ni sawa mkuu lakini sio fair kuniita MWIZI
Mwizi anachukua mali ya mtu bila ruksa sasa mimi nilikuwa naiba nini?
Ni kweli mkuu,Tamaa ndio inayowaponza wengi. ila nachompongeza mtoa uzi ni kuwa na msimamo kutotoa hela na kufanikiwa kuwatoka, maana wanakuwaga wamejipanga vilivyo, na wanajua wanachotaka kwako KIPO. kiasi hata usipotaka hela zao ukiingiza tu ubinadamu kujifanya umsaidie tu bila kutaka chochote UMELIA!Utapeli wowote una kanuni moja muhimu: mtu anakuvutia kuwa utapata pato nono kwa kufanya kazi ndogo sana! Ukiishaijua hii kanuni wala hutakaa utapeliwe kirahisi namna hii. Halafu hii aina ya utapeli anayoiongelea mwanzisha thread ni ya siku nyingi mno mno ila version zinabadilika tu! Nakumbuka zamani sana nilishasikia bibi yangu anahadithia babu yangu akiwa kijana alienda mjini akakutana na wale waangusha pochi. Mbele anatangulia mtu anaangusha pochi halafu nyuma anakuja mwenzake ambaye humjui na kukushawishi muichukue mkagawane kilichopo. Matokeo yake ukienda wanakuchenjia uchochoroni na kukunyanganya kila kitu. Sasa mwanzisha thread alifanya kosa kubwa sana kukubali kufuatana nao kwani wangeweza kutumia nguvu kuzichukua zile fedha.
Achana nae kala maarage ya juzi huyoFuta hiyo kauli yakusema mimi ni MWIZI tafadhari mkuu
Lengo langu ni kuwajuza watu yalonisibu ili wachukue tahadhar sababu haya ni maisha ofcorse hakuna anayejua kila kitu.... ila wewe unajiona much know
...ok it's up to you
No,big NO! hawahusiki, japo unaweza ukahisi,au kuna mtu kawachoresha?Me nahisi watu wabank na walee askari huwa wanaelewa mchezo kabisa wootee wanasubirig kamisheni ishu ikitiki
Mie 2015 nilikutana nao posta nimetoka zangu kuchukua dollar zangu kidogo nipo mwendo nawahi kidogo eti dada nina madini kuna mtu kanielekeza huku nimechanganya halafu ni mwanamke tena jimama bila hata aibu nikamgomea akaja mbaba hapo nikaachana nao ile napiga hatua ile kugeuka hata mmoja sikumuona kilichoniokoa nilikuwa nawahi ibada hawa watu jamaniUna bahati sana Mshkuru sana Mungu ingekula kwako
Alishapigwa jamaanguu crdb France corner arusha. Wale askari wapo tukatia timu kuwahoji hawataki hataa kuonyeshaa CCTV za ndani ya bank na menejaa anagoma walipojua sisi kina nani wakawa wapole tukaonyeshwa CCTV na majamaa wakaonekanaa semaa ndo vile walikuwa washatararikaa zaoNo,big NO! hawahusiki, japo unaweza ukahisi,au kuna mtu kawachoresha?
Wale ni kama mbwa, wanaposikia harufu tu mipango inaanzia hapo hapo.
Nachohisi huwa wanafanyia Sana mazoezi kwa kuzingatia mazingira tofauti tofauti!
KabisaSiku zingine jifanye hujui kitu. kaaa kimya tu fanya mambo yako ondoka..wema unaponza sometimes