Jinsi nilivyofedheheka: Ati Niliitwa "MSOMI MALAYA"....

Na huyo mama ndivyo walivyokuwa enzi hizo siku mtoto wa kike akitongozwa anamsimulia mama yake na unakaribishwa na mama mkwe ndio anawaandalia chakula na vinywaji mambo mengi mtaamua wenyewe
 
Na huyo mama ndivyo walivyokuwa enzi hizo siku mtoto wa kike akitongozwa anamsimulia mama yake na unakaribishwa na mama mkwe ndio anawaandalia chakula na vinywaji mambo mengi mtaamua wenyewe

Ndiyo , we wajua... Mtoto wa mwenzio ni wako... Ilikuwa kihivyo..
 
Ilikuwa mwaka 1973,nikiwa sekondari ya serikali,kidato cha pili. Na dhahama hilo lililtokea nikiwa likizo nyumbani Korogwe,Tanga.
Kipindi hicho mtoto kufaulu ililuwa jambo la ujiko sana..hata jamii ya kijijini kwetu ilikuwa ikiniheshimu sana.

Wakati huo ndiyo naanza kubalehe,nilikuwa nampenda sana dada mmoja aliyekuwa akisoma darasa la saba. Shida ni kwamba alikuwa anabanwa sana na familia yake hivyo kuonana ilikuwa taabu ingawa naye alishakubali maombi yangu.

Siku moja ya Jumapili tulikutana kanisani na tulipotoka tukapanga mpango,ambapo aliniambia nimfuate nyumbani kwao usiku wa saa 8! Nalimwuliza kwa nini muda huo akajibu,kuwa kwao huchelewa kulala hadi saa 6 usiku,hivyo saa 8 wanakuwa wameshazama kwenye usingizi mzito.Nikakubaliana naye.

Kwangu kutoka haikuwa shida kwani nilikuwa naishi mabanda ya uani. Nilipofika kwao,nilijibanza karibu na mlango wa ua na ndipo nilipoona mlango wa ua ukifunguliwa taratibu,na mtoto akatoka. Ingawa kulikuwa na gizagiza nilitambua alikuwa amevaa khanga,nami nikamrukia na kumkumbatia kwa mahaba.Akanivuta ndani kwa fujo kidogo,badala ya mahaba,nikashangaa lakini nikahisi itakuwa ni sababu ya woga.

Aliniingiza uani kwao ambako hakukuwa na taa,lakini ghafla taa ziliwashwa! Nilistuka kwani niliona kuna kikundi cha watu pembeni. Halafu nilipomwangalia kwa makini yule niliyedhani ni yule binti,nilitamani kupiga yowe kwani alikuwa ni mama yake mzazi!

"Haya mkwe wangu sema utanipa mahari kiasi gani nikupe binti yangu"alisema mama yule. Nilipotazama kwa makini lile kundi pembeni,nilitamani ardhi ipasuke kwani alikuwa ni baba na mama yangu na kaka yangu mkubwa! Nikiwa nimeduwaa,nilijaribu kuangaza bila mafanikio nikimtafuta yule binti.. Kwanini hakuwepo sikupata majibu.

Lakini baba yangu alikuwa na majibu... Kwani alikuja na kunibana mbavu,akanidunda sana kama mbwa mwizi!ilibidi waliokuwepo pale kuingilia.. Kaka yangu mkubwa naye aliniwasha vibao hevi kama vitatu vya haraka. Nasema hevi maana niliona nyota nyingi sana!

Wakati huu yule binti aliletwa akaamriwa kulala chini,nami nilale chini. Hapo tulitandikwa sana bakora. Wakati huo majirani walishasikia zogo lile na walishajaa uani pale..Tulichapwa na tulilia kama watoto wanaonyonya!

Baada ya adhabu hiyo,baba alichukua tenga na mauchafu-chafu mengine ambayo naamini alikuwa ameyaandaa,akanifunga mwilini na kuniambia twende nyumbani. Wakati huo aliwaomba majirani wanizomee. Nilizomewa njia nzima na huku wengine wakinirushia mchanga! Walikuwa wakiimba "msomi malaya,msomi malaya"
Hadi nafikishwa nyumbani nilikuwa hoi. Kufika asubuhi habari ile ilishaenea karibu kijiji kizima. Kwa kweli nilijisikia fedheha sana.Bahati na likizo ilikuwa ndiyo inaishaisha.

Baadaye nilikuja kujua ni mdogo wa yule binti,ambaye walikuwa hawaelewani,alikuwa amejificha huku akisikiliza mpango wetu,na akaenda kumwambia mama yake,mpaka yakatokea hayo yaliyotokea..

Hata hivyo baada ya kuwa nimeanza kazi,yule binti alikuja kuwa mpenzi wangu..

mh! Inamaana wakati nyumbani kwenu wanatoka hukusikia? Nani aliwataarifu kama na huyu binti nae alisulubiwa?
 
mh! Inamaana wakati nyumbani kwenu wanatoka hukusikia? Nani aliwataarifu kama na huyu binti nae alisulubiwa?

Wakati wanatoka,sikuwaona.
Tulikula nami nikaingia chumbani kwangu kulala. Mama haishiwi shughuli na mara nyingi anakuwa wa mwisho kulala,so haikuwa rahisi kwangu kuzuga nje na kufuatilia nyendo zao.
 
@ Shine...

Binti aliletwa na tukachapwa wote palepale kwao kabla sijarudishwa kwetu kwa staili ya kindumbwendumbwe...
 
Nlikuwa kila nikiiona heading yako nairuka naenda soma vitu vingine lakini baada ya kuifungua nimefarijika,imenikumbusha mbali saaana,sasa baada ya upenzi, ulivuta kabisa au ulionja ukamwaga?
 
Hata kidogo... Hakukuwa na na denda...
Ilikuwa ni environment ya hofu na mfadhaiko. So hug haikupokelewa na ndiyo maana nilidoubt huyo dear wangu kunivuta kwa fujo ndani kwao...

Ilikuwa ndiyo game yangu ya kwanza kama ningefanikisha... Nikafail Vanmedy! Kwa kuwa hakuwa manzi wangu,ndiyo tulikuwa tuanze mahusiano.. nilikuwa sijamzoea kuweza kumtofautisha,na ukichanganya na giza tena,ndiyo hivyo...

Duuh. Hapo nimekupata.. Ndio hivyo tena usipochafuka utajifunzaje.. Ona sasa unakula kiulaiiini lyf goes on.. Ila kisirisiri wazazi wako walifurahi coz waliona mtoto zinachaji/ngangari kidume
 
Nlikuwa kila nikiiona heading yako nairuka naenda soma vitu vingine lakini baada ya kuifungua nimefarijika,imenikumbusha mbali saaana,sasa baada ya upenzi, ulivuta kabisa au ulionja ukamwaga?

Makubaliano si yalifanyika miaka iliyopita?
Kwa hiyo tulifanya tu "umaliziaji" after all,baada ya kukua,mnaakuwa na mitazamo ya aina tofauti... So hatukudumu..
 
Duuh. Hapo nimekupata.. Ndio hivyo tena usipochafuka utajifunzaje.. Ona sasa unakula kiulaiiini lyf goes on.. Ila kisirisiri wazazi wako walifurahi coz waliona mtoto zinachaji/ngangari kidume

Ah.. Nauita huo "umaliziaji",maana kazi ilishafanyika miaka kadhaa nyuma..

Kwa wazazi wa enzi hizo,wala si sifa hata kidogo... Labda wa kileo...
 
Tena ya kweli..

1.Nimeiquote tu

Asant NS...

Sema ni ya kweli... 2.Na ingawa hainihusu mimi,ila ni kisa kilichomtokea huyo baba miaka hiyo.

Hata kidogo... So hug haikupokelewa na ndiyo maana nilidoubt huyo dear wangu kunivuta kwa fujo ndani kwao...

Ilikuwa ndiyo game yangu ya kwanza kama ningefanikisha... . nilikuwa sijamzoea...

sikuwaona. Tulikula nami nikaingia chumbani kwangu kulala. .

Kwa hiyo tulifanya tu "umaliziaji" ... So hatukudumu..

Ah.. Nauita huo "umaliziaji"
Kwanza HONGERA SANA. Kusema kweli hadithi nzuri, nimeisoma mpaka mwisho, lakini imebidi niirudie tena na kudondoa hizo nyekundu.
Kwenye 1 na 2, umeeleza "uliiquote tu" na "haikuhusu wewe"; lakini zilizofuatia zote umeingia ndani ya kiatu cha mhusika na kujibu katika "mtu wa kwanza".
Naomba ufafanuzi juu ya utata huu.
 
pole mgosi,aliishia kuwa mpenzi au ulimwoa kabisa?
Tell me mgosi,itokee leo mwanao afanye haya haya what will be your reaction?
 
Kwanza HONGERA SANA. Kusema kweli hadithi nzuri, nimeisoma mpaka mwisho, lakini imebidi niirudie tena na kudondoa hizo nyekundu.
Kwenye 1 na 2, umeeleza "uliiquote tu" na "haikuhusu wewe"; lakini zilizofuatia zote umeingia ndani ya kiatu cha mhusika na kujibu katika "mtu wa kwanza".
Naomba ufafanuzi juu ya utata huu.

Yeah.. Asante kwa kumakinika kiasi hicho...

Wakati nainukuu hii stori ya huyu baba,nilitafakari mengi... Ili ilete maana,ladha,na ujumbe kwa mhusika...
Njia rahisi niliyoiona ni kuuvaa uhusika wa stori yenyewe.. Ni kweli kuwa nimeiquote na NITAENDELEA kuwapatia stori nyingine za kweli nitakazokuwa naquote na zote ni za watu halisi wa hapa Tanzania..

Nitawapa za vituko mbalimbali walivyokutana navyo watumiaji wa daladala,fedheha nyingine tena za watu mbalimbali...

Hope umenipata MAMMAMIA...
 
pole mgosi,aliishia kuwa mpenzi au ulimwoa kabisa?
Tell me mgosi,itokee leo mwanao afanye haya haya what will be your reaction?

Hakuolewa hata kidogo nami! Baada ya miaka kupita,tukakutana,na tukaufanya huo ninaouita "umaliziaji".. Kiukweli haikuwa natural love,na hakukuwa na zile feelings zilizokuwepo utotoni...

Mimi naheshimu sana nidhamu... Na mtoto anayekosea huadabishwa.. Akiadabishwa si kwamba kaonewa,la hasha,ni kumrudisha kwenye njia na asithubutu kukosea tena...
Huoni kama mimi sasa ni mtu bora,si kwa familia yangu iliyonilea vema tu,bali ni raia mwema wa nchi yangu pia..
 
Back
Top Bottom