Jinsi Mwanafunzi wa Form Six Anaingiza Pesa Mtandaoni Kupitia Freelancing

Jinsi Mwanafunzi wa Form Six Anaingiza Pesa Mtandaoni Kupitia Freelancing

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641

Jinsi Mwanafunzi wa Form Six Anaingiza Pesa Mtandaoni Kupitia Freelancing​

1*c-Oql6DsTPgl4CkZM6BH_A.jpeg

Wakati vijana wengi waliomaliza kidato cha sita wakisubiri majibu ya chuo au kutafuta “kazi ya kuajiriwa,” kijana mmoja kutoka Mwanza aliamua kuchukua njia za tofauti.

Jina lake ni Festo

kijana mnyenyekevu, mpole lakini mwenye ndoto kubwa kichwani. Alimaliza kidato cha sita mwaka 2023 katika shule ya sekondari ya serikali (Nsumba boys), akiwa na passion kubwa ya kuwa graphics designer na kuwa video editor.

Wakati wengine wakipumzika wakisubiri matokeo ya NECTA, Brian alianza kutafuta njia ya kaka yake kujifunza digital skills na kutafuta pesa.

Aligunduaje Freelancing?​

Akiwa anaangalia YouTube video moja ya “Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kwa Kuuza Ujuzi Wako,” aligundua kuwa kazi za video editing na 3D animation zinahitajika sana duniani.

Hakusubiri — alianza kujifunza zaidi kupitia YouTube tutorials, mitandao kama Skillshare na Udemy.

Baada ya wiki tatu tu za kujifunza, Brian alitengeneza portfolio yake ya kwanza kupitia video fupi alizokuwa anatengeneza kipindi anajifunza.

Alianza Wapi Kufanya Kazi?​

Aliingia kwenye mitandao ya freelancers kama:

  • Fiverr
  • Upwork
  • PeoplePerHour
  • Behance (kwa kuonyesha kazi zake)
Akaweka profile nzuri, akaweka baadhi ya kazi zake alizotengeneza bure kama mfano.

Kazi ya kwanza aliyopata ilikuwa ya mzungu kutoka Canada aliyemlipa $20 kwa video ya sekunde 30 ya 3D intro kwa YouTube channel.

Kumbuka — hiyo ilikuwa mara ya kwanza kupata pesa ya mtandaoni.

Mapato Yalianza Kuongezeka​

Baada ya hapo, alianza kupata referrals kutoka kwa wateja wake. Alijifunza jinsi ya kuandika proposal nzuri, jinsi ya kujieleza kwa client, na jinsi ya kukuza jina lake kama freelancer anayeaminika.

Mwezi wake wa pili, alipata jumla ya $300 (zaidi ya TZS 750,000) kutoka kwa kazi mbalimbali video editing, animation, intros, na 3D mockups.

Alianza kusaidia wazazi wake, akanunua simu mpya, laptop na kujiwekea akiba ya kwenda chuo (Ila alihairisha kwenda chuo aliona pesa ni tamu sana na anajua kuitafuta). alienda mwaka uliofata

Alipoenda Chuo, Alikuwa Tayari ni Mjasiriamali​

Baada ya kupangiwa chuo (CBE — Dar es Salaam), Festoalienda akiwa tofauti na wengi: tayari alikuwa na laptop yake, fedha ya kujikimu na hata aliweza kusaidia wanafunzi wenzake kwa kuwafundisha freelancing na video editing.

Brian hakusubiri ajira. Alijiajiri kupitia freelancing na kuanza maisha akiwa na uhuru wa kifedha.

Leo hii kuna vijana wengi wana talenti kubwa sana lakini wanazikalia tu wakisubiri ajira ya serikalini au nafasi ya chuo.

Ukweli ni kwamba, mtandao umefungua milango ya pesa kwa mtu yeyote mwenye simu au laptop na ujuzi hata kidogo.

festo hakusubiri “tangazo la kazi” alijitangazia mwenyewe kupitia kazi zake mtandaoni.

“Kama unajua kufanya kitu chochote hata kuchora, kuandika, kutengeneza video, au hata kutafsiri lugha unaweza kuanza kuingiza pesa kupitia freelancing,” anasema Brian.
Sasa ni zamu yako. Usisubiri ajira. Jifunze, jitangaze, fanya kazi zako kwa bidii.

Dunia ya freelancing iko wazi kwa wote ukiwa na simu yako tu na akili ya kutafuta, utashangaa ulipo mwaka mmoja kutoka leo.
 
JFISS ( Jamii forums intelligence secret services)
Imebaini Hii ni simulizi ya kubuni haina uhalisia.
Festo na Brian ni akina nani?
 
Back
Top Bottom