Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,429
Sawa mkuu. Inawezekana na mimi nimeshaathiriwa na tatizo la msingi linalozungumziwa kwenyye hoja ya msingi maana limeshawaathiri wengi.Mkuu kwema? Mkuu una hoja nzuri sana lakini hujui namna ya kuwasilisha hoja kabisa. Uandishi wako haushawishi hata kidogo mkuu. You have to improve your communication skills.
Ahsante sana.
You are right brother. Also ,undoubtedly you're a decent man. Just wanted to see your reaction.Sawa mkuu. Inawezekana na mimi nimeshaathiriwa na tatizo la msingi linalozungumziwa kwenyye hoja ya msingi maana limeshawaathiri wengi.
In summary, tunajenga aina ya siasa inayochochea utamaduni wa kutopenda kupewa changamoto, kutopenda kukosolewa au kujifunza. Matokeo yake mbele ya safari tutatukwa na kizazi cha wanasiasa (ambao kimsingi ndio viongozi) wasio na fikra madhubuti , na sio kwamba watapenda kuwa hivyo, bali itakuwa ni matokeo ya mazingira.
Ni vyema tukajisahihisha.
Nilifundishwa utulivu na mwalimu wangu mmoja. Kila ninachoaandika anasema 'Hamna kitu, nenda kaandike tena' nikimuuliza usahihi unapaswa kuwa vipi ananiambia 'nenda kafikiri zaidi uniletee majibu ya maana hapa' nikawa nakasirika weee lakini hatimaye nikagundua kuwa kweli kuna vitu vipya najifunza.You are right brother. Also ,undoubtedly you're a decent man. Just wanted to see your reaction.
Ni changamoto mkuu, ila inaweza kuwa ni sehemu ya madhara ya yaliyoelezwa kwenye mada ya msingi. Ni muhimu kuwa na mkakati mpana wa kitaifa kujenga kizazi kinachofikiri 'Critical thinking generation' na tunaweza kufanya hivyo kwa kujenga utamaduni wa ku intertain challenges. Kinyume na hapo ni balaa ndugu yangu.Ni vema ungempa intro ya uandishi mzur na bora kuliko kulaumu na kukimbia
Kabisa uko sahihiNi changamoto mkuu, ila inaweza kuwa ni sehemu ya madhara ya yaliyoelezwa kwenye mada ya msingi. Ni muhimu kuwa na mkakati mpana wa kitaifa kujenga kizazi kinachofikiri 'Critical thinking generation' na tunaweza kufanya hivyo kwa kujenga utamaduni wa ku intertain challenges. Kinyume na hapo ni balaa ndugu yangu.
Ni kweli unachosema, tatizo mlaji hula chakula anacholetewa mezani, wakileta hoja fikirishi zitajadiliwa, bahati mbaya mengi yanayoletwa mezani huwa hayahitaji akili kubwa kufikiria coz majibu yake huwa ni yale yale, unadhani kwanini thread nyingi unazoleta huwa zinakosa wachangiaji wengi? tatizo unawaletea chakula kigumu kutafuna wakati upande wa pili huwa kuna keki wanajua hata wakimumunya watameza tu.Mkuu denooJ angalizo lako ni la msingi sana. Zaidi ya hapo ni kwamba kwa kawaida kama mtu hupati changamoto kwenye hoja unazotoa, kidogo kidogo una sees kufikiri. Ujue kufikiri ni kazi ngumu na inayosababisha disconfort, kwa hiyo bila push factors, hali hiyo lazima itokeee tu. Kwa hiyo muhimu ni kila mmoja wetu kujitahidi awezavyo kubalilia culture ya ku entertain challanges na kujifunza
Very good, umejenga hoja yako vizuri sanaKwa mujibu wa mfumo wetu, Wanasiasa ndio viongozi wa nchi ambapo kiongozi ndio hutoa muelekeo wa wapi pa kwenda au kutokwenda na ili iweje. Kwa mantiki hiyo, ili kupunguza ‘chances’ za kupotea, ni jambo la muhimu sana wanasiasa wetu wawe na uwezo mkubwa sana wa kufikiri.
Uwezo mkubwa wa kufikiri huchangiwa na mambo makubwa matatu. Changamoto, Ukosolewaji na kujifunza (Challenges, criticism and learning). Mtu yoyote mwenye akili timamu, akiyapitia hayo, lazima uwezo wake wa kufikiri uimarike.
Hata mtu akazaliwa akiwa na akili kiasi gani, asipokutana na changamoto za kutosha, mawazo yake kukoselewa sana na pia akajifunza sana, baada ya muda atakuwa ‘Very low’ na kinyume chake, sio kwa sababu ni mtu mbaya bali kwa sababu ya mazingira.
Sasa basi, kwa muelekeo wa siasa zetu, kuna kitu kinajengeka kwa kasi sana. Kutopenda kuwa ‘Challenged’ Kutopenda ‘kukosolewa’ na kupuuza ‘kujifunza’ (kusoma). Yaani mtu akipewa challenge anakasirika , akikosolewa anafanya uadui, akiona mtu amesoma, au anasoma utasikia ‘ kasoma lakini hana mchango kwa taifa’(maana yake tuna discourage wanasiasa/viongozi kujifunza).
Misuli ili ikue lazima kunyanyua vitu vizito, na kwa kadiri unavyonyanyua vitu vizito ndio misuli hukuwa zaidi na kinyume chake. Vile vile uwezo wa kufikiri; kwa kadiri unavyokumbana na ‘challenges’, ‘critiscims’ na kujifunza ndivyo uwezo wa kufikiri unavyokuwa na kinyume chake.
Nitoe mifano michache, Ukiwa na mtoto, kila anachotaka anapata bila kuhojiwa, unaandaa mtoto ambaye uwezo wake wa kufikiri utakuwa ‘very low’ na usipokuwepo atakuwa amekwisha. Kama Toyota kwa mfano wasingekuwa ‘challenged’ na Nissan n.k wasingekuja na uvumbuzi mpya kila siku. N.k.
Kwa hiyo hata binadamu hata awe mzuri vipi, asipokuwa ‘challenged & Criticized intensively’ atakuwa ‘very low’ hii ni kanuni tu ya kimaumbile. Hata wewe unayesoma hapa, kama vitu unavyofikiri, kusema na kufanya hakuna watu wanaoku ‘challenge’ na kuku ‘criticize seriously’, utakuwa ‘very low’ tu. Yaani kila unachosema watu ‘yes’ ukikohoa walioko karibu yako ‘wanasema umekohoa vizuri’ n.k lazima utaingia kwenye comfort zone na utapotea tu.
Wito wangu;
Ni muhimu sana kama taifa tukajenga mazingira ya kisiasa ambayo yatachochea kuongeza uwezo wa wanasiasa/viongozi kufikiri zaidi na zaidi. Mazingira hayo si mengine bali kujingea utamaduni wa kukubali kupewa changamoto, kuokosolewa, kujifunza/kutafuta elimu.
Kwa mantiki hiyo, sio tu kwamba tunapaswa kujijengea utamaduni wakukubali kukosolewa (japo kwa kujilazimisha kama mtu anavyojilazimisha kuamka asubuhi) bali pia tunatakiwa ku ‘promote’ utamaduni huo. Hiyo ndio njia pekee itakayotusaidia kuwa na wanasiasa na hatimaye viongozi wenye fikra madhubuti zaidi leo kuliko jana na kesho kuliko leo. Vinginevyo, tunatakuwa tumeemua kujielekeza shimoni wenyewe kwa hiyari yetu.
Aidha, watu wanaotu challenge na kutukosoa au kutuelimisha; hatupaswi kuwachukulia kama maadui badi wadau wa maendeleo, kwani wanatuwezesha tufikiri zaidi na hivyo kufanya vyema zaidi na kuwa wabunifu.
Kupanga ni kuchagua, la muhimu ni kuchagua ukijua unachagua nini na ili iwe nini.
Uko sahihi sana mkuu. Kuna suala pia la 'incentives'. Kama unajua ukiwa na mawaziri ya maana, ukisoma na kujielimisha na.k sio tu kwamba hutokubalika kulingana na mfumo uliopo bali pia hutopata ' incentives' lakini ukiwa mkurupukaji kwa mfano unachafu watu wengine, kwanza unapata support na pili unapata incentives, kwa vyovyote vile mazingira hayo yatawasukuma wengi kama sio wote kuchukua option ya pili. Ndio maana nasema ni mfumo fulani ambao pia unaweza kuwa kinyume chakeNi kweli unachosema, tatizo mlaji hula chakula anacholetewa mezani, wakileta hoja fikirishi zitajadiliwa, bahati mbaya mengi yanayoletwa mezani huwa hayahitaji akili kubwa kufikiria coz majibu yake huwa ni yale yale, unadhani kwanini thread nyingi unazoleta huwa zinakosa wachangiaji wengi? tatizo unawaletea chakula kigumu kutafuna wakati upande wa pili huwa kuna keki wanajua hata wakimumunya watameza tu.