Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,427
Uwezo mkubwa wa kufikiri huchangiwa na mambo makubwa matatu. Changamoto, Ukosolewaji na kujifunza (Challenges, criticism and learning). Mtu yoyote mwenye akili timamu, akiyapitia hayo, lazima uwezo wake wa kufikiri uimarike.
Hata mtu akazaliwa akiwa na akili kiasi gani, asipokutana na changamoto za kutosha, mawazo yake kukoselewa sana na pia akajifunza sana, baada ya muda atakuwa ‘Very low’ na kinyume chake, sio kwa sababu ni mtu mbaya bali kwa sababu ya mazingira.
Sasa basi, kwa muelekeo wa siasa zetu, kuna kitu kinajengeka kwa kasi sana. Kutopenda kuwa ‘Challenged’ Kutopenda ‘kukosolewa’ na kupuuza ‘kujifunza’ (kusoma). Yaani mtu akipewa challenge anakasirika , akikosolewa anafanya uadui, akiona mtu amesoma, au anasoma utasikia ‘ kasoma lakini hana mchango kwa taifa’(maana yake tuna discourage wanasiasa/viongozi kujifunza).
Misuli ili ikue lazima kunyanyua vitu vizito, na kwa kadiri unavyonyanyua vitu vizito ndio misuli hukuwa zaidi na kinyume chake. Vile vile uwezo wa kufikiri; kwa kadiri unavyokumbana na ‘challenges’, ‘critiscims’ na kujifunza ndivyo uwezo wa kufikiri unavyokuwa na kinyume chake.
Nitoe mifano michache, Ukiwa na mtoto, kila anachotaka anapata bila kuhojiwa, unaandaa mtoto ambaye uwezo wake wa kufikiri utakuwa ‘very low’ na usipokuwepo atakuwa amekwisha. Kama Toyota kwa mfano wasingekuwa ‘challenged’ na Nissan n.k wasingekuja na uvumbuzi mpya kila siku. N.k.
Kwa hiyo hata binadamu hata awe mzuri vipi, asipokuwa ‘challenged & Criticized intensively’ atakuwa ‘very low’ hii ni kanuni tu ya kimaumbile. Hata wewe unayesoma hapa, kama vitu unavyofikiri, kusema na kufanya hakuna watu wanaoku ‘challenge’ na kuku ‘criticize seriously’, utakuwa ‘very low’ tu. Yaani kila unachosema watu ‘yes’ ukikohoa walioko karibu yako ‘wanasema umekohoa vizuri’ n.k lazima utaingia kwenye comfort zone na utapotea tu.
Wito wangu;
Ni muhimu sana kama taifa tukajenga mazingira ya kisiasa ambayo yatachochea kuongeza uwezo wa wanasiasa/viongozi kufikiri zaidi na zaidi. Mazingira hayo si mengine bali kujingea utamaduni wa kukubali kupewa changamoto, kuokosolewa, kujifunza/kutafuta elimu.
Kwa mantiki hiyo, sio tu kwamba tunapaswa kujijengea utamaduni wakukubali kukosolewa (japo kwa kujilazimisha kama mtu anavyojilazimisha kuamka asubuhi) bali pia tunatakiwa ku ‘promote’ utamaduni huo. Hiyo ndio njia pekee itakayotusaidia kuwa na wanasiasa na hatimaye viongozi wenye fikra madhubuti zaidi leo kuliko jana na kesho kuliko leo. Vinginevyo, tunatakuwa tumeemua kujielekeza shimoni wenyewe kwa hiyari yetu.
Aidha, watu wanaotu challenge na kutukosoa au kutuelimisha; hatupaswi kuwachukulia kama maadui badi wadau wa maendeleo, kwani wanatuwezesha tufikiri zaidi na hivyo kufanya vyema zaidi na kuwa wabunifu.
Kupanga ni kuchagua, la muhimu ni kuchagua ukijua unachagua nini na ili iwe nini.