Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,330
- 33,951
Baada ya Mapinduzi (matukufu?) ya Zanzibar Mwaka 1964, chama cha ASP kikapiga marufuku vyama vingine vya siasa na kuharamisha viongozi wake. Ukiwa Zanzibar ilikuwa ama uwe ASP au uwe adui wa Mapinduzi. Kwa ivo kila mtu aliyetaka kufanya siasa Zanzibar ilibidi ajiunge na ASP ili afanye siasa na awe salama. Hapa kuna kumbukizi ya utata kwa watu kama Kina Kassim Hanga walikufaje na Salim Ahmed Salim ambaye ililazimika apewe Ubalozi wa Tanzania ili kumnusuru na hisia dhidi yake kwamba yeye ni Hizbu.
Tanganyika nako baada ya uchaguzi wa vyama vingi Mwaka 1965, TANU ilipiga marufuku vyama vingine vya siasa na kubakia peke yake. Hapo napo ndiyo kwenye ile misukosuko iliyowapata kina Abdalah Fundikira na baadhi ya wenzake. Kulikuwa kuna kundi kubwa sana ndani ya TANU ambalo lilikuwa halikubaliani na TANU lakini kwa kuwa vyama vingine vilikuwa vimepigwa marufuku, kundi hilo la watu ilibidi kuvumilia kubaki TANU.
TANU na ASP ziliunganisha nchi ya Tanganyika na Zanzibar lakini ilishindikana kuunganisha vyama vyao mpaka miaka 13 baadae walipoiunganisha ASP na TANU na kuzaliwa chama cha Mapinduzi-CCM. CCM ilirithi tabia ya TANU na ASP ya kutokutaka mawazo tofauti na wao. Na hapo ndipo walipoanzisha falsafa ya chama kushika hatamu.
Chama kushika hatamu ulikuwa ni mfumo kwa wananchi kutii bila ya kuuliza chochote dhidi ya mambo yote yanayotendwa na kuamuliwa na viongozi. Hali hiyo ndiyo imedumaza uwezo wetu watanzania kwenye kutumia akili zetu kujenga hoja.
Mtanzania anaweza kuwa na maneno meeengi lakini inakuwa taabu kwa msikilizaji au msomaji kujua msemaji anataka kusema nini. Kwa kweli watanzania wengi wamedumazwa uwezo wao wa kutumia akili zao kwenye kufikiri na kujenga hoja.
Kujenga hoja kunahitaji mantiki na mantiki haiwezi kujengwa na watu wasiotumia mbongo zao kufikiri kwa uhuru. Leo hii wanaofikiri kwa uhuru wameanza kuchukiwa kama ni maadui kwa kuwa eti ni kwa nini wao wanafikiri tofauti na viongozi, Ndipo ule msemo wa " Wewe unajua zaidi kuliko kiongozi" unapoibuka.
Tupo sehemu mbaya sana kama taifa. Hatuwezi kupiga hatua nzuri ya kimaendeleo kama hatutoruhusu mbongo zetu kufanya kazi kwa uhuru na kwa tafakuri jadidi. Matokeo yake mtu ana shahada tatu anafukuzwa ukuu wa Mkoa anaanza kutubu kama mwendawazimu mbele ya Kamera. Au ni sawa na Professa ambaye kwa hofu anamwita Rais "Mheshimiwa Mungu".