Jinsi mkoa wa Kagera unavyotengwa na Serikali

Jinsi mkoa wa Kagera unavyotengwa na Serikali

Hicho kilimo cha wa South Korea, ndo maendeleo, tangu ichimbwe nikeli, kule KABANGA - nikel, tangu uhuru, Ngara, imendelezwa? Mpaka leo mdai wanatafiti zaidi ya miaka hamsini. Uchungu mwana ajuye mzazi, siyo mkunga!
 
Naomba watu Wa Kagera tuwahamishie mkoa Wa Dodoma halafu Wa Dodoma waende Kagera. Maana Dodoma inakumbukwa sana na serikali haijatengwa.
 
Nashuka kama MVUA YA RADI, niongee kwa vitendo kama UPEPO WA KISURISURI hakika tumechoka natena tumecho haswa, mkoa wetu wa kagera sasa hatuheshimiwi tena zimebakia dharau na kebehi za KUTUITA INSHOMILE na kutusifia kwa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa eti mkoa wa wasomi[emoji36][emoji36][emoji36][emoji36][emoji27][emoji27][emoji27].

Ujinga huhu uliratibiwa tangu zamani na kuturudisha nyuma kimaendeleo hakika nasema kabisa tuamke, wahaya tuliojuana kwa stori za senene maofisini tujuani tena, watu tuliokumbukana kwa kukutana ktk safari za meli yetu pendwa VICTORIA hatukumbukani mkoa kagera ukiwa na wilaya kongwe kama MULEBA, NGARA, BIHARAMULO, BUKOBA MJINI NA KARAGWE nyumbani kwetu, kwa kutaja chache tulikuwa maarufu kwa kuzalisha kahawa, ndizi na wasomi waliotukuka, sasa hii legacy ilienda wapi???

Nasema kwa masikitiko kabisa mh. Magufuri tumekutunza na kukulea vyema unakumbuka ulipokuja na tukakumbukana kwa story za MZILANKENDE, sasa tuseme dhaihiri tunahitaji legacy yetu irudi mahala pake. Karagwe iliwahi kuwa wilaya bora kabisa kimaendeleo hivi leo umasikini umatalaki na kukita mizizi na kuzaliana hakika mkoa wetu uko pembezoni mwa mwa nchi na kimaendelei umewekwa pembezoni kusema kweli.

Wazawa wa mkoa kagera tumechangia damu za jamii ya watu KITUSI na WAHUTU, hivyo ni watu wenye uwezo wa kiakili sana watu wengi walishangaa kwa kuwa na wasomi wengi hii ilitokana na jamii ya watu hawa kula nyama na maziwa kwa wingi sababu tulikuwa wafugaji sana, nyerere analitambua vyema. Sasa hivi hayo maisha yamekoma kwasasa kula nyama ni ANASA mno.

Namaliza kwa kusema sasa tumeamka kwa silaha zote za elimu, kuwa mkoa wa pembezoni, fursa za kimaendeleo(Ziwa, madini, mifugo, ardhi bora, mipaka na nchi za jirani zaidi ya nne na mapori na vivutio vya utalii) hamtaki kutukumbuka tuacheni tujitawale.

Nitoe lawama zetu kwa wabunge wa mkoa kagera hakika mumelala tena usingizi wa pono kabisa huku maendeleo ya KAGERA yakiporomoka kwa kasi ya ajabu. Hakuna mkoa utakuwa na watu wengi ughaibuni (diaspora) kutuzidi wanaweza kutufuata kwa mbali wachaga, ambao wengi wao walio ughaibuni ni wamissionari hivyo tukijiongeza tutainyanyua tena legacy ya kagera.

Kwa pamoja tuseme imetosha KGERA KWANZA mikoa mingine badae.
 
Halafu Mi nahisi nyie sio watanzania na hamuijui Tanzania. Tatizo la Kagera ni moja tu , hampendi kubadilika, ni kahawa na ndizi tu.

Ila kwenu kuzuri aisee kijani kibichi mwaka mzima Ardhi yenye rutuba, ziwa Victoria, senene, fursa za Kampala nk. Hakuna nyumba mbovu mbovu kuanzia kyaka mpaka muleba, nshamba, kamachumu, msiililie serikali watu ambao toka 1930's mlishakuwa na shule ushirika imara na tajiri , diaspora Wa kutosha. Nadhani tuwape mkoa mmoja ulioendelezwa na serikali mchague mkaishi.
 
nawashangaa,kimkoa chao hakina asset yoyote ya maana,hawafanyi kaz uvivu tu wanataka maendeleo wakat hata ubunifu wa kuanzsha daladala pale bukba wameshindwa imagine mji wa bkb haina daladala
Kwani daladala ndo kipimo cha maendeleo mbona kuna miji mi kubwa tu kama Jakarta,Kampala,kisumu,manila nk usafiri wa mjini ni pikipiki tu.halafu hujui faida za pikipiki wew .vile vipanya vya moshi unakaa wee mpaka ijae hata nikupoteza mda ni tofauti na mwanza au dar.kwa bukoba bodaboda ni faster na nyingi na zinachangamsha mji na isitoshe daladala zipo nitakuletea stendi yake ingawa mfumo wake wa usafirishaji ni tofauti na wa tz ni kama wa Kampala na Kigali kama ulishafika
 
Hazipo tena nyie Wa ajabu sana zile ghorofa mnazojenga wanaishi popo. Halafu mnalalamikaa au mnataka tuwatambue jinsi mlivyoendelea ?
Hapana kuna vitu havitendwi kwenye mkoa huu hasa public mfano meli miaka ishirini imepita hakuna meli ya uhakika Victoria yenyewe mbinde wakati wanananunua madege ambayo mengi hawayapandi kwanini tusijitenge
 
Wahaya wanamaliza wenyewe kumbuka mradi wa yule mayor na kagasheki, mayor katafuta Mwekezaji wa kuendelea maeneo mbunge kagasheki anapinga mpaka mradi ukafa, world bank walitaka kutoa pesa ya kuweka mitandao wa maji na barabara zote Mjini ugomvi wa madiwani hawakutoa maamuzi mpaka WB wakafutilia mbali.
Leo mnaibuka kulaumu serikali wakati wachawi wa maendeleo ni nyie wenyewe.
Hata uwanja wa Ndege ni JK kusimamia ndio ukatekelezwa lakini walishaanza kugombana sehemu ya kujenga
Hawa jamaa wana matatizo gani ? sasa usomi wao wanautumiaje..
 
Hapana kuna vitu havitendwi kwenye mkoa huu hasa public mfano meli miaka ishirini imepita hakuna meli ya uhakika Victoria yenyewe mbinde wakati wanananunua madege ambayo mengi hawayapandi kwanini tusijitenge
Acha ni niiii, mama tibaijuka anashindwa kununua boti kama ya bakhresa? mafuruki anashindwa kuchukua loan akaunda meli pale Mwanza. Shida zitasafirisha nini?, hamzalishi ndugu zenu kule wanategemea muwatumie hela ili waishi, uvivu umewazidi. Msingekuwa vizuri kichwani mngepata sana shida .
 
Hivi ule mpango wa kuifanya kagera kuwa dubai umefikia wapi?
 
Mtoa mada ana point nzur kwenye mkoa wa kagera kutengwa na serikali ingawa wengi wanambeza kwa sababu wanazozijua wao labda ndo walewale wanaohusika na hiki alichokisema mwandishi
Kwanza kagera hakuna institution yoyote ya maana ya serikali. Leo hii ukienda kagera hamna hata chuo cha veta utafikiri ni mkoa ulioanza juz
Pili kila siku wanakagera wanalilia meli ila serikali imekuwa haisikii hiki kilio. Juz kwenye gazeti la mwananchi wameandika miaka 22 baada ya mv bukoba kuzama bado hanna mbadala wake. Can you imagine miaka 22 imepita!!!!!
Ni mambo mengi ambayo yako wazi yanayoonesha kwamba kuna kitu behind. Ni busara kujitafakar mlifikiri haya ni ya mwandishi tu yeye kaandika mawazo ya wanakagera wengi ambao hawaridhishwi na mwenendo wa serikali
 
Kwanza nakuunga mkono katika hii move. Tuko tayari na nilishawahi kuandika the move has just began, kinachohitajika ni kukaa chini na kuona namna nzuri ya akili ili kufikia malengo yetu.

Sie kutoka kule ndo tunajua hili tunalolisema na wala hatutahangaika na mbinu zozote kutoka kwa wenzetu mikoa mingine.

Nakucheki mda si mrefu tuongee ...Aluta continua
 
Kwanza nakuunga mkono katika hii move. Tuko tayari na nilishawahi kuandika the move has just began, kinachohitajika ni kukaa chini na kuona namna nzuri ya akili ili kufikia malengo yetu.

Sie kutoka kule ndo tunajua hili tunalolisema na wala hatutahangaika na mbinu zozote kutoka kwa wenzetu mikoa mingine.

Nakucheki mda si mrefu tuongee ...Aluta continua
 
Simple sana ..alafu siku zote tambua, tukiongea hatuongei ili wewe kamjusi utende. Huu ujumbe hauna uhusiano kabisa na familia yako hata kidogo.

So far so good, mkoa hauna la kuchangia kwa Taifa lenu wekeni wazi ili wenye kuuhitaji watangaze nia, ukitaka kujua nani mbaya wako mwache mkeo. Wakati Tz inauona Kagera mzigo wenzetu wako hawalali wanatamani uwe wao.

Tulieni hivyo hivyo tumalize kazi kwanza ili tuwapunguzie mashuzi
Mi sijui huyo MTU ana tatizo gani yaani anachukia wahaya kama nini yaani ye ana tabia za kichawi dhidi yao .anaumia sana akisikia wahaya wanamzidi mbali
 
Kuna special move nilitaka niianzishe lakini niliona ina madhara kidogo.

Uliwahi kujiuliza maswali haya ya msingi?

1. Kwanini Zanzibar Ana special treatment? Anapewa hata ambavyo hakusitahili

2. Kwanini jimbo la Catalonia nchini Spain linapewa special treatment kuliko malaga, au sevilla au kwingine?

3. Kwanini Mombassa ndani ya Kenya inapewa special treatment kuliko nakuru, kisumu, lamu na kwingine?

4. Kwanini crimea inapewa au ilikuwa inapewa special treatment na Ukraine kuliko majimbo kama dnipropetrovisk, baglovshchensk, luhansk au Donestk,

Sababu ni kwamba zilitisha kujitenga na nchi hizo

Mawazo yangu ni kwamba, tukiweka mezani sababu ya msingi ya Kagera kutaka nchi yetu kama sisi japo tunajua hatutapata ila

Tukaandika barua UN, AU na Marekani kuomba seat kwenye UN na kuomba nchi yetu,

Zile sababu tutakazotaja serikali itazishughulikia mara moja, pia kimataifa tutapata wafuasi na watu hasa wazungu wanafiki wa kutupa misaada ili tujitenge vema, hii itasaidia ku alert TZ na serikali kwamba hawa watu

Wanataka nao reli ifike

Wanataka vyuo vya serikali huko

Wanataka kuunganishwa na wengine biashara kupitia bulk transportation means of cargo kama meli na reli siyo lami tu,

Watajua kwamba restrictions za kufanya biashara na nchi jirani si nzuri hasa wana Kagera wanapokatazwa kufanya na Uganda

Watajua kwamba kuna tourism sites ambazo serikali imeshindwa ama kwa makusudi au uzembe kuziendeleza,

Ni mengi sana,

Pia Tunabaguliwa muda huu kama hamjui

Ni wazo zuri sana. Naunga mkono. Wazo hilo liratibiwe kisomi. Wala wazo si la uasi bali lahitaji akili kubwa kulichakata na kuliweka kwenye vitendo. Suala la kupambana bila kuonesha njia ya mapambano na yupi unayepambana naye ni kama halipo au limekufa. Kwa wazo langu adui wa Kagera anaonekana. La msingi ni mkakati wa kisomi kwa kuandikia ili kuyaleta mapinduzi. Kubwa ni kuitangaza Kagera wote wakajua halafu mapambano yakaanza.

Wapo wasomi (uzamili na uzamivu) ambao wanaweza kuonesha njia japo baadhi yao wakiwa waoga tunaweka pembeni. Si lazima mabadiliko waletwe na wasomi tu japo mchango wao mkubwa sana. Hilo suala lilitokea Mtwara ingawa halikuratibiwa kisomi. Hivi sasa ukimgusa mtu wa Kigoma wote wanaamka, Kagera wapo tu. Mliona hata kwenye tetemeko serikali ilibaki kufanya danadana. Dr Kahangwa alijitahidi ila alikuwa peke yake japo naye alikuwa kwenye tafiti na si hamasa mbali na kuwa mwathirika mkubwa. Wasomi wenzake, viongozi kimya hata kutoa matamko dhidi ya mamlaka hakuna kabisa. Misaada yote ilipotea.

Nina uwezo na nina jua jinsi ya kuratibu suala ili.

Nasema hivi

Sidhani kama wote wataguswa na kuchangia changia post hii, ni wakazi na wenyeji wa mkoa wa kagera watakaoguswa sana!! Wa Kagera atayebisha haelewi Au aidha wamesoma sana au ni mbumbumbu wa kufikiri, kunghamua, kutathimini, na kulinganisha kagera ya sasa na mikoa mingine inavyo kimbia kimaendeleo.

Kuna mikoa ukimaliza miezi 6 tu haupo ukienda unakuta mabadiliko ya kusonga mbele kimaendeleo!! Lkn Kagera hakuna kitu, nitakupa, vitu vinavyo letã changes za haraka linganisha na kagera yetu, ujenzi wa vyuo mbalimbali, miundo mbinu bora, masoko ya kisasa, stend za kisasa, bandari na usafirishaji kwa njia ya maji, reli na hanga, soko lá mazao ya biashara na chakula, ugunduzi na uchimbaji wa madini, uwekezaji wa miradi mikubwa na viwanda, kujituma kwa wakazi husika bila kubagua kazi, supporting ya serikali na viongozi, uwanzishwaji wa kilimo na ufugaji wa kisasa, je kati ya haya ni yapi angalau tunaweza kujinadi kuwa tumepiga hatua? Kama sio sisi wenyewe kuchambana na kuishia kwenye umasikini wa kipato na hakili, ebu tuwe wamoja kwa hoja zenye manufaa kwetu wote.
Ni PM tuongee mkuu make nimejaribu nimekwama ...fanya hivyo tuongee
 
Napinga hoja hii.
Kukwama na kutoendelea kwa maendeleo Kagera chanzo no moja ni wanakagera wenyewe wala siyo serikali .
Nitaadika kirefu baadaye.
Byabato
+255754527358
Karibu uandike na hatutegemei usiandike, wewe ni mwanahabari na ulitakiwa kuwa umeandika siku nyingi kuliko kusubiri ukurupushwe huko uliko.

Nasubiri ukiandika ntakujibu na ukituelewa karibu, usipotuelewa pia sawa. Kupanga ni kuchagua na si lazima tukubaliane 100% ila kupinga kwako hakutakuwa na lolote na project yetu na mkoa wetu
 
Wale tulio tayari tuwasiliane ili tutengeneze mikakati na ajenda, we need to be so focused.

We have power and vision
 
Wale tulio tayari tuwasiliane ili tutengeneze mikakati na ajenda, we need to be so focused.

We have power and vision
Hivi huo umoja mtautoa wapi? Si mtasilitiana kama kawaida yenu?
 
Kwanza Ni muhimu kubaini matatizo Kama kweli ndio yaliyotukwamisha au la
yaliyotukwamisha ndio tu deal nayo.
Niongeze mtizamo kweli Kagera ni bado ya wanaKagera?
Nilipata story kwamba aliyekuwa mkuu wa mkoa Masawe alikusanya wachaga wote waliokuwawafanyakazi Kagera na kuwahawia mashamba Kyerwa wilaya mpya Mara baada ya kuanzisha.Tunaweza kuwa tunachanganya wanaKagera kuwa bado Ni wahaya kumbe sio kweli Tena Kyerwa tayari Ni wachaga,mtoa hoja pia taambua wanyarwanda walivamia Karagwe na muleba.
Kama Ni hivyo tujue jinsi ya kuendesha huu mjadala.
Rai yangu mawazo ya kila mtu,solution haitoki unapoishi ila kwenye bongo zetu bila kujali unaishi wapi.
Kwa sababu wachaga ni wakenya...
We akili zako sijui zinatokea wapi.... Nadhan huna kazi ya maana kila mara kujamba ujinga Tu.
 
Mi naunga mkono hoja na vuguvugu hapa bukoba limeanza serikali isipotambua haya kumbuka Rwanda ni kanchi kadogo kanahitaji eneo,Uganda ni pazr maana Bk ni karibu na Kampala ikishindikana wasomi wote na wafanyabiasjara wote wa bukoba ambao wako kila mkoa watarudiahwa na kagera mjomba nchi yake
Hakika
 
Back
Top Bottom