Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Nimekuuliza "Ibara ya juu ya thread ipi inasema rais ana mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya siasa?"

Ibara ya 29 na 30 hazijamtaja rais kabisa.

Ibara ya 31(4) imeeleza tu kwamba "hali ya hatari" itatangazwa na rais.

Lini rais Magufuli katangaza hali ya hatari? Unafahamu tamko la kutangaza hali ya hatari linakuwaje?

Hii marufuku aliyopiga sasa hivi Magufuli, kaipiga kwa ibara gani ya katiba?
Ndio maana nimekupa hizo ibara kutokana na kwamba hakuna ibara ndani ya katiba inayoongelea vyama vya siasa kufanya mikutano.
Serikali ndio iliyopewa mamlaka kuhakikisha watu wanafuata makubaliano yaliyomo kwenye katiba. Na kiongozi mkuu wa serikali ni rais.

Kwa misingi hiyo sasa kwamba kwakuwa hakuna ibara ndani ya katiba inaongelea vyama vya siasa kufanya mikutano isipokuwa tu kutokana na ibara ya 18 inayoongelea uhuru wa kukusanyika. Na ule uhuru na haki ya kukusanyika umepewa limitation kwenye ibara ya 29,30 na 31.
Sasa basi ile mikutano ya kisiasa inabanwa na ibara hizo kwamba haki ya wachache isije ikanyima haki watu wengi. Na serikali pekee ndiyo inayosimamia na kuhakikisha katiba haivunjwi.
 
Hujajibu swali langu.

Hujanionesha ni wapi rais amepewa mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Umeweka ibara za 29, 30, 31.

Nimezisoma.

29 na 30 hata hazimtaji rais.

31 imetaja rais katika context ya kuwa hali ya hatari itatangazwa na rais.

29 na 30 si relevant kwa swali langu kwa sababu hata hazimtaji rais.

31 si relevant kwa sababu hatuna hali ya hatari sasa hivi, haijatangazwa.

Hujatoa ibara niliyokutaka uitoe.

Hakuna popote pale kati ya hizo ibara iliposemwa kwamba rais ana mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya siasa kama alivyopiga marufuku sasa.
 
Hujajibu swali langu.

Hujanionesha ni wapi rais amepewa mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Umeweka ibara za 29, 30, 31.

Nimezisoma.

29 na 30 hata hazimtaji rais.

31 imetaja rais katika context ya kuwa hali ya hatari itatangazwa na rais.

Hakuna popote pale kati ya hizo ibara iliposemwa kwamba rais ana mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya siasa kama alivyopiga marufuku sasa.
Basi kifupi tu niambie ni nani anaye hakikisha ibara ya 29 na 30 hazivunjwi?
 
Basi kifupi tu niambie ni nani anaye hakikisha ibara ya 29 na 30 hazivunjwi?
Watanzania wote wana wajibu wa kuilinda na kuitetea katiba.

Ukianza kusoma ibara ya 29 utaona Watanzania wote wanapewa haki, ni wajibu wao kuzilinda haki hizi.

Tatizo una focus sana top down kama nchi ya kikomunisti.
 
Watanzania wote wana wajibu wa kuilinda na kuitetea katiba.
Hapo umesema vyema lakini tu kunakimoja hujamalizia kwamba serikali ndiyo inayosimamia ili raia waweze kuilinda na kuitetea.

Sasa basi kwa mantiki hiyo ya serikali kusimamia ibara ya 29 na 30 inaipa serikali meno ya kuweka limitation ya haki na uhuru. Na rais ndiye kiongozi wa serikali.
 
Serikali ni nini ?

Unafahamu kwamba wanaoendesha serikali ni vijakazi tu wa wananchi?

Utasemaje housegirl ndiye ana mamlaka ya kuweka limitation ya haki na uhuru wa baba mwenye nyumba atakula nini na nini asile katika nyumba yake mwenyewe?

You have it backwards. Hao viongozi wa serikali wanawajibika kwa wananchi. Wananchi hawawajibiki kwa viongozi wa serikali.
 
Naona sasa bwana Kiranga umeanza kuandika hekaya.
Naomba tuongee facts.
 
Naona sasa bwana Kiranga umeanza kuandika hekaya.
Naomba tuongee facts.
Hufahamu kwamba representative democracy ni social contract inayowapa wanaochaguliwa mandate ya kuwa custodians inayotoka kwa wananchi?

Na kwamba kuwa custodian hakuna maana wewe ni mfalme usiye na mipaka, unaamua tu kupiga marufuku mikutano ya kisiasa bila kutumia kifungu chochote cha katiba?

Magufuli katumia kifungu gani cha katiba kupiga marufuku mikutano ya siasa?

Hujanipa hicho kifungu bado.
 
Sasa kama rais amezuia wewe kikatiba unatakiwa ufanye nini sasa?
 
Sasa kama rais amezuia wewe kikatiba unatakiwa ufanye nini sasa?
Impeach his ass.

Kitu ambacho Kibongo hakiwezi kufanyika kwa sababu watu wanamuona rais kama Mungu mtu halafu wanaendekeza maslahi ya watu wachache dhidi ya yawengi.
 
Impeach his ass.

Kitu ambacho Kibongo hakiwezi kufanyika kwa sababu watu wanamuona rais kama Mungu mtu halafu wanaendekeza maslahi ya watu wachache dhidi ya yawengi.
Wewe naona unahasira zako binafsi. Nimekuuliza kikatiba unatakiwa ufanyenini? Taja kifungu cha katiba kulingana na hicho unachokisema.
Bwana Kiranga sitaki hekaya hapa. I need facts with references from constitution.
 
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
Twende taratibu ndugu! Ibara ya 17.-(1) inasema: "Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano."

Kwamba, wewe (singular) una haki na uhuru wa kuishi kokote katika Jamhuri ya Muungano! Wewe ni tajiri na kwa kutumia utajiri wako, unataka kijiji chooooooooote uishi peke yako na wengine wote wakupishe... HIYO HAPANA hata kama una haki na uhuru wa kuishi popote kv unataka kuutumia uhuru huo wewe binafsi huku ukitaka kuingilia haki na uhuru wa watu wengine (plural)! Kinyume chake, wewe mmoja hata kama una haki ya kuishi popote, unaweza kuondolewa kwa maslahi ya wengi!!

CHADEMA sio mtu (singular) bali ni taasisi inayoundwa na watu (plural). Technically, taasisi ya kisiasa inabeba maslahi ya watu na sio mtu... na watu hawa ni mamilioni!

Ibara ya 12 & 13 inaelezea Haki ya Usawa, Ibara ya 14 hadi ya 17 inaelezea Haki ya Kuishi, Ibara ya 18 hadi 21 inaelezea Haki ya Uhuru wa Mawazo, Ibara ya 22 hadi ya 28 Haki ya Kufanya Kazi na Ibara ya 29 ni Masharti ya Jumla.

Hata kama CHADEMA tungeweza kuichukulia ni individual, unless useme ni namna gani haki za watu wengine kwa kuzingatia Ibara ya 12 hadi 29 vitaathiriwa vinginevyo Ibara ya 30(1) becomes inapplicable. Ni rahisi kusema kwamba itaathiri shughuli za watu na hivyo kuvunja Ibara 22 hadi 28 inayotoa haki ya kufanya kazi! Na ni kutokana na hofu ya maandamano kuathiri shughuli za watu wengine ndipo pakawa na sheria kwamba, kabla ya ku-excute maandamano, waandaaji wanatakiwa kuliarifu jeshi la polisi. Moja ya busara iliyomo ndani ya sheria au utaratibu huo pamoja na mambo mengine, pale inapobidi, jeshi la polisi liweze kutoa muongozo maandamano yapitie wapi ili kukwepa kuathiri haki ya watu wengi zaidi ya kufanya kazi. Kwa maana nyingine ni kwamba, popote pale panapo umuhimu wa kutekeleza haki ya mtu mmoja au kundi fulani, panatengenezwa mazingira muafaka ili nao wasiathiri haki za wengine lakini sio kuzuia haki ya mtu kwa kigezo ataathiri haki za watu wengine wakati ipo namna ya kutengeneza win-win situation!

Kutokana na maelezo hayo hapo juu, nachuku nafasi hii kuhitimisha Ibaya ya 30 (1) haina maana hiyo katika utetezi wako!! Tuje Ibara ya 30(2):
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
Sawa kabisa! Ikiwa inathibitika CHADEMA wanakiuka sheria basi watakuwa wanavunja Katiba kwa kuanagalia Ibara ya 30 (2). Swali: Je, kuna sheria yoyote wanayovunja?

Tujikumbushe: Chanzo cha UKUTA ni baada ya CHADEMA na wenzao kutoridhishwa na hali iliyokuwa inaendelea bungeni. Baada ya maneno ya kisiasa ya hapa na pale, hatimae wakaadhimia kufanya shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ili kupinga hali hiyo. Kufuatia kusudio hilo, ndipo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano akaziwekea quotas/vikwazo shughuli za kisiasa kwamba; anayeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa sasa ni yule tu ambae amechaguliwa na wananchi (kwenye uchaguzi mkuu) na shughuli hizo atafanyia ndani ya mipaka ya jimbo TU!!

Watu wamekuwa wakisema kwamba anachosema Rais ni kauli ya mwisho kwa maana hiyo, hao watu wanataka kutuaminisha kwamba kv Rais keshayasema hayo basi hiyo inakuwa ni kauli halali na ndio maana katika kutekeleza kauli hiyo ya Amir Jeshi Mkuu, ndipo linaingia Jeshi la Polisi kutaka ku-enforce agizo hilo la Rais!

Swali: Je, Rais ana mamlaka ya kusema kamata yule na piga risasi? Je, ana mamlaka ya kusema kuanzia leo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi inafungwa kwa matumizi ya watu wengine isipokuwa yeye tu? Je, ana mamlaka ya kumtoa Mheshimiwa Kassim Majaliwa pale alipo na kumweka Mama Janeth Magufuli?

Maswali yote hayo na mengine kama hayo majibu yake ni HAPANA!! Hii maana yake ni nini? Chochote atakachosema au kuagiza Rais kitachukuliwa ni kauli halali endapo tu kauli au agizo husika litasimama ndani ya mipaka ya katiba na sheria za nchi na agizo lolote lililo nje ya mipaka ya katiba litakuwa batili kv lina uwezekano wa kuvunja hata katiba yenyewe!

Tukirejea kwenye agizo la Rais na shughuli za siasa hadi 2020. Kwanza kabisa, Ibara ya 3(2) inasema:
"Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo."

Picha unayopata toka kwenye hiyo ibara ni kwamba, kumbe vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa katiba.

Lakini tukirudi kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2007, Sura ya 258, Sehemu ya Pili inayotaja Haki ya Chama; Ibara ya 4(1)b inasema: Kila chama cha siasa kitakuwa na haki ya kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar.

Aidha 4(1)e inasema: Kila chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisisasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Hapo tena tunaona si tu kwamba Vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa katiba lakini pia sheria ya vyama siasa inatoa haki kwa vyama siasa kufanya maandamano.

Kama ambavyo Rais hawezi kuagiza kamata yule piga risasi au kuanzia sasa Ali Hassani Mwinyi Road itakuwa reserved exclussively kwa ajili yake kv hiyo itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa katiba na sheria za nchi; ndivyo vile vile asivyo na mamlaka ya kusema ama kufanya lolote litakalokiuka sheria hizo hapo juu!

Kwahiyo, msingi hapa ni uzuiaji wa shughuli za kisiasa... shughuli halali kikatiba na kisheria. Mheshimiwa Rais angeweza kutoa agizo litakalopelekea ukiukwaji wa sheria hiyo endapo tu ingeonekana katika ku-enjoy matunda ya sheria hiyo hapo juu, in the first place, CHADEMA watakuwa wanavunja katiba (au hata sheria) kwa kuingilia haki na uhuru wa watu wengine kama inavyosema Ibara ya 30 (1).

Ni rahisi kusema kwamba CHADEMA watakuwa wanapinga amri halali ya jeshi la polisi! Kama umenisoma nukta kwa nukta, amri hiyo ya polisi haiwezi kuwa amri halali kwavile imezaliwa kutoka kwenye agizo haramu linalokiuka katiba na sheria za nchi!

No one is above the law!

Kwa kuzingatia maelezo hayo hapo juu, kama ilivyokuwa kwa Ibara ya 30(1); Ibara ya 30(2) nayo haina msingi wowote kwenye jambo hili na hivyo vifungu vyote vidogo vya Ibara ya 30(2) navi-discredit!
 
Wewe naona unahasira zako binafsi. Nimekuuliza kikatiba unatakiwa ufanyenini? Taja kifungu cha katiba kulingana na hicho unachokisema.
Bwana Kiranga sitaki hekaya hapa. I need facts with references from constitution.
Hufahamu kifungu cha katiba kinachoongelea impeachment?

Unafahamu impeachment ni nini kwanza?
 
Back
Top Bottom