Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Hufahamu kifungu cha katiba kinachoongelea impeachment?

Unafahamu impeachment ni nini kwanza?
Sasa nimekuambia acha hekaya. Leta hapa hivyo vifungu. bwana Kiranga ninahitaji hapa references ya hicho unachodai sawa?
 
Twende taratibu ndugu! Ibara ya 17.-(1) inasema: "Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano."

Kwamba, wewe (singular) una haki na uhuru wa kuishi kokote katika Jamhuri ya Muungano! Wewe ni tajiri na kwa kutumia utajiri wako, unataka kijiji chooooooooote uishi peke yako na wengine wote wakupishe... HIYO HAPANA hata kama una haki na uhuru wa kuishi popote kv unataka kuutumia uhuru huo wewe binafsi huku ukitaka kuingilia haki na uhuru wa watu wengine (plural)! Kinyume chake, wewe mmoja hata kama una haki ya kuishi popote, unaweza kuondolewa kwa maslahi ya wengi!!

CHADEMA sio mtu (singular) bali ni taasisi inayoundwa na watu (plural). Technically, taasisi ya kisiasa inabeba maslahi ya watu na sio mtu... na watu hawa ni mamilioni!

Ibara ya 12 & 13 inaelezea Haki ya Usawa, Ibara ya 14 hadi ya 17 inaelezea Haki ya Kuishi, Ibara ya 18 hadi 21 inaelezea Haki ya Uhuru wa Mawazo, Ibara ya 22 hadi ya 28 Haki ya Kufanya Kazi na Ibara ya 29 ni Masharti ya Jumla.

Hata kama CHADEMA tungeweza kuichukulia ni individual, unless useme ni namna gani haki za watu wengine kwa kuzingatia Ibara ya 12 hadi 29 vitaathiriwa vinginevyo Ibara ya 30(1) becomes inapplicable. Ni rahisi kusema kwamba itaathiri shughuli za watu na hivyo kuvunja Ibara 22 hadi 28 inayotoa haki ya kufanya kazi! Na ni kutokana na hofu ya maandamano kuathiri shughuli za watu wengine ndipo pakawa na sheria kwamba, kabla ya ku-excute maandamano, waandaaji wanatakiwa kuliarifu jeshi la polisi. Moja ya busara iliyomo ndani ya sheria au utaratibu huo pamoja na mambo mengine, pale inapobidi, jeshi la polisi liweze kutoa muongozo maandamano yapitie wapi ili kukwepa kuathiri haki ya watu wengi zaidi ya kufanya kazi. Kwa maana nyingine ni kwamba, popote pale panapo umuhimu wa kutekeleza haki ya mtu mmoja au kundi fulani, panatengenezwa mazingira muafaka ili nao wasiathiri haki za wengine lakini sio kuzuia haki ya mtu kwa kigezo ataathiri haki za watu wengine wakati ipo namna ya kutengeneza win-win situation!

Kutokana na maelezo hayo hapo juu, nachuku nafasi hii kuhitimisha Ibaya ya 30 (1) haina maana hiyo katika utetezi wako!! Tuje Ibara ya 30(2): Sawa kabisa! Ikiwa inathibitika CHADEMA wanakiuka sheria basi watakuwa wanavunja Katiba kwa kuanagalia Ibara ya 30 (2). Swali: Je, kuna sheria yoyote wanayovunja?

Tujikumbushe: Chanzo cha UKUTA ni baada ya CHADEMA na wenzao kutoridhishwa na hali iliyokuwa inaendelea bungeni. Baada ya maneno ya kisiasa ya hapa na pale, hatimae wakaadhimia kufanya shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ili kupinga hali hiyo. Kufuatia kusudio hilo, ndipo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano akaziwekea quotas/vikwazo shughuli za kisiasa kwamba; anayeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa sasa ni yule tu ambae amechaguliwa na wananchi (kwenye uchaguzi mkuu) na shughuli hizo atafanyia ndani ya mipaka ya jimbo TU!!

Watu wamekuwa wakisema kwamba anachosema Rais ni kauli ya mwisho kwa maana hiyo, hao watu wanataka kutuaminisha kwamba kv Rais keshayasema hayo basi hiyo inakuwa ni kauli halali na ndio maana katika kutekeleza kauli hiyo ya Amir Jeshi Mkuu, ndipo linaingia Jeshi la Polisi kutaka ku-enforce agizo hilo la Rais!

Swali: Je, Rais ana mamlaka ya kusema kamata yule na piga risasi? Je, ana mamlaka ya kusema kuanzia leo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi inafungwa kwa matumizi ya watu wengine isipokuwa yeye tu? Je, ana mamlaka ya kumtoa Mheshimiwa Kassim Majaliwa pale alipo na kumweka Mama Janeth Magufuli?

Maswali yote hayo na mengine kama hayo majibu yake ni HAPANA!! Hii maana yake ni nini? Chochote atakachosema au kuagiza Rais kitachukuliwa ni kauli halali endapo tu kauli au agizo husika litasimama ndani ya mipaka ya katiba na sheria za nchi na agizo lolote lililo nje ya mipaka ya katiba litakuwa batili kv lina uwezekano wa kuvunja hata katiba yenyewe!

Tukirejea kwenye agizo la Rais na shughuli za siasa hadi 2020. Kwanza kabisa, Ibara ya 3(2) inasema:
"Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo."

Picha unayopata toka kwenye hiyo ibara ni kwamba, kumbe vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa katiba.

Lakini tukirudi kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2007, Sura ya 258, Sehemu ya Pili inayotaja Haki ya Chama; Ibara ya 4(1)b inasema: Kila chama cha siasa kitakuwa na haki ya kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar.

Aidha 4(1)e inasema: Kila chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisisasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Hapo tena tunaona si tu kwamba Vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa katiba lakini pia sheria ya vyama siasa inatoa haki kwa vyama siasa kufanya maandamano.

Kama ambavyo Rais hawezi kuagiza kamata yule piga risasi au kuanzia sasa Ali Hassani Mwinyi Road itakuwa reserved exclussively kwa ajili yake kv hiyo itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa katiba na sheria za nchi; ndivyo vile vile asivyo na mamlaka ya kusema ama kufanya lolote litakalokiuka sheria hizo hapo juu!

Kwahiyo, msingi hapa ni uzuiaji wa shughuli za kisiasa... shughuli halali kikatiba na kisheria. Mheshimiwa Rais angeweza kutoa agizo litakalopelekea ukiukwaji wa sheria hiyo endapo tu ingeonekana katika ku-enjoy matunda ya sheria hiyo hapo juu, in the first place, CHADEMA watakuwa wanavunja katiba (au hata sheria) kwa kuingilia haki na uhuru wa watu wengine kama inavyosema Ibara ya 30 (1).

Ni rahisi kusema kwamba CHADEMA watakuwa wanapinga amri halali ya jeshi la polisi! Kama umenisoma nukta kwa nukta, amri hiyo ya polisi haiwezi kuwa amri halali kwavile imezaliwa kutoka kwenye agizo haramu linalokiuka katiba na sheria za nchi!

No one is above the law!

Kwa kuzingatia maelezo hayo hapo juu, kama ilivyokuwa kwa Ibara ya 30(1); Ibara ya 30(2) nayo haina msingi wowote kwenye jambo hili na hivyo vifungu vyote vidogo vya Ibara ya 30(2) navi-discredit!

Umejitahidi kutoa maneno meengi sana huku ukijaribu kubatilisha katiba kwa kutumia vifungu vya kwenye sheria ya vyama vya siasa. Umesahau kwamba pia kunasheria za polisi.
kwanza katiba tuanze kwenye katiba ibara ya 29.5 inasema:-

(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na
Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli
zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu
wengine au maslahi ya umma.

Sasa basi kulingana na hicho hapo juu kukawepo na sheria za jeshi la polisi kuhusu mikusanyiko na maandamano.
Katika sheria za polis ibara ya 43 inatoa namna ya kufanya mikusanyiko na maandamano:-

43. (1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.
(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.
(4) Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au mwendelezo wa mkusanyiko au maandamano katika hadhara/sehemu za umma ambayo yanaitishwa, kusanywa, kuundwa au andaliwa vinginevyo tofauti kulingana na taarifa chini ya kifungu kidogo cha (1) au kutokana na kwamba maelezo yaliyoainishwa na Waziri chini ya aya (c) ya kifungu kidogo cha (1) yamekiukwa au yanakiukwa , na anaweza, kwa dhumuni lolote lililotajwa, kutoa amri kama atakavyoona ni lazima au inafaa , ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya mkusanyiko wowote au maandamano kama ilivyotajwa hapo juu.
(5) Waziri anaweza, kwa amri, kutangaza kwamba masharti ya kifungu hiki hayatatumika katika mkusanyiko au maandamano yaliyoitishwa, kusanywa, kuundwa au kupangwa pasipokuwepo na sababu moja au zaidi au muungano wa sababu moja au zaidi kama itakavyoweza kuainishwa katika amri hiyo.
(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.

Huo hapo juu ndio utaratibu wa kufanya mikusanyiko au maandamano. Ukusoma hiyo ibara 43.3 Inaeleza namna ya mikusanyiko au maandamano yanaweza kuzuiliwa.

Mpaka hapo tupo sawa.

Sasa tukiendelea hapo hapo kwenye sheria ya polisi ibara ya 44 inasema hivi:-

44. Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au kuendelea kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano yoyote katika sehemu yoyote ile kama, kwa mawazo ya afisa huyo anaona kufanyika au kuendelea kufanyika, kama inavyoweza kuwa, kwa mkusanyiko au maandamano hayo yanavunja amani au kuvuruga usalama wa umma au kulinda amani na amri, na anaweza, kwa manufaa ya umma, ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya kwa mkusanyiko huo au maandamano kama ilivyosemwa.

Ukiendelea kusoma zaidi kwenye ibara ya 45 ya sheria za jeshi la polisi inahusu kutawanya mkusanyiko au maandamano:-

45. Mkusanyiko au maandamano yoyote ambayo watu watatu au zaidi wanaohudhuria au kuchukua nafasi wanazembea au kukataa kufuata amri yoyote ya kutawanywa iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 43 au kifungu cha 44, itahesabika kuwa mkusanyiko kinyume na sheria katika maana iliyopo katika kifungu cha 74 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*

Ngoja kwanza niishie hapa nikusubiri unasemaje ili tuendelee kujadiliana.
 
Nilitoa changamoto ya namna gani UKUTA na maandamano yao vitaathiri Ibara ya 30 (1) ambayo msingi wake ni sawa na ibara hiyo hapo juu! Hujanijibu!

Tangu post yangu ya kwanza nilishasema kwamba, ili kukidhi Ibara ya 30(1) kwamba haki na uhuru wa mtu mmoja usije ukawa ni chanzo cha kukiuka haki na uhuru wa mtu mwingine, na ndio maana ingawaje chama cha siasa kina haki ya kufanya maandamano' kabla ya kufanya hivyo wanatakiwa kutekeleza masharti ya sheria hiyo uliyoitaja ili jeshi la polisi liweze kusimamia maandamano hayo na ikiwezekana kuelekeza hata route muafaka ili maandamano hayo yasije yakawa chanzo cha kukiuka haki na uhuru wa watu wengine kv uhuru wa kufanya kazi! Kwahiyo badala ya polisi kuzuia pasipo na sababu za msingi na hatimae kupoka haki ya yule aliyetaka kuandamana, wao wanatakiwa kuhakikisha yule mwenye haki ya kuandamana anaipata haki hiyo na wengine wote (wasiohusika)hawaathiriki na wakati wa utekelezaji wa haki ya yule mwingine (ya kuandamana)!

YES... lakini sio tu kutoa amri ya kuzuia bila sababu maalum! Si polisi si yeyote aliye juu ya sheria kwahiyo hata polisi wanapotoa zuio wanatakiwa kuwa na tangible reason!
(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.
Hahahaa! Kifungu kinawasuta wenyewe... na ndio maana awali nikasema unazuia kwa sababu ambazo ni tangible! Hebu nieleze, viashiria gani vya kuvunjika kwa amani ambavyo jeshi la polisi iliviona hata watoe zuio?
(4) Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au mwendelezo wa mkusanyiko au maandamano katika hadhara/sehemu za umma ambayo yanaitishwa, kusanywa, kuundwa au andaliwa vinginevyo tofauti kulingana na taarifa chini ya kifungu kidogo cha (1) au kutokana na kwamba maelezo yaliyoainishwa na Waziri chini ya aya (c) ya kifungu kidogo cha (1) yamekiukwa au yanakiukwa , na anaweza, kwa dhumuni lolote lililotajwa, kutoa amri kama atakavyoona ni lazima au inafaa , ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya mkusanyiko wowote au maandamano kama ilivyotajwa hapo juu.
(5) Waziri anaweza, kwa amri, kutangaza kwamba masharti ya kifungu hiki hayatatumika katika mkusanyiko au maandamano yaliyoitishwa, kusanywa, kuundwa au kupangwa pasipokuwepo na sababu moja au zaidi au muungano wa sababu moja au zaidi kama itakavyoweza kuainishwa katika amri hiyo.
(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.

Huo hapo juu ndio utaratibu wa kufanya mikusanyiko au maandamano. Ukusoma hiyo ibara 43.3 Inaeleza namna ya mikusanyiko au maandamano yanaweza kuzuiliwa.

Mpaka hapo tupo sawa.

Sasa tukiendelea hapo hapo kwenye sheria ya polisi ibara ya 44 inasema hivi:-

44. Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au kuendelea kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano yoyote katika sehemu yoyote ile kama, kwa mawazo ya afisa huyo anaona kufanyika au kuendelea kufanyika, kama inavyoweza kuwa, kwa mkusanyiko au maandamano hayo yanavunja amani au kuvuruga usalama wa umma au kulinda amani na amri, na anaweza, kwa manufaa ya umma, ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya kwa mkusanyiko huo au maandamano kama ilivyosemwa.

Ukiendelea kusoma zaidi kwenye ibara ya 45 ya sheria za jeshi la polisi inahusu kutawanya mkusanyiko au maandamano:-

45. Mkusanyiko au maandamano yoyote ambayo watu watatu au zaidi wanaohudhuria au kuchukua nafasi wanazembea au kukataa kufuata amri yoyote ya kutawanywa iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 43 au kifungu cha 44, itahesabika kuwa mkusanyiko kinyume na sheria katika maana iliyopo katika kifungu cha 74 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*

Ngoja kwanza niishie hapa nikusubiri unasemaje ili tuendelee kujadiliana.
Naona yote ama vifungu vyote ulivyoweka vinaelezea kitu kile kile ambacho nami nishaelezea vya kutosha! Vifungu vyote havijajibu hoja zangu! Kila mtu anafahamu kwamba Jeshi la Polisi wana mamlaka ya kuzuiaa ama kusitisha maandamano lakini lazima pawe na sababu za msingi.

Sababu zilizotolewa na amiri jeshi mkuu kuzuia maandamano hayo na shughuli zingine za kisiasa si sababu halali kikatiba wala kisheria! Na kwavile sababu hizo sio halali basi na katazo lenyewe nalo haliwezi kuwa na uhalali! Polisi nao wanataka kutekeleza agizo ambalo pia si halali! Polisi wangepata uhalali wa kuzuia endapo endapo pangetokea viashiria kama ambavyo vimeelezwa kwenye vifungu ulivyoweka wewe mwenyewe!
 
Sasa ndio umeona/umesikia leo? Tunafahamu sana hiyo. Hujamaliza ulichotaka kusema then wanasheria "wenzako" watakuja kukupeleka shule ya bure. Hiyo ni sheria sio katiba ya Saccoss.
 
Nilitoa changamoto ya namna gani UKUTA na maandamano yao vitaathiri Ibara ya 30 (1) ambayo msingi wake ni sawa na ibara hiyo hapo juu! Hujanijibu!
Tangu post yangu ya kwanza nilishasema kwamba, ili kukidhi Ibara ya 30(1) kwamba haki na uhuru wa mtu mmoja usije ukawa ni chanzo cha kukiuka haki na uhuru wa mtu mwingine, na ndio maana ingawaje chama cha siasa kina haki ya kufanya maandamano' kabla ya kufanya hivyo wanatakiwa kutekeleza masharti ya sheria hiyo uliyoitaja ili jeshi la polisi liweze kusimamia maandamano hayo na ikiwezekana kuelekeza hata route muafaka ili maandamano hayo yasije yakawa chanzo cha kukiuka haki na uhuru wa watu wengine kv uhuru wa kufanya kazi! Kwahiyo badala ya polisi kuzuia pasipo na sababu za msingi na hatimae kupoka haki ya yule aliyetaka kuandamana, wao wanatakiwa kuhakikisha yule mwenye haki ya kuandamana anaipata haki hiyo na wengine wote (wasiohusika)hawaathiriki na wakati wa utekelezaji wa haki ya yule mwingine (ya kuandamana)!
YES... lakini sio tu kutoa amri ya kuzuia bila sababu maalum! Si polisi si yeyote aliye juu ya sheria kwahiyo hata polisi wanapotoa zuio wanatakiwa kuwa na tangible reason!Hahahaa! Kifungu kinawasuta wenyewe... na ndio maana awali nikasema unazuia kwa sababu ambazo ni tangible! Hebu nieleze, viashiria gani vya kuvunjika kwa amani ambavyo jeshi la polisi iliviona hata watoe zuio?Naona yote ama vifungu vyote ulivyoweka vinaelezea kitu kile kile ambacho nami nishaelezea vya kutosha! Vifungu vyote havijajibu hoja zangu! Kila mtu anafahamu kwamba Jeshi la Polisi wana mamlaka ya kuzuiaa ama kusitisha maandamano lakini lazima pawe na sababu za msingi.

Sababu zilizotolewa na amiri jeshi mkuu kuzuia maandamano hayo na shughuli zingine za kisiasa si sababu halali kikatiba wala kisheria! Na kwavile sababu hizo sio halali basi na katazo lenyewe nalo haliwezi kuwa na uhalali! Polisi nao wanataka kutekeleza agizo ambalo pia si halali! Polisi wangepata uhalali wa kuzuia endapo endapo pangetokea viashiria kama ambavyo vimeelezwa kwenye vifungu ulivyoweka wewe mwenyewe!
Ngoja nifike sehemu ili tujadiliane vizuri. Japo umetoa maelezo kutoka kwenye kichwa chako tu bila kutoa references kwenye vifungu vya katiba au sheria.
Huwezi kuijibu katiba kwenye ibara ya 29 na 30 kwa kutoa maelezo tu. Hiyo naweza kusema ni matamanio ya kwamba katiba ingekuwa kama unavyotaka.

Vifungu vyote vya sheria ya polisi vimeweka wazi kabisa na kueleza kwamba malalamiko ya kuhusu kukusanyika yanapelekwa kwa waziri na yeye ndiye anatoa maamuzi ya mwisho.

Sijui kwanini hutaki kuelewa wakati vitu vyote vipo wazi hapa.
 
Sasa nimekuambia acha hekaya. Leta hapa hivyo vifungu. bwana Kiranga ninahitaji hapa references ya hicho unachodai sawa?
Kabla ya kukupa kifungu, unafahamu maana ya impeachment?

Kwa sababu kama unafahamu maana ya impeachment, na umeisoma katiba, huwezi kuniuliza hilo swali.
 
Sasa bwana Kiranga sijui unaongea kitu gani sasa!!! Kile unachoongea wala hakiendani na tunachoongelea. Katiba imetoa njia moja tu ya kumuondoa rais akiwa madarakani. Ni kupitia wa bunge tu. Sasa wewe kwa ufahamu wako hawa chadema wanafanya maandamano ili wamuondoe rais?
 
Unasoma ninachoandika au unajifaragua tu?
 
Rais amevunja ibara ya ngapi mpaka ukaanza kuuliza kama ninajua impeachment?
Wewe bwana Kiranga acha kujibaraguza
Nimeanza kukuuliza hapa nipe ibara aliyotumia rais kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, hujanipa.

Ukinipa ibara hiyo, nitakupa aliyoivunja Magufuli.

Unaweza kunipa ibara hiyo?
 
Umejitahidi kutoa maneno meengi sana huku ukijaribu kubatilisha katiba kwa kutumia vifungu vya kwenye sheria ya vyama vya siasa. Umesahau kwamba pia kunasheria za polisi.
kwanza katiba tuanze kwenye katiba ibara ya 29.5 inasema:-

(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na
Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli
zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu
wengine au maslahi ya umma.

Sasa basi kulingana na hicho hapo juu kukawepo na sheria za jeshi la polisi kuhusu mikusanyiko na maandamano.
Katika sheria za polis ibara ya 43 inatoa namna ya kufanya mikusanyiko na maandamano:-

43. (1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.
(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.
(4) Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au mwendelezo wa mkusanyiko au maandamano katika hadhara/sehemu za umma ambayo yanaitishwa, kusanywa, kuundwa au andaliwa vinginevyo tofauti kulingana na taarifa chini ya kifungu kidogo cha (1) au kutokana na kwamba maelezo yaliyoainishwa na Waziri chini ya aya (c) ya kifungu kidogo cha (1) yamekiukwa au yanakiukwa , na anaweza, kwa dhumuni lolote lililotajwa, kutoa amri kama atakavyoona ni lazima au inafaa , ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya mkusanyiko wowote au maandamano kama ilivyotajwa hapo juu.
(5) Waziri anaweza, kwa amri, kutangaza kwamba masharti ya kifungu hiki hayatatumika katika mkusanyiko au maandamano yaliyoitishwa, kusanywa, kuundwa au kupangwa pasipokuwepo na sababu moja au zaidi au muungano wa sababu moja au zaidi kama itakavyoweza kuainishwa katika amri hiyo.
(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.

Huo hapo juu ndio utaratibu wa kufanya mikusanyiko au maandamano. Ukusoma hiyo ibara 43.3 Inaeleza namna ya mikusanyiko au maandamano yanaweza kuzuiliwa.

Mpaka hapo tupo sawa.

Sasa tukiendelea hapo hapo kwenye sheria ya polisi ibara ya 44 inasema hivi:-

44. Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au kuendelea kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano yoyote katika sehemu yoyote ile kama, kwa mawazo ya afisa huyo anaona kufanyika au kuendelea kufanyika, kama inavyoweza kuwa, kwa mkusanyiko au maandamano hayo yanavunja amani au kuvuruga usalama wa umma au kulinda amani na amri, na anaweza, kwa manufaa ya umma, ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya kwa mkusanyiko huo au maandamano kama ilivyosemwa.

Ukiendelea kusoma zaidi kwenye ibara ya 45 ya sheria za jeshi la polisi inahusu kutawanya mkusanyiko au maandamano:-

45. Mkusanyiko au maandamano yoyote ambayo watu watatu au zaidi wanaohudhuria au kuchukua nafasi wanazembea au kukataa kufuata amri yoyote ya kutawanywa iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 43 au kifungu cha 44, itahesabika kuwa mkusanyiko kinyume na sheria katika maana iliyopo katika kifungu cha 74 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*

Ngoja kwanza niishie hapa nikusubiri unasemaje ili tuendelee kujadiliana.

Duuh,aisee wewe jamaa ni sifuri...u are getting schooled in and out and u still got nerves kubisha...

Ignorant people who actually even do not know kua wao ni ignorant,hawana mshipa wa noma aisee...

Ignorants need schooling,and u are getting it...they issue,u are so ignorant mpaka upo kwenye ignorance denial ambapo hakuna cure by schooling,mpaka ukafanyie psychological counselling for many years
 
Rais amevunja ibara ya ngapi mpaka ukaanza kuuliza kama ninajua impeachment?
Wewe bwana Kiranga acha kujibaraguza

Annael umeingia cha kike,fani hii ni ya watu and u got exposed kua wewe ni fraud...

Tatizo la fani professional hua imitation ni rahisi kumshika...na kwa makamo haya Annael,ni aibu kwako...

Mpaka layman kama mimi mwenye IQ ya kawaida kabisa,tukiondoa ushabiki wa pande yoyote,umekua debunked left and right...u got embarassed on your own sh.it bra.
 
Kwanini sasa Lisu and Company hawaendi mahakamani wanasisitiza maandamano tu?
Kwahiyo unataka kuniambia baadhi ya ibara kwenye katiba ni batili?
Au umelenga kuongea kitu gani hasa?
Unataka kuniambia ibara ya 29, 30 na 31 siku hizi hazitumiki?
Hebu nijibu maswali yangu haya machache tuondoe utata.
Jibu ni ndio....Jaribu kusoma R v Dominic Mbushuu....
 
Annael umeingia cha kike,fani hii ni ya watu and u got exposed kua wewe ni fraud...

Tatizo la fani professional hua imitation ni rahisi kumshika...na kwa makamo haya Annael,ni aibu kwako...

Mpaka layman kama mimi mwenye IQ ya kawaida kabisa,tukiondoa ushabiki wa pande yoyote,umekua debunked left and right...u got embarassed on your own sh.it bra.
Sasa maelezo yote hayo ya kushikwa yametoka wapi hapa.
Hapa katiba inasema wazi kwanini wasiende mahakamani? Kama sio kuwatumia watu kwa ujinga wao ili wafikishe taarifa zao.
Tatizo lenu mnaongea maneno ya ajabu ajabu tu. Katiba imeweka wazi kwamba kama unaona katiba imevunjwa, inavunjwa au inaelekea kuvunjwa unaenda mahakamani.
Sasa hapa unapoleta taarabu maneno meengi ni ujinga.
 
Mkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.

Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!

Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.

Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest. Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.

Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.

Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.

Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!

Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!

Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!

Hawa jamaa wagonjwa na hawaiona ikulu kamwe
 
Hahahaaaaa.....walianza na operation sangala,wakaja na Ukawa,na sasa wamekuja na kiki mpya ya Ukuta,wewe mwananchi mwenzangu hujashtuka tu!!!!!!
 
Nimeanza kukuuliza hapa nipe ibara aliyotumia rais kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, hujanipa.

Ukinipa ibara hiyo, nitakupa aliyoivunja Magufuli.

Unaweza kunipa ibara hiyo?

hapa jibu halitotoka akikupa na mimi unipatie,,,,,, hapa ndipo ukuta ulipopamba moto.
 
Hawa jamaa wagonjwa na hawaiona ikulu kamwe

ikulu sio mali ya chama flani hata hashimu rungwe anaweza kuingia shida ipo nchi hii kwa waliondelea na wenye fikra pana wanaamini ktk sera na ushawishi ili taifa lisonge mbele haijalishi unatokea upande upi ila sio ushindani wa kivyama.
 
Lisu anawaingiza mkenge.
 
Back
Top Bottom