Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

kwa nini umesubiri kwa muda wa maika 10 ndipo unatueleza?Wakati ulipokuwa unapata mishahara kwa fedha za wizi,uliuchana.leo fedha zetu umeanzisha biashara unaamua kuwamwagia mchanga kitumbua wezi wenzako.miaka .10 kukaa kimya ni mingi sana.
 
yaani@voda ndo mababa wa utapeli mi siku hizi ni airtel afadhali

Skia mkuu,yan hii ni kwamakampun yote ya sim hapa Tanzania na bila ubishi vitu vyote alivyotaja mtoa mada vipo kwel na vinaonekana kwenye matumiz ya kila siku,kwaiyo uwezi kukoswa na mkono wa Escrow huu!!
 
Waziri wa tecnologia na mawasiliano na naibu wake yupo na wanayajua haya kisa10% alafu naibu waziri wa wizara husika anataka Urais kwa mtaji huu Urais asahau labda awe rais wa Bumbuli
 
TANU ilianza mwaka 1954 jamani TANU eeenhe iyeee iyee wimbo mzuri xana
 

duuuu mzee vocha ya laki 2 inafanya nn kwenye sim.....kama n kawaida yake......asingejutia......
any way...mchrzo uliishaje
 
tigo duka lao lililopo malindi Zanzibar ndio majambazi kabisa,vocha ikikwanguka vibaya ukiwapelekea ndio imekula kwako,niliwahi kuwapelekea vocha ya 5000 ilikwanguka vibaya.Walichofanya walinipa fomu nijaze ikisha wakaiambatanisha na hiyo vocha wakaniambia watanitumia basi mpaka leo mwaka wa pili huu.
 
tigo duka lao lililopo malindi Zanzibar ndio majambazi kabisa,vocha ikikwanguka vibaya ukiwapelekea ndio imekula kwako,niliwahi kuwapelekea vocha ya 5000 ilikwanguka vibaya.Walichofanya walinipa fomu nijaze ikisha wakaiambatanisha na hiyo vocha wakaniambia watanitumia basi mpaka leo mwaka wa pili huu.
 
Na kibaya ni kwamba kampuni hizi zimeunda partnership ya hatari sana kwa lengo la kuwakamua wateja wao bila huruma. Mwanzoni kila kampuni ilikuwa inafanya kazi zake kwa kujitegemea lakini baadaye waliamua kuungana ili wawadhibiti wateja vizuri zaidi. Mfano halisi ni kwamba kifurushi cha Tsh 500 kwa Voda na tiG0 ni dakika 8, sms 300 na 40MB…wamelinganisha viwango kwa makusudi! Hii maana yake ni kwamba wameweka viwango sawa ili wateja wakose pa kuponyokea…ukienda tigo unakula kirungu na ukirudi voda pia unakula kirungu hicho hicho! There is no way you can escape being exploited!

Mfano mwingine: Hebu tazama ushahidi huu hapa jinsi walivyopanga ku synchronize huduma zao kwa lengo lilelile la kuwanyonya wateja kwa pamoja. Siku hizi hata promo wanapiga equally and at the same time:

******************************************************************************
Pata Sh1000 BURE kila uongezapo salio la Sh1000 au zaidi.Ongeza salio kwa Vocha,TigoPesa au TigoRusha.
******************************************************************************
Jaza kuanzia BUKU upate BUKU! Ongeza salio kuanzia Tsh.1000 upate nyongeza ya Tsh.1000 BURE ya Vodacom-Vodacom kwa saa 24. Maisha ni murua ukiwa na Vodacom.
 
kwa nini umesubiri kwa muda wa maika 10 ndipo unatueleza?Wakati ulipokuwa unapata mishahara kwa fedha za wizi,uliuchana.leo fedha zetu umeanzisha biashara unaamua kuwamwagia mchanga kitumbua wezi wenzako.miaka .10 kukaa kimya ni mingi sana.

Mkuu, napenda nikuhakikishie kwamba mimi sikuhusika kwa wizi huu hata kidogo. Mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye kitengo cha Corporate Solution na Marketing....wanaofanya wizi huu hasa wapo kitengo cha IT na Network.
 

tpaul big up bro.naona umeamua kuanika kila kitu. Ila Vipi hawa jamaa hawajakutafuta na kuanza kukuchimba mikwara kweli? Maana wengine wapo humu humu, kama hawa "kazi ni kwako"?
 
Last edited by a moderator:
tpaul big up bro.naona umeamua kuanika kila kitu. Ila Vipi hawa jamaa hawajakutafuta na kuanza kukuchimba mikwara kweli? Maana wengine wapo humu humu, kama hawa "kazi ni kwako"?

Mkuu, hao WAIZI bado hawajanighasi kwa kuwa wanafahamu kwamba nimesema ukweli ambao hawana uwezo wa kuukanusha. Tayari wadau wameishawaitwa waje kujitetea lakini wameingia mtini...WAIZI wakubwa!
 
Last edited by a moderator:

Wanayo internet bila kikomo ya wizi
 
Jamani tutaponea wapi?

Wisi, wisi, wisi kila kona
 
Wizi mwingine, wakati mwingine ukijiunga bandle na mtandao unapotea hapohapo mpaka masaa 24 yanaisha na haurudishiwi chako
 
Na Yona Maro, Mwananchi

Ni dhahiri wengi tumewahi kupokea ujumbe mfupi wa maneno (sms) bila wenyewe kutaka, halafu hapo hapo utaona kiasi fulani cha fedha kimeondoka kutokana na ujumbe huu.
Wakati mwingine simu haina fedha lakini unapoingiza salio tu ujumbe utaingia na fedha hiyo itakatwa. Kwa Tanzania hivi sasa tabia hii imekuwa kama ada.
Wateja wanatumiwa sms wasizopenda, lakini kibaya zaidi ni namna fedha zao zinavyokatawa kienyeji na watoa huduma wa simu za mkononi.
Katika baadhi ya nchi wameanza kufikishana mahakamani kutokana na aina hizi za ujumbe wa promosheni. Watu wanataka haki zao za mawasiliano ziheshimiwe na waamue wenyewe kama wanataka kujiunga kwenye huduma fulani au la.
Mwanasheria mmoja nchini Uganda ameifikisha mahakamani kampuni ya MTN, kwa madai ya kumtumia ujumbe mfupi wa matangazo. Mwanasheria huyu anataka kampuni ya MTN Uganda kuacha mara moja kumtumia ujumbe mfupi wa matangazo.
Anasema yeye ni mtumiaji na amesajiliwa kutumia simcard ya mtandao wa MTN, sio kwa minajili ya kutumiwa matangazo na kwamba kitendo hicho ni kuvunja haki zake.
Mahakama imeitaka kampuni ya MTN Uganda kuwasilisha utetezi wake baada ya shauri hilo kupelekwa mahakamani.
Kabla ya suala hili la mahakamani , taasisi inayohusika na usimamizi wa mawasiliano nchini Uganda (Uganda Communications Commision) ilipiga marufuku utumaji wa ujumbe mfupi wa matangazo kwa watumiaji wa huduma za simu nchini humo. Marufuku hii ilianza kutumika tangu Juni 8 mwaka huu.
UCC imetaka kampuni zote za mawasiliano nchini Uganda kuandaa utaratibu wa jinsi zitakavyoendesha huduma kama hizo bila kusumbua watumiaji wa huduma za mawasiliano hasa kwenye suala la ujumbe mfupi.
Pamoja na yote hayo kuna masuala kama matatu ambayo wateja wengi wamekuwa wakiyalalamikia ambayo yanafanana na yanayotokea hapa nchini.
Moja ni mkataba au makubaliano kati ya mtumiaji wa namba husika na mtoa huduma wake; kwamba hakuna mkataba rasmi ambao unatamka rasmi kwamba mteja amekubali mwenyewe kutumia sms za matangazo au sms zozote zile kutoka kwa mtoa huduma. Kimsingi kunatakiwa kuwepo kwa mkataba kama huu ili mteja aamue mwenyewe kama anataka kujiunga ama la.
Pili ni suala la kampuni za simu kutumia mwanya huo wa kutokuwapo kwa mkataba kuanzisha promosheni na kuzituma kwa wateja wake, kwa sababu ya sheria mbovu za mawasiliano.
Kwa yanayaotokea Uganda, ni vyema tujiandae kujadili suala na hatimaye kuliingiza katika Sheria ya Mawasiliano kwa mjadala bungeni.
Japo inajulikana kuwa kampuni zinaweza kupinga kipengele hiki, kwa sababu ndicho wanachokitumia kupata faida nono, lakini bado ni suala muhimu kuwa mteja awe na haki ya kuamua kama anataka kupokea ujumbe au la. Kuwepo na uchaguzi wa aina gani ya ujumbe mteja anataka atumiwe.
Jambo hili limekuwa likipigiwa kelele na wadau kadhaa wa mitandao ya simu, lakini kampuni zinajitetea kuwa watumaji wa ujumbe ni wengine, wao wanawezesha tu utumaji.
Katika Sheria ya Mawasiliano kuna kipengele cha faragha. Hiki kinahusika na masuala binafsi ya kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano na hapo ndipo tunapoweza kuongeza kipengele hiki cha kudhibiti matangazo au promosheni.
 
Unanunua bundle.......then network hakuna hadi muda wa bundle uishe.
Hebu tuwe tunaweka hayo matukio hapa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…