Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Nimefanya kazi kwenye kampuni mbali mbali za simu hapa nchini kwa muda wa zaidi ya miaka 10, kabla ya kuamua kujiajiri mwenyewe. Katika muda wote huo nimeshuhudia kampuni hizi zikiwaibia wateja kwa namna mbalimbali. Nimekaa na huu ushahidi kwa muda sasa lakini naona roho inanisukuma niuanike hadharani mbele za watanzania ili wafunguke macho na kufahamu UFISADI huu unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini. Nitaanika wizi wote kadri nitakavyoweza kuukumbuka hapa:

Huduma za bure
Kuna hizi huduma ambazo wanaziita huduma za “BURE” kana kwamba zinapatikana bure wakati si kweli! Kwa mfano, wateja hutumiwa SMS zinazowadanganya kwamba wanaweza kupata huduma za bure na ili wazipate wanaelekezwa kutuma ujumbe kwenda kwenye namba fulani. Na mteja akisharogwa akatuma ujumbe kwenda kwenye namba husika, imekula kwake! Nyingi ya huduma hizi zinzoitwa za bure hugharimu fedha na mara ujiungapo hujikuta unakatwa salio lako kimya kimya. Ni mara nyingi mtakuwa mmewahi kusikia mtu akilalamika kwamba salio lake limepungua….unaweka airtime ya Tsh 1000 leo bila kuitumia, ikifika kesho unakuta zimebaki sh 350! Tsh 650 zimeenda wapi? Zimekatwa kwenye zile huduma za “BURE” ulizotangaziwa.

Promosheni feki
Promosheni nyingi zinazoanzishwa na makampuni ya simu zinalenga kuwanyonya na kuwakandamzia wateja. Mfano halisi ni pale wateja wanapotangaziwa kwamba huduma ya FESIBUKU inapatika bure! Thubutuuu! Hakuna kitu cha bure nchi hii, ndugu yangu. Huu ni wizi wa mchana! Kupona kwako ni pale utakapotumia hiyo huduma ukiwa hauna salio kwa kuwa huwezi kupata access ya huduma husika (kama vile fesibuku, twita, nk). Ikiwa utafungua huduma hiyo ukiwa na salio, salio lako lote litakombwa sawia! Kuna mtandao mmoja wa simu unajinadi kwamba unatoa huduma ya fesibuku bure wakati ni uongo mtupu. Ingia kwenye hiyo fesibuku uone utakavyoliwa fedha! Aidha kuna mtandao mmoja uliwahi kuwa na fesibuku ya bure siku za nyuma (kama mtakumbuka). Kwa muda fulani huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa. Kumbe ilikuwa ni janja ya nyani…..baadaye ile “bure” ilifutwa kimya kimya, wateja wakaendelea kukamuliwa kama kawaida na mpaka leo hawajawahi kuwataarifu wateja wao kwamba hiyo “bure” imesitishwa! Kuna wateja wengi sana, hasa wa kule vijijini, ambao wanaendelea kukamuliwa kwa kujidanganya kwamba huduma ni ya bure hadi leo, kumbe ilishasitishwa kitambo sana!

Ulaghai wa Kimangungo
Kuna wakati ambapo makampuni ya simu hupandisha tariffs kimya kimya bila kuwataarifu wateja wake na kuendelea kuwaibia bila kujua. Mwaka 2006 gharama za kupiga simu, kutuma sms na kutumia data zilipandishwa kinyemela na wateja wakaendelea kukamuliwa fedha kimya kimya hadi pale baadhi yao waliposhtukia dili na kuja juu. Aidha, prosheni fulani zinapoanzishwa, kama vile punguzo la gharama za kupiga simu nyakati za usiku, pindi zinafikia tamati wateja hawapewi taarifa na kujikuta wakitumia fedha zaidi ya matarajio yao. Promosheni inapoisha kampuni hizi huwakataza wafanyakazi wake wasiwaambie wateja ili waendelee kukamuliwa fedha kilaghai. Huu ni wizi, tena wa mchana na hauna tofauti na ufisadi wowote ule.

Kutotoa taarifa kwa wateja kwa makusudi
Wateja wanapojiunga kwenye vifurushi mbalimabli huletewa taarifa immediately via SMS kwamba wamefanikiwa kujiunga lakini kifurushi kikiisha ama wateja huchelewa kutumiwa meseji ya taarifa au hawatumiwi kabisa. Hili tatizo huwakumba zaidi wale wateja wanaopenda kubaki na salio kubwa kwenye simu zao. Kwa mfano, mtu unanunua vocha ya Tsh 2000 kisha unanunua kifurushi cha Tsh 500 na kubakiwa na Tsh 1500 kwenye simu. Pindi kifurushi cha 500 kikiisha hutatumiwa ujumbe wowote hadi utapokuwa umekausha 1500 zilizosalia kwenye simu. Huu pia ni wizi wa mchana na unaofanywa kwa makusudi na kampuni za simu hapa nchini. Ninao ushahidi usiokuwa na mashaka katika huu wizi wa makusudi.

Njia nyingine inayotumika kuiba hapa ni kutotoa call details pindi upigapo simu. Ukimaliza kupiga simu ukiangalia call details unakuta inasoma 00:00:00! Details hizi zinafichwa kwa makusudi ili kujenga mazingira ya wizi. Kwa mfano mtu unaongea kwa dakika 3, wao wanakata dakika 4.30 na kukuibia dakika 1.30! Matokeo yake unakuta muda wa hewani uliopewa wakati wa kujiunga umeibiwa na kampuni kwa maslahi yake binafsi. Lakini pia kuna wizi mwingine huu hapa: – unaponunua kifurushi hupewa dakika ambazo ungetegemea zizotozwe kwa sekunde (per second billing) lakini badala yake hutozwa kwa dakika (per minute billing) kinyume cha mkataba kwa lengo la kumkamua mteja kiujanja. Huu ni wizi na haukubaliki hata kidogo.

Kuvuruga mawasiliano kwa makusudi
Kuna wakati wahandisi wa kampuni husika hupewa jukumu la kuvuruga mawasiliano ya wateja ili watumie muda mwingi na pesa nyingi kwenye maongezi. Inakuwaje hapa? Inakuwa hivi: Ukimpigia mtu yeye anakuwa anakusikia lakini wewe humsikii au vice versa. Hii husababisha kutumia muda mwingi kuelewana wakati huo salio likinyonywa kama kawaida – hata kama mkichukua muda mwingi kuelewana salio hutafunwa sawia! Njia nyingine inayotumika hapa ni kuvuruga access to customer care ili unapokuwa umepatwa na tatizo usiweze kuwafikia watu wa huduma kwa wateja kupata msaada. Hii ndio sababu 90% ya wateja wenye matatizo genuine hawaipati namba 100. Mtu unaweza kupiga siku nzima na usiunganishwe kuongea na mshauri. Hatimaye wengi wao hukata tamaa na kuamua kukubali “kuliwa”!

Hii ni sehemu ya ushahidi ambao nimeukusanya while working with different mobile companies in Tanzania. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Nawasilisha.
Nimejifunza kitu kikubwa sana hapa itabidi kubuni mbinu mpya za kuhakikisha hakuna cha ziada kinaliwa
 
yaani@voda ndo mababa wa utapeli mi siku hizi ni airtel afadhali
 
tigo na voda jamani kamisheni wanatuibia sana kuweni akini hakikisha hufuti message kabla ya ku zirokod kwenye kitabu mwisho wa siku ukiona kamisheni ndogo nirahisi kupiga hesabu zqko na kuwakamata ukienda kulalamika wanajisikiaga noma balaa acheni kutuibia mchaa kweupe mnatia aibu
 
Mzee hilo la kutokupewa taarifa kifurushi kinapokwisha ni la kweli kabisa. Mimi nishaliwa hela nyingi kwa mtindo. Kuna demu mmoja yeye alitaka kulia, alikua na laki mbili za salio kwenye simu yake. Sasa alijiunga na kifurushi so akawa comfortable kutumia internet. Wakati anaendelea kutumia kifurushi kikaisha na wazee wa mtandao wakaanza kumkata. Huwezi amini laki mbili zilikatwa usiku mmoja tu. Just imagine internet gani hiyo ya kumkata mtu laki mbili usiku mmoja!!!!

Sasa dawa yao ni moja tu. Mimi sasa hivi pesa zangu siweki salio moja kwa moja nazihifadhi kwenye tigopesa au easy pesa. Kila siku natoa 600 najiunga kifurushi, kikiisha simu inakuwa zero , najiunga tena.
 
Hakuna Kinachokera Vodacom kushindwa kunipa taarifa pindi kifurushi kinapoisha matokea yake mpaka wakwangue salio lote lililobaki ndio wanatoa taarifa.

Na usiombe kama unasalio kwenye simu, hata kama una elfu kumi haidawnlod hata Mb 20
 
tpaul nimetumiwa ujumbe huuu leo na hawa rafiki zangu. Sijui huu wema wameutoa wapi huko
Ndugu mteja! Tafadhali jibu OK Kwenda 155100000051 uanze kuongea BURE Tigo-Tigo saa 24 na tuma SMS BURE BILA KIKOMO SIKU 7. Jibu message hii kati ya leo hadi tar 30/11.
 
Last edited by a moderator:
Haya makampuni ya simu ni wanyonyaji wakubwa sana' na si kwamba serikali haijui wanajua sana' ila wahusika kuna kamisheni wanapata! Hata mishahara ya wafanyakazi hasa wale waliopo kwenye hivyo vitengo vya kuiba na kutudanganya! Wanatuumiza sana kikweli! Hamna wenye nafuu wote majizi makubwa! Pumbavu zao
 
Nashukuru sana kwa taarifa ila sisi watanzania tunatakiwa tuwe na chama cha watumia simu ilo kuhskikisha haki zetu zinasikika. Ni bahati mbaya tume ya mawasiliano haina meno ya kusaidia wananchi ila nina hakika tukiungana hawa wezi tutawaona mchana kweupee!
 
Mzee hilo la kutokupewa taarifa kifurushi kinapokwisha ni la kweli kabisa. Mimi nishaliwa hela nyingi kwa mtindo. Kuna demu mmoja yeye alitaka kulia, alikua na laki mbili za salio kwenye simu yake. Sasa alijiunga na kifurushi so akawa comfortable kutumia internet. Wakati anaendelea kutumia kifurushi kikaisha na wazee wa mtandao wakaanza kumkata. Huwezi amini laki mbili zilikatwa usiku mmoja tu. Just imagine internet gani hiyo ya kumkata mtu laki mbili usiku mmoja!!!!

Sasa dawa yao ni moja tu. Mimi sasa hivi pesa zangu siweki salio moja kwa moja nazihifadhi kwenye tigopesa au easy pesa. Kila siku natoa 600 najiunga kifurushi, kikiisha simu inakuwa zero , najiunga tena.

Laki mbili inaweza ikaisha tena kwa masaa machache mkuu,inategemea unatumia simu yenye uwezo gani na unafanya nin kwenye internet,kuna watu wanadownload videos au wanaangalia videos youtube...so kutumia laki mbili overnight kama hujajiunga na bundle ni very possible mkuu.
 
Mengi ya unayo yasema kwangu binafsi nimeyaona kitambo ila hayakwepeki , TCRA wana titazama tu tukinyonywa.mfano wa kutotoa taarifa pindi kifurushi kikuishiapo katikati ya matumizi, na makato yasio na taarifa.

Haishangazi, ndio maana wanasiasa wakubwa ama wana hisa ktk haya makampuni ya simu, au wanateuliwa kuingia kwenye bodi za makampuni hayo.

Nia na malengo yao ni kuhakikisha wanatuibia huku waliopaswa kuwa watetezi wetu wakionjeshwa asali kwa gharama yetu.

Vv
 
Kuna jamaa mmoja ambaye kwa sasa ana uwezo na mamlaka ya kufanya jambo juu ya wizi huu. Sijaona akifanya lolote. Ajabu ni kwamba eti naye anautaka "urahisi". Kweli Tanzania haiishi vituko!!
Januari???
 
VODA wanaib jameni ...yuuuei.
Ukinunua soda ukaingiza zile namb kwenye kisude ile sms ikiwafikia ndo wsnsanza kuhesabu hizo dk 5, ikifika dk ya 4 ndo unapata sms keamba umefanikiwa kuunganishwa ,ukipiga unaambiwa ushatumi mda wako wa bure.

Hawa share holda watamjibu nn Mungu wa İsrael ?


Hayo yamenikuta juzi tu. Ni wizi mtupu halafu wanavyokomaa kuitangaza hiyo promosheni....
 
Back
Top Bottom