Jinsi Introverts wanavyopata tabu kuingiliana na watu wanaowazunguka

Watu kama dr Shaun Murphy naamini ndio hawa introvert waukweli
images%20(1).jpg
 
Jitahd kukaa maeneo yenye watu wanaopiga story mfano kwny vibandaumiza n.k mm ni introvert ila sometimes naongea mpaka huezi amini kama ndo mm.
Kwa mazingira niliyopo hakuna vijiwe wala vibanda umiza labda uende bar nami siendi sehemu hizo. Lakini hata nikisema nijichanganye bado sikawii kuboreka, kwanza hua naona stori zao hatuendani napenda marafiki zangu wawe na miaka 35+
Shida yangu kubwa ni aibu na kutoweza kuongea mbele za watu
 
Duuuh kumbe hii tabia ya kupenda kujitegemea n kwa introvert wote asee. Mm home cjawahi kuznguliwa chochote yaan mda mwngne narud saa 7 usku lakn hakuna anaeniuliza. Lakn nliamua tu kutafta geto langu yaan nlijikuta tu nlijiskia tu kujitegemea
Ndio mkuu afu ndio maana wagunduzi wa vitu vikubwa hapa duniani ni introverted. Hautegemei mawazo sana ya watu. Hapa natoka chuo soon ola nyumbani hawajui ya kuwa Januari nasepa home.
 
Ndio mkuu afu ndio maana wagunduzi wa vitu vikubwa hapa duniani ni introverted. Hautegemei mawazo sana ya watu. Hapa natoka chuo soon ola nyumbani hawajui ya kuwa Januari nasepa home.
Introvertism inaenda sambamba n higher intelligence. Introverts wengi wanauwezo wa kufikiria karibia wanasayansi wote walikua Introverts.
Hatupendi kua tegemezi wala kusaidiwa
 
Nachojikubali mimi kama mtu wa hii calibre ni kuwa tunapenda kutumia efforts zetu hatupendi slope lbda iwe ni kwa issue kubwa sana. In short tunapenda kutumia nguvu zetu kutatua mambo. Ila nguvu zetu zikifika. Kikomo ndio huomba msaada kwa wale wanaotuelewa. Mf mimi nilivokuwa nasoma nikiishiwa pocket money ni hadi mzazi mwenyewe ashtuke. Kuna likizo fulani imefika siku ya kufunga shule mie nimejiwekea kiakiba changu kama nauli wala sijaomba hela kitambi nyumbani basi mzazi akahisi hizi si tarehe za kufunga chap akaagiza mtu aniletee hela shule. Cha ajabu nilivofika home pesa yao nikawapa.
Napenda kujitegemea aisee.
ulikuwa darasa la ngapi?
 
Hivi wenzangu mnawezaje kufit In na watu??
Kiukwekeli naishi kama niko mwenyewe duniani, Najitahidi sana kujaribu kua karibu na watu naomba namba za watu ila nikishachukua namba tu naifuta. Yaani simu yangu kukaa wiki haijapigiwa wala kutumiwa text ni kitu cha kawaida coz tatizo lipo kwangu I push people back.
Mtu akijitahidi kua nami karibu na mawasiliano nawahi kuboreka namblovk au sijibu jumbe zake... I'm living Vagrantly asee.

Basi Mungu angenipa uwezo mzuri wa kuzungumza mbelel za watu.. Hii kitu inanitesa sana (being introvert) wala sijidai maana nakosa mengi na siijui maisha yangu yatakuaje huko mbeleni
John Joba
mzee unateseka kuwa introvert?? aisee nina maongezi marefu na wewe PM
 
Kwa mazingira niliyopo hakuna vijiwe wala vibanda umiza labda uende bar nami siendi sehemu hizo. Lakini hata nikisema nijichanganye bado sikawii kuboreka, kwanza hua naona stori zao hatuendani napenda marafiki zangu wawe na miaka 35+
Shida yangu kubwa ni aibu na kutoweza kuongea mbele za watu
una demu?
 
Introvertism inaenda sambamba n higher intelligence. Introverts wengi wanauwezo wa kufikiria karibia wanasayansi wote walikua Introverts.
Hatupendi kua tegemezi wala kusaidiwa
ushasoma kitabu chochote kuhusu introverts?
 
introverts wote wana sifa hizi

  • Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
  • Ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
  • Wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
  • Ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
  • Wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati

- Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)

Sifa zao nyingine ni pamoja na;

  • Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
  • Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine

- Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)

- Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasani si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)

- Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)

  • Wakata tamaa wanapokosolewa.
  • Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.

Nyinginezo ni;

- Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)

- Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo.

  • Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
  • Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao

- Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa).

- Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.

- Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.

- Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe.

- Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani

Pia, wanafahamika kwa;

- Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)

  • Wana busara na hekima nyingi
  • Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
  • Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
  • Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
  • Ni kundi la watu wanoridhika haraka

- Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa.

- Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.

  • Kundi linalopenda amani na utulivu
  • Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto

- Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu.

Wana sifa nyingi sana, nyinginezo ni;

- Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa

  • Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
  • Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
  • Wakati mwingine hupenda kujikataa.
  • Ni waaminifu na wasema ukweli
  • Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
  • Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
  • Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu

- Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick

Kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tamaa mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani].

- Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}

- Kwa upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua.
Mwenyezi Mungu akubariki na azidi kukupa afya njema na kukuepusha na shari pamoja na mitego ya wanadamu.
Hakika wewe ni mwanga (Light) na sio Giza (Dark) usichoke kuandika na kuyaishi maisha mema. Hili kufungua mlango wa maarifa na kuongeza kujitambua na kuyaishi maisha matakatifu.
Najua wewe ni Grateful person, sometimes unakatishwa tamaa na Ungrateful people.
Don't regret to be such a kind of person..........Always be Grateful and Humble.
Be blessed The Man Of Wisdom

sina mkuu🙄
🤭🤭🤭🤭😆😆😆😆
 
Hivi mwendazake anaangukia kwenye kundi gani hapa nimewaza tu maana walimpa sifa za shujaa wa Afrika
 
Mwenyezi Mungu akubariki na azidi kukupa afya njema na kukuepusha na shari pamoja na mitego ya wanadamu.
Hakika wewe ni mwanga (Light) na sio Giza(Dark) usichoke kuandika na kuyaishi maisha mema. Hili kufungua mlango wa maarifa na kuongeza kujitambua na kuyaishi maisha matakatifu.
Najua wewe ni Grateful person, sometimes unakatishwa tamaa na Ungrateful people.
Don't regret to be such a kind of person..........Always be Grateful and Humble.
Be blessed The Man Of Wisdom


so ukiishi maisha mema milango ya maarifa inafunguka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mates;

Binaadamu tumeumbwa kwa matabaka tofauti tofauti sio wa rangi wala jinsia, katika upande wa Personalites binaadamu yupo katika makundi mabalimbali. Kuna Makundi makuu mawili ya personalities,ambazo ni Extroverts na Introverts. Kwa upande wa introverts dunia kwao si kikwazo au haina kikwazo chochote ambacho kinaweza kuwafanya wasisonge mbele au kupata yale wanayoyahitaji.

Upande wa Introverts mambo ni tofauti sana sana, wao dunia si mahali salama kwa muono wao na inakua ni ngumu sana kwao kupata yale wanayoyahitaji humu duniani. Introverts wanaamini au wanaiona dunia ist the bed of roses na unaweza kuishi na ku-Earn yale unayoyata bila kutumia nguvu kubwa sana ya mwili ila ya akili.

Bahati mbaya dunia haipo hivyo, dunia imejaa michongoma hii inawafanya introverts kuona hawafit kuishi duniani hapa ila ndio wapo sasa inabidi wakubaliane na matokeo.

Kama tunavyoelewa kua Extroverts ni watu Fulani ambao ni waongeaji wazuri na hawana aibu hata kidogo wakitaka kitu watakueleza mojakwamoja ila Introvert ni watu wasio na uwezo wa kujieleza vizuri na wana aibu sana, mara nyingi hutuia muda mwingi katika kufikiri na kutafakari vitu vipya!

Aliyeumba hizi aina kinzani za watu hakua mjinga, alikua na maana kubwa sana kuwaweka pamoja hapa duniani, katika hizi pande mbili kinzani zimeunganishwa na kitu kimoja ambacho ni Kutegemeana katika mazingira. Pande zote mbili zinategemeana mno kwa kiasi kikubwa kwakua introvert wanatumia muda mwingi kufikiria na kutafakari vitu basi hawa walijaliwa Creative and Genius mind!

Ukiangalia maandeleo katika Nyanja ya dunia hii yameletwa na watu ambao ni Introverts. Lakini Introvert person akiungana na extrovert person basi hua wanatengeneza the best duo, Introvert hua anamtumia huyo extrovert kama mdumo wake au nguvu yake huku yeye akitumia akili yake zaidi katika mambo japo maranyingi sana hua extroverts wanawatapeli introverts baada ya muda.

NB, sio kwamba extrovert hua hawana uwezo wa akili no, ila siku zote mtu anayeanza kutafakari maneno wakati wewe uko unaongea muheshimu sana, lakini pia usichanganye introvert na kibuli.

Wapo watu wengi walikua ni introvert wakaungana na extrovert wakatenda mambo makubwa hapa duniani Nitatoa baadhi ya mifano

Mussa
Huyu jamaa alikua nae ni introvert, hana uwezo mzuri sana wa kujieleza ndio maana alipoitwa na Mungu alimuuliza atawezaje kuzungumza nao wakati hawezi kuongea vizuri? Mungu akampatia msaidizi wake amabae ni Aaron, walitengeneza moja ya kolabo bomba hapa duniani nadhani mambo waliyofanya tunayajua na yataendelea kuwepo daima

Tesla
Tesla alikua ni introvert aliyepitiliza, alijua duniani kila mtu ni mwema kama yeye. Alikutana na bwana Thomas Eddison wakafanya kazi pamoja mpaka leo umoja wao ndio unatufanya tunaweza kuchati hapa, bahati mbaya Thomas alimdhurumu tesla ila hakujali kufa maskini alishukuru tu kua akaili yake imeweza kuleta maendeleo duniani.

Mark Zuckenburg
Binafsi hua nikiamuangalia tu mark namuonea huruma tu kwa munekano wake, ni moja kati ya watu amabao wana Innocent face, ukimuangalia tu unamuhurumia. Ni watu wachache sana wenye hiyo haiba yay a kuonekana wanatia huruma. Mark ni introvert maisha yake chuoni alikua sio muongeaji hata ukimuudhi vipi hua anabaki kimya.

Kuna kipindi kama miaka 2 imepita ilitokea mgogoro kwamba mark kaiga ile technology ya kuangalia game in vitual reality. Ikatakiwa alipe pesa, ilimuuma mno ila hakuongea alibaki nalo rohoni. Rafiki yake mkubwa amabae amemsaidia sana kufanikisha facebook kufika hapa ilipo ni Eduardo Sevarin. Eddu alikua muongeaji tu na mtafuta masoko na investors mpaka leo umoja wao huo ndio umeawafikisha hapa mark ni billionea.

David Benioff
Huyu jamaa ni moja kati ya watengenezaji wa tamthiria ya game of thrones, nayeye sio muongeaji kama walivyo introverts wote pia ana aibu mno. Anar rafiki yake waliyekutana nae chuoni anaitwa Daniel Brett Weiss (D.B.Weiss) naye huyu ni moja ya watengenezaji wa tamthiria hii. Ila huyu DB Weiss hana aibu hata kidogo na nimuongeaji sana.

Hata wakiwa kwenye interview maswali yanayomuhu David benioff hua anayjibu yeye the funny thing ni kwamba walipokua wanafanya casting ya actors labda kama kuna actor Fulani ambaye the next season alitakiwa afe David Benioff alikua hawezi kuwaambia eti anaogopa! So aliyekua anafanya kazi hiyo alikua ni DB Weiss tena kwake ilikua rahisi mno.

View attachment 1526082

Issack Newton
Kama kawaida ya introverts wote basi Newton pia hakua na marafiki kabisa alipenda kujifungia ndani ya maabara yake kufanyia tafiti fikra zake na kujipa nafasi ya kufikiri zaidi. Alikua anamsemo wake anasema kwamba “ Plato is my friend, Aristotle is my friend, but my best friend is truth” Lakini naye alikua na rafiki yake ambae alikua ni muongeaji mzuri/Extrovert aliitwa John Locke. Huyu ndio alikua rafiki pekee wa Newton na yeye ndio aliweza kumuelezea vizuri tabia zake za upweke japo baadae walishindwana urafiki wao. Maana Muda mwingi Newton alikua bize.

Albert Eintein
Albert alipohamia Switzerland akaanza kufanya kazi kwenye ofisi za Patent right (haki miliki) ndipo alipoanza kufanyia kazi Hobby yake pendwa ya Kufikiria. Ofisini kwake kulimwezesha kufikiria maana hakua na kazi ngumu, kupitia dirisha lililokua ofisini mwake aliweza kuformulate theory of relativy maana alikua anautafakari mwanga uliokua unaingia ofisini mwake kupitia dirishani….Japo alikua ni mtu mmoja mkimya sana na alikua anaongea kila baaada ya kutafakari sana anachotaka kuongea pia alikua na rafiki yake wa karibu toka zamani ambae wamesaidiana mengi si mwingine ni Michelle Besso. Beso ndio alikua rafiki yake mkubwa na kumuwezesha Albert kufanya mengi makubwa.

Mifano ni mingi sana ya urafiki wa introverts na extrovert, watu maarufu ambao ni Introverts..na wametenda mengi makubwa duniani mfano:

Albert Einstein,Rosa Parks,Bill Gates,Steven Spielberg,Sir Isaac Newton,Eleanor Roosevelt, Mark Zuckerberg,Larry Page,Al Gore,Marissa Mayer, Abraham Lincoln,
JK Rowling,Warren Buffett, Mahatma Gandhi,Hillary Clinton, Michael Jordan,Meryl Streep,Elon Musk,Dr. Seuss,Frederic Chopin

Introverts kwakua wao hawawezi kuingiliana vizuri na jamii waliyomo hivyo basi muda wao mwingi hua wanautumia kwenye mitandao ya kijamii. Huku kwenye jamii hawana attention kwa watu so wanachofanya ni kutafuta attention mitandaoni at any cost. Introvertism,Geniusity,Lonelness na Ugonjwa wa akili ni vitu vinavyoenda sambamba. Ukikuta mtu anaandika mapost marefu,anatukana au kuudhi watu mitandaoni usimchukie.

Muhurumie sana maana anakua muhanga wa matatizo niliyoyaainisha hapo juu. Wanafanya kuudhi watu ili nao waonekane kama wanaweza kufanya kitu, wanajitahid kufit in ila bahati mbaya wanatumia approach mbaya ya kuudhi watu.. Introverts ni watu poa sana, wana mioyo mizuri sana na wana akili zenye uwezo mkubwa.

-Vinci
Moja ya nyuzi makini kabisa jamii forum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wenzangu mnawezaje kufit In na watu??
Kiukwekeli naishi kama niko mwenyewe duniani, Najitahidi sana kujaribu kua karibu na watu naomba namba za watu ila nikishachukua namba tu naifuta. Yaani simu yangu kukaa wiki haijapigiwa wala kutumiwa text ni kitu cha kawaida coz tatizo lipo kwangu I push people back.
Mtu akijitahidi kua nami karibu na mawasiliano nawahi kuboreka namblovk au sijibu jumbe zake... I'm living Vagrantly asee.

Basi Mungu angenipa uwezo mzuri wa kuzungumza mbelel za watu.. Hii kitu inanitesa sana (being introvert) wala sijidai maana nakosa mengi na siijui maisha yangu yatakuaje huko mbeleni
John Joba
Tunapata shida sana hii hali nnayo mm siwez interact na watu asee nko very selective kwenye marafiki in short sina marafiki wengi,nnapenda kukaa ndan muda mrefu ,furaha yangu ni kusafiri kimawazo
 
Back
Top Bottom