#COVID19 Jinsi Corona inavyoweza kuwa Fursa kwa jamii

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Hapa nitatolea mfano ambao upo unaishi jinsi mjasiriamali anavyo weza badili Tatizo kua Fursa.

Dunia nzima bila shaka umekubwa/Ishawahi kukubwa na janga hili la CORONA Tangu mwaka 2019 ikiwa ni covid 19.

Kwa wajasiriamali Kuna slogan ambayo hupenda kuitumia kwamba Badili Tatizo kua Fursa.

Ukiachilia mbali Hasara na matatizo ya CORONA, hivyo bado CORONA ilileta Faida kwa jamii na Watu wengine japo si wote.

Pengine unaweza kupata ukakasi kwamba kivipi CORONA ambalo ni janga hatari liwe faida kwa wengine?.
Naam, hapa nitakurudisha nyuma kidogo.

Ni kwamba corona ni faida kwa wajasiriamali na wafanyabishara wengine pia pamoja na kada nyingine tofauti.

Tuanze kwa kumjua mjasiriamali

Mjasiriamali: ni mtu ambaye anatoa mda wake, nguvu zake na rasilimali zingine kwa kuwekeza katika ubunifu au kuendeleza kitu kwa matarajio ya faida na kupuuza matatizo.

Ukiangalia baadhi ya sifa za mjasiriamali zinamfanya anafaidike na baadhi ya fursa zinazo jitokeza.

Mfano wa sifa za mjasiriamali ni Mtu mwenye maono,mvumbuzi, anaye pambana na matatizo na sifa zingine.

Jinsia Coronavirus ilivyo geuka fursa
Kipindi cha maambukizi ya CORONA biashara nyingi zilitokea kwa mfano.

Uuzaji barakoa na utengenezaji, uuzaji vitakasa mikono na utengenezaji wake.

Pia kipindi hicho ndo Tanzani ilipanda na kufikia uchi wa kati wa kiwango cha chini pamoja na utajiri wa Jeff uliongezeka wakati wa kipindi hicho kwa ongezeko la mauzo ya mtandao wake wa Amazon.

Licha ya hayo kipindi cha coronavirus Awamu ya kwanza tulivyo tangaziwa Baadhi ya vitu kusaidia kupambana na corona kama vile Kikao na tangawizi biashara yake ilipanda gafla.

Hivyo vijana na Watu wengine wawe wabunifu katika kuvumbua tatizo na kulifanya fursa.

Badili Tatizo kua Fursa
 
Back
Top Bottom