Uchaguzi 2020 Jinsi CCM ilivyo wafukarisha Watanzania kwa miaka 60

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,459
17,268
Kwa kingereza ungeweza kusema how CCM underdeveloped Tanzanians for 60 years.

Kwa miaka 60 chini ya CCM bado huduma za afya sio za uhakika Tanzania. Wamama wajawazito wanafariki kila siku kwa kujifungua, watoto wachanga wanakufa kwa kukosa huduma. Vituo vya afya havina madawa wala vifaa tiba ila CCM watakwambia wamenunua ndege.

Kwa miaka 60 chini ya ccm wanafunzi bado wanasomea kwenye miti kama nyani na kukaa chini kama mbuzi, hakuna waalimu, hakuna vifaa vya kufundishia halafu ccm watasema wamejenga daraja la Ubungo.

Miaka 60 chini ya CCM hakuna miundombinu ya maana, mipango miji ya hovyo, hakuna maeneo ya kufanyia biashara kwa wafanya biashara wadogo, hakuna maeneo ya wazi wala viwanja vya michezo hasa kwenye miji, CCM watasema wamenunua ndege.

Kwa miaka 60 hakuna mazingira mazuri ya kujiajiri, unatakiwa ulipe kodi kabla hujaanza biashara au kujiajiri. Miaka 60 bado serikali ndiyo inategemewa kama muajiri mkuu. Maendeleo yatapatikana wapi?

Miaka 60 tunaambiwa kununua ndege na kujenga madaraja ndio maendeleo, miaka 60? Wakoloni walijenga barabara, mabwawa ya umeme, walinunua ndege, walijenga hospitali, shule, vyuo, je na wao walileta maendeleo? Kama walileta maendeleo leo hii CCM inafanya ambayo wakoloni walifanya miaka 60 iliyopita na inatuambia ndio maendeleo.

Watanzania kuendelea kuichagua CCM ni kwamba tumekubali kuwa tuendelee kua masikini.
 
John yeye ktk miaka 5 hii alijikita kuwafukarisha matajiri. Sijui lengo lake nini?
 
Kwa kingereza ungeweza kusema how ccm underdeveloped Tanzanians for 60 years.

Kwa miaka 60 chini ya ccm bado huduma za afya sio za uhakika Tanzania. Wamama wajawazito wanafariki kila siku kwa kujifungua, watoto wachanga wanakufa kwa kukosa huduma. Vituo vya afya havina madawa wala vifaa tiba ila ccm watakwambia wamenunua ndege.

Kwa miaka 60 chini ya ccm wanafunzi bado wanasomea kwenye miti kama nyani na kukaa chini kama mbuzi, hakuna waalimu, hakuna vifaa vya kufundishia halafu ccm watasema wamejenga daraja la Ubungo.

Miaka 60 chini ya ccm hakuna miundombinu ya maana, mipango miji ya hovyo, hakuna maeneo ya kufanyia biashara kwa wafanya biashara wadogo, hakuna maeneo ya wazi wala viwanja vya michezo hasa kwenye miji, ccm watasema wamenunua ndege.

Kwa miaka 60 hakuna mazingira mazuri ya kujiajiri, unatakiwa ulipe kodi kabla hujaanza biashara au kujiajiri. Miaka 60 bado serikali ndiyo inategemewa kama muajiri mkuu. Maendeleo yatapatikana wapi?

Miaka 60 tunaambiwa kununua ndege na kujenga madaraja ndio maendeleo, miaka 60? Wakoloni walijenga barabara, mabwawa ya umeme, walinunua ndege, walijenga hospitali, shule, vyuo, je na wao walileta maendeleo? Kama walileta maendeleo leo hii ccm inafanya ambayo wakoloni walifanya miaka 60 iliyopita na inatuambia ndio maendeleo.

Watanzania kuendelea kuichagua ccm ni kwamba tumekubali kua tuendelee kua masikini.
Na hivyo hawapaswi kuendelea kutuongoza. Wamefeli na wameshiba maana wao ni mabilionea.
 
bila ya kuwa na serious upinzani kuna 60 nyingine coming...

Back
Top Bottom