Jini mahaba chanzo cha wadada wengi kutoolewa

Jini mahaba chanzo cha wadada wengi kutoolewa

Haya mambo yapo kweli.Ubaya ni hadi yakukute au yamkute mtu wako wa karibu ndio utaamini.

Hii haina tofauti na wale wanaoshindwa kufanikiwa kielimu au kimaisha kwasababu za kishirikina.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna Mambo hayo.
Wanafunzi wasome shule wafaulu.
Hakuna uchawi wa kumloga mtu asifanikiwe kielimu.
Wengine tusingesoma. Maana waliotuombea mabaya walikuwa wengi.
Vijana tufanye kazi tusitegemee miujiza. Ukiwa mvivu au mchaguzi wa kazi za kufanya unapoteana tu.
Unaishia kulalamika kulogwa.

Huku kurogwa kupo Africa tu na wanaoombea kurogwa ni wachungaji wa kiafrica tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majini mahaba yapo wajameni....yaani live bora ilo anaona ndotoni kuna mtu alikuwa anatembea nalo wameshikana mikono mpaka mchana na lilimtambulisha mpaka kwa ukoo wake ilo jini...linamnunulia viatu vya shule linampa Pesa...na ole wako umtongoze utakoma....inshort hata wanaume na wanawake wengi yanawapitiaga hawawezi tuu kufunguka
 
Kila kitu kinaanzia kwenye kuwaza kwako,

Wadada Wana kasumba ya kuishi maisha ya marafiki, majirani na ndugu zao. Anakua hana maamuzi yake kamili.

Matokeo yake akipata bwana anaanza kumgrade kwa kuangalia marafiki, ndugu na majirani, Mwishowe wanashindwana na bwana
Visirani na hasira Za kukosa chaguzi sahihi vinakua anakua mtu wa kukataa wanaume.

Siku akijitambua akipata mtu wakakaa anasema jini limeondoka kumbe amejitambua.

[emoji252] [emoji479]
 
Wakuu,

Nimesimuliwa na rafiki yangu aliyeteswa na jini mahaba zaidi ya miaka 32...

Yawezekana umewahi sikia kuhusu jini mahaba...mimi pia nilikuwa nikisikia watu wakimueleza na namna anavyomuoa mdada bila yeye kujua.

Pia majini mahaba ambayo huwa na mahusiano na wadada na wanajua hata hufurahia kuwa nayo.

Inasemekana jini huyu mara nyingi humpenda mdada na kuanza kumfuata katika ndoto.


Kisa kipo hivi...


Rafiki yangu anasema wakati akiwa amelala usiku alikuwa akiota ndoto za kufanya mapenzi.

Anasema mwanzoni aliona ni kawaida, ila aliumia tu....maana alikuwa anapata mwanaume lakini anamuacha.

Anazidi kueleza pia ilifika wakati miaka ilienda ila hana mahusiano ya kudumu.

Hadi ndugu na watu wa karibu wakawa wanamuuliza mbona huolewi na uzuri wote huo?

Ananiambia aliumia na kulia alisali ila wanaume walizidi kumjia wakitembea nae na kumuacha...hadi ilifika wakati wanasahau wanamtongoza upya.

Na kuna wakati wale wa zamani waliomuacha wanamjia na kutaka kutembea nae tena ...maana wengine walioa na wengine bado.


Jinsi jini mahaba alivyomjia ndotoni...


Wakati anamjia ktk ndoto huota kama anafanya mapenzi na ndugu yake wa kiume au wakati mwigine rafiki wa karibu wa kike au wa kiume.

Ndoto hiyo humfanya afurahie na baada ya kushtuka ndotoni hujiona amefika kileleni.

Wakati mwingine huota ndoto ya kuona utupu wa mwanaume na sio sura ya mwanaume.

Anasema ndoto nyingine huota akiwa yeye na mwanamke mwenzie wakisagana.

Baada ya kushtuka ndotoni moyo wake hujuta na kulia sana...

Anasimulia zaidi akisema...dalili nyingine aliyokuwa nayo ni hamu ya tendo la ndoa lililopitiliza na wakati mwingine kujichua.

Anadai kuwa alikuwa hana tofauti na kahaba kwani idadi ya wanaume aliolala nao hakuikumbuka...

Alihangaika sana lakini hakujua chanzo
cha matatizo...

Kama ilivyo Mungu husikia vilio vya watu wake...alisikia kilio chake na baadae akaja kuombewa na kujulikana na jini mahaba...akapona

Sasa amepata mchumba....tunasubiri ndoa












Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka 32 ameteswa na jini mahaba,kwahiyo ndio kusema anaolewa akiwa n umri gani kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna Cha jini mahaba wala nini.
Ni tabia tu ya kuwa selective na uasherati.
Tunapokosa tunachokitaka hatukosagi wa kumsingizia.

Mungu yupo na hawezi kukuacha mwanadamu uteseke bila wewe kuanza kujitesa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo kipindi Yesu anatoa pepo Mungu hakuwepo?

Kuna mambo yanatokea ili Mungu ajidhihirishe, ila kumbuka pia kuna mfalme wa dunia hii na amewateka watu wengi sana.
 
Back
Top Bottom