Jina la Ukoo wetu!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Wadau,

Je jina la ukoo huanzia wapi katika mfululizo wa ukoo?

Nilijaribu kuangalia familia yangu nikagundua kuwa kuna utata, NA HASA baada ya huu utaratibu wa majina ya kizungu!

Mjukuu wangu anaitwa Samsoni.
Baba yake, ambaye ni mwanangu anaitwa Paulo.
Mini ninaitwa Damas.
Baba yangu anaitwa Julius.
Babu yangu (ambaye alibahatika kubatizwa) anaitwa Yohana Mandiga.

-Je inawezekana mtoto wa mwanangu akatumia jina langu kama la ukoo, au na yeye lazima ajiite ukoo wa Mandiga?

-Je yawezekana mtu kutumia jina la ukoo la kizungu mfano Yohana?

-
Jina la ukoo linaanzia nyuma kiasi gani kutoka kwangu?....au hakuna fomula?
 
Ilipaswa uitwe Damas Yohana Mandiga na hapo jina lenu la ukoo ni Mandiga sasa kwa kutumia majina ya ubatizo la kwako na la baba la ukoo unalipoteza.
 
Ilipaswa uitwe Damas Yohana Mandiga na hapo jina lenu la ukoo ni Mandiga sasa kwa kutumia majina ya ubatizo la kwako na la baba la ukoo unalipoteza.

na babayake ataitwa julius yohana mandiga, then baba na mwana wanakuwa kama m2 na mdogo wake
 
Mandiga ndio la ukoo.

Nakubaliana na wewe. Lakini kwa hoja ya mtoa hoja na mlolongo huo wa majina inaonekana kuna wakati majina ya ukoo yatapotea manake itafika wakati hilo Mandiga likapotea na ikawa ni Yohana Julius Samson Paul Amos Mathias William Lucas ............. Mandiga linakufa kifo cha asili!!
 
Back
Top Bottom