Tuache siasa za kuhusisha jina la mtu na dini yake. Je, wasio na dini wasiteuliwe?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Kwa sisi wazee, Tangu utoto wangu sijawahi sikia mtu sehemu yeyote ya Tanzania iwe shule, ofisini au mitaani akiniuliza wewe dini gani? au wewe Kabila gani?. Mambo haya ya ujinga yanaonekana sasa tena kwenye kizazi cha sayansi na digital.

Kuna shida kubwa kwa vijana wetu badala ya kujenga fikra za Maendeleo kwa sayansi na teknolojia iliyopo duniani kwa wakati wao, Wanawaza jina la mtu na kuanza kulitafsiri ni dini gani au Kabila gani Katika kuongoza Taifa.

Mtu wangu wa karibu ninayeishi naye tu wa kuamka na kulala pamoja sikuwahi kumuuliza kabila lake wala dini yake Katika hatua za kumpenda, Kama kuyajua labda Yeye angelisema lakini sio mimi kuuliza ujinga wa dini au kabila.

Yawezekana wazazi wa kipindi chetu walitoa majina yenye maana ya tukio, kitu, ushujaa au hofu na wakati mwingine walipenda tabia ya mtoto fulani na kutoa jina.

Mfano utakutana na watu wanaitwa

Tumaini Ramadhani

Agustino Ramadhani

Mohamed Mawazo

Mohamed Joseph

Mwafilombe Musa Mwakalindile

Maeneo baadhi ya Mwanza na Shinyanga kuna watu Wanaitwa Hamza, Musa, Hussein na Jumanne lakini hawa watu sio waislamu kabisa bali ni majina yanayopendwa sana na baadhi ya watu wa Mwanza, Utawahukumu hawa watu kama waislamu kumbe ni wakristo.

Yapasa watu kutambua jina ni alama tu na alama unaweza kuibadili muda wowote ule.

Jina lako unaweza kulikana muda wowote na kupewa jina ulitakalo na haya yanafanyika kila siku mahakamani na serikalini kwa anayetaka.

Kuna watu Baba zao waliwakana na wanatumia majina za upande wa Mama zao, Wakati Baba na Mama walioana kwa mtazamo tofauti wa ufia dini.

Mfano, Ukoo wa Mama ni wakristo na ukoo wa Baba ni waislamu, Baba kamkana Mama na Mama kapata hasira badala ya kumwita mwanae jina la baba labda Mohamed Hussein Yeye anamwita jina la ukoo wake Mohamed Joseph Kalinga.

Je, utamuhukumu Mohamed kama mwislamu au mkristo?

Je, kwa wale wanaoamini mawazo ya dini hayapo na hivyo vitabu vyenu wa naona ni hadithi tu wasipewe uongozi?

Kuna maelfu ya watanzania hawana mambo ya udini, Kama kila mtanzania angekuwa na dini basi misikiti na makanisa isingetosha kabisa.

Kuna wakati huwa nashangaa vijana wanaongelea Simba na Yanga bila kufanya kazi masaa ishirini na nne na sasa wanaongelea udini masaa ishirini na nne.

Tambua ukiwa na kipaji na ukajituma utaonekana hata Marekani huko utaitwa na wala watu hawataangalia jina lako ni gumu kutamka au jepesi bali wataangalia uwezo ulio ndani yako.
 
Matajiri hawajadili dini na ukabila

Maskini ili kujipa faraja mara nyingi hujadili dini na ukabila

Walio bize na kutafuta hawazi udini na ukabila
 
Gussie,

Huenda picha hizo hapo chini umeshaziona mara nyingi sana hapa.

Nakuwekea ili uziangalie vizuri na ukae kitako ufikiri kama hali ilikuwa hivi wakati tunapigania uhuru wa Tanganyika kimetokea nini leo tuko hivi udugu na mapenzi yale yametoweka.

Nini sababu ya kutoweka udugu huu?

1677733298411.jpeg

Baraza la Wazee wa TANU 1957

1677733377842.jpeg

Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo Dodoma Train Station 1955/56
1677733549437.png

Kulia Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na kushoto mwanzo ni Bi. Tatu bint Mzee wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO 1955
1677733802566.jpeg

Kulia Ali Msham na Julius Nyerere aliyekaa nyuma ya meza 1955
Ndugu zangu,
Nini sababu ya kupotea kwa historia hii na mapenzi haya?

Kuna ujumbe gani tunapata katika picha hizi?
 
Sukuma gang wachache wanampaka matope mama kwa propaganda za kijinga,wala awana athari yoyote,kwanza vijeba hata rishe nzuri awana wamejaa yutiai na marelia kibao.
 
Udini na ukabila upo kwa wasiojiamini mara aseme anafanyiwa hivi mara hivi , kila mtu apambanie nafasi yake sio kujua huyu dini gani ili upate point.

Ebu fanya tathmini nyuzi za hivi karibu je ni wangapi wanalala udini?
 
Back
Top Bottom