Jina La Rais Jakaya M. Kikwete Kuongoza Marais 100 watakaomzika Nelson Mandela Leo

Baba akirudi kutoka kuzika nawasemea Tanesco wote na limuongo lao kwa kutukatia umeme wakati anakaribishwa hadi tumeshindwa kumuona alivyopendeza na tai yake na tabasamu lake.leeo..leeo..nawathemea thubilini aludi!
 
Baba akirudi kutoka kuzika nawasemea Tanesco wote na limuongo lao kwa kutukatia umeme wakati anakaribishwa hadi tumeshindwa kumuona alivyopendeza na tai yake na tabasamu lake.leeo..leeo..nawathemea thubilini aludi!

Baba yako harudi mpaka mwaka kesho, x-mass na mwaka mpya anasherehekea kwa kaka yake Obama,,mpaka aje utakuwa unakumbuka kumthema kweli
 
So what?Purely nonsense.
Johannesburg. Serikali ya Afrika Kusini, imetoa orodha ya majina ya wakuu wa nchi na Serikali 91 ambao wamethibitisha kushiriki katika shughuli zinazohusiana na safari ya mwisho ya Rais wa kwanza mzalendo wa taifa hilo, Nelson Mandela.

Jina la Rais Jakaya Kikwete ni la kwanza katika orodha hiyo inayowaweka viongozi hao katika makundi kutokana na mabara wanakotoka. Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili jana usiku tayari kuhudhuria Ibada ya Kitaifa ya Mandela ambayo imepangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa FNB (Soccer City).

Kabla ya Serikali kutoa orodha hiyo,Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane alisema wakuu wa nchi na Serikali 53 walikuwa wamethibitisha lakini jana mchana idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia 91. Kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka na kuzidi 100.

Msemaji wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Clayson Monyela aliwataja marais wengine kutoka Afrika kuwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC),Joseph Kabila, Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Mike Sall wa Senegal,Allessane Ouattara wa Cote d’Ivoire,Goodluck Jonathan wa Nigeria,Robert Mugabe wa Zimbabwe,Dennis Sassou-Nguesso wa Congo Brazaville, John Dramani wa Ghana na Ali Bongo wa Gabon.

Kutoka Amerika ya Kusini ni marais Nicolus Maduro Moros wa Venezuela na Dilma Rousseff wa Brazil ambaye ataambatana na marais wanne wastaafu wa nchini kwake.

Waziri Mkuu wa Bahamas, Perry Christie, Rais wa Guyana, Donad Ramotar, Rais wa Haiti, Michael Martelly na Rais wa Jamaica, Portia Miller, wakati kutoka Asia, kutakuwa na marais Pranab Mukherjee wa India na Hamid Karzai wa Afghanistan.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa,Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon Tayari Rais wa Marekani, Barrack Obama na mkewe Michelle walishathibitisha kushiriki, pia watangulizi wake, Bill Clinton,George W. Bush na Jimmy Carter wanatarajiwa kushiriki katika mazishi ya Mandela yatakayofanyika Qunu, Mthatha Jumapili.

Armando Guebuza wa Msumbiji, Abdelkader Bensalah wa Algeria,Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vicente, Rais wa Niger, IssoufouMahamdou, Kaimu Rais wa Agentina,Amado Boudou, Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key na Rais wa Bangladesh, Abdul Hamid MD Abdul.

Malkia Haakon wa Norway, Mfalme wa Philippe wa Ubelgiji, Rais wa Pakistan, Mamnoon Hussain, Rais wa Benin, Boni Yayi, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Rais wa Botswana,Seretse Ian Khama, Rais wa Ureno,Anibal Cavaco Silva na Mfalme wa Saudi Arabia, Muqrin bin Abdulaziz Al-Saud, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Rais wa Saharawi,Mohamed Abdelaziz, Waziri Mkuu wa Canada,Stephen Harper wa Chad, Idriss Deby Itno, Rais wa Serbia, Tomislav Nikolic,Makamu Rais wa China, Yuanchao,Rais wa Shelisheli, James Alix Michel,Rais wa Comores, Dr Ikiliou Dhoinine na Mfalme wa Hispania, Felipe de Borbon.

Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa,Makamu Rais wa Sudan, Hassan Salih,Rais wa Suriname, Desire Delano Bouterse, Rais wa Slovenia, Pahor,Rais wa Croatia, Josipovic Ivo, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kir Mayardit, Rais wa Cuba, Raul Castro Ruz, Rais waDjibouti, Ismail Omar Guelleh, WaziriMkuu wa Swaziland, Dr Sibusiso Dlamini, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Ato Hailemariam Dessalegn na Rais wa Equatorial Guinea, Obiang Mbasogo.

Rais wa Finland, Sauli Niinisto, Rais wa Tunisia, Mohamed Moncef Marzouki, Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago, Kamla Persad-Bissessar, Rais wa Gambia, Prof Alhaji Dr Yahya Jammeh, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa Ujerumani,Joachim Gauck, Rais wa Guyana,Donald Ramotar, Rais Michael Satta wa Zambia na Rais wa Guinea,Profesa Alpha Conde.

Mwanamuziki Bono, Mtangazaji,Oprah Winfrey na Mwanamitindo,Naomi Campbell na watoto kutoka Familia ya Malkia wa Uingereza,Prince Charles na Prince Harry.
 
headline ujumbe mtupu, habari hapa ni Mandela kuagwa na watu mashuhuri wengi, hii mambo ya sijui kuongoza ni kujipendekeza tu. Kuongoza mchezo!
 
Wana JF
Nina duku duku langu na kwa kuwa hapa kuna wengi tafadhali naombeni msaada wenu .Nimeumia sana leo katika kumuaga Madiba .Tanzania tulitumia ardhi yetu na pesa na misaada mingine kuhakikisha Mandela anatoka Jela na SA wanakuwa huru katika Nchi yao .JK jana alirudia maneno haya uwanjani , kwa maana hiyo Tanzania kama Taifa iwe TANU au CCM na sote tunahusika katika historia ambayo jana JK alitumia muda kulieleza Taifa .

JK akiingia nimemuona FNB lakini sikuweza kusikia anatajwa kama yupo kiwanjani tafadhali mwenye taarifa aniweke sawa .Nimeshangaa sana Nchi maa Uganda , DRC, Uganda wametajwa ila Rais wangu sikumsikia kabisa akitajwa kuwepo.Ulifika mahali pa kutaja Nchi ambazo zimetumia kila aina ya uwezo wao kuisaidia ANC , Tanzania haikutajwa kabisa ila Zimbabwe , Angola , Cuba walitajwa .Mwalimu Nyerere nina hakika wakati alifanya kazi kubwa mno .Je ni sahihi kwamba ANC hawakumbuki mambo ya wakimbizi wa Mazimbu Morogoro ? Ni kweli hatukuwa na mchango kwa ANC hadi wasiweze kuikumbuka Tanzania ?

Naomba kusahihishwa na kuambiwa pale ambapo sikuelewa .
 
Alitajwa , na neno la kiswahili lilitumika kumkaribisha KARIBU NDUGU YETU, sina uhaika na hilo neno la kiswahili, lakini alitajwa.
 
Alitambulishwa tu Rais wetu,baada ya hapo ziiiiiiiii,wakabaki kina Obama ndio wametawala coverage yote lol!
 
Alitajwa , na neno la kiswahili lilitumika kumkaribisha KARIBU NDUGU YETU, sina uhaika na hilo neno la kiswahili, lakini alitajwa.

Kuna uzi hapa ulianzishwa eti JK ataongoza viongozi wengine katika Mazishi ya kitaifa, ni kweli kaongoza?
 
Alitajwa , na neno la kiswahili lilitumika kumkaribisha KARIBU NDUGU YETU, sina uhaika na hilo neno la kiswahili, lakini alitajwa.

Uko sahihi kabisa yule mama (Zuma? ???!!!!!!) ndio alitangaza na hiyo swahili ilikuwapo!!!!
 
hata mimi nimesosoneka kwa kweli.nilikuwa chonjo sana kusikia jina la jk time ile maraisi waliohudhuria msiba wanatajwa.
 
Katajwa mara moja tu,then wakasahau.kama yupo,japo nafikiri hali hii haifuti yale aliyoongea jana uwanja wa UHURU kuhusu sisi na Afrika Kusini....Nimeshangaa hata nafasi ya kuongea....
 
Sina uhakika na unachokisema maana sikufuatilia. Lakini najua jambo moja tu katika maisha, ukiamua kutenda wema tenda na usingoje shukrani. Lakini pia hata kama hawajataja leo mbona siku zote huwa wana appriciate msaada wa Tanzania kwa wapigania uhuru wa SA. Hivyo kutokutajwa leo (Kama kweli hawajataja) kusikusononeshe. Nani alijenga lami na campus ya Mazimbu chuo kikuu SUA kama si wao. Je hiyo si ishara ya kuthamini mchango wa tanzania kwao? Ungana nao katika wakati huu wa majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.
 
Zambia,Zimbabwe na Tanzania zina mchango mkubwa sana kwa ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa na zina heshma kubwa huko achaneni na hizi cheap popularity za kuonekana kwenye tv,wanatuheshimu sana tu hasa wale ambao umri wao umesonga na wengi wanajeshi wanasema kiswahili utashangaa
 
Alitajwa , na neno la kiswahili lilitumika kumkaribisha KARIBU NDUGU YETU, sina uhaika na hilo neno la kiswahili, lakini alitajwa.

Upo sahihi ndugu,tena kamtaja akamkalibisha kwa kingereza na kiswahili..nitofauti walivyokaribishwa maraisi wa congo,nawengineo walikuwa wanatajwa tu majina ila kwa kikwete kamtaja akamkalibisha kwa lugha zote na shangwe uwanjani zikasikika,then mshehereshaji akaendelea.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Sina uhakika na unachokisema maana sikufuatilia. Lakini najua jambo moja tu katika maisha, ukiamua kutenda wema tenda na usingoje shukrani. Lakini pia hata kama hawajataja leo mbona siku zote huwa wana appriciate msaada wa Tanzania kwa wapigania uhuru wa SA. Hivyo kutokutajwa leo (Kama kweli hawajataja) kusikusononeshe. Nani alijenga lami na campus ya Mazimbu chuo kikuu SUA kama si wao. Je hiyo si ishara ya kuthamini mchango wa tanzania kwao? Ungana nao katika wakati huu wa majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Mkuu hakuna siku muhimu sana kama ilivyo kuwa leo kwa Tanzania kutajwa kama Nchi muhumu katika Free SA .Mali zetu , damu zetu , ardhi yetu ,hakika unapotaja Angola na Zimbabwe ukaacha Namibia na Tanzania hapo tunaumia wengi .Maana kuna siku Kabila anaweza kusahau kwamba hata askati wetu wamekufa ili kuisaidia Nchi yake kama alivyo sahau Museveni leo .That is my point .Nimeumia sana .Nilitegemea hata JK aseme kkitu kuhusiana na Mazimbu , Mandela kuja Tanzania mlore often kama alivyo lieleza Taifa jana kwenye sherehe za Uhuru .
 
Bora hawakumtaja angevimba kichwa awe anaenda huko kila siku....aje nyumbani tumem-miss
 
Hii habari ipo kwenye gazeti la mwananchi. Mleta hii topic ndio amepotosha kichwa cha habari. Huu ndio upuuzi wa JF. Hakuna standard. Huwezi kunukuu habari ya gazeti halafu ukaiukaaingiza huko maneno yako. Habari ni kama ilivo kwenye gazeti, kichwa cha habari ni tofauti. This is not acceptable

Kichwa cha habari cha Mwananchi ni: Jina la JK laongoza marais 100 watakaomzika Mandela. Kuna gazeti pia liliandika kuwa JK atazungumza kwa niaba ya SADC. Sijui hawa wahariri wanatoa wapi taarifa, wanafanya watanzania kuonekana tunajikweza sana duniani na baadaye kufadhaika bila sababu.
 
mara ya kwanza kusoma hiyo heading.. nilijua inatoka kwenye magazeti kama uwazi,wikienda etc, kuona ni mwananchi nikajua supu ishaingia nzi...... kweli mchawi mpe mwana alee
 
Zambia,Zimbabwe na Tanzania zina mchango mkubwa sana kwa ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa na zina heshma kubwa huko achaneni na hizi cheap popularity za kuonekana kwenye tv,wanatuheshimu sana tu hasa wale ambao umri wao umesonga na wengi wanajeshi wanasema kiswahili utashangaa

Mkuu ukiheshimiwa inakuwa wazi mahali kama leo .Inakuwaje uheshimiwe sirini lakini kwa uwazi hata wasitaje ?
 
Back
Top Bottom