Jina La Rais Jakaya M. Kikwete Kuongoza Marais 100 watakaomzika Nelson Mandela Leo


Aleyn

Aleyn

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Messages
11,639
Likes
15,638
Points
280
Aleyn

Aleyn

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2011
11,639 15,638 280
Johannesburg. Serikali ya Afrika Kusini, imetoa orodha ya majina ya wakuu wa nchi na Serikali 91 ambao wamethibitisha kushiriki katika shughuli zinazohusiana na safari ya mwisho ya Rais wa kwanza mzalendo wa taifa hilo, Nelson Mandela.

Jina la Rais Jakaya Kikwete ni la kwanza katika orodha hiyo inayowaweka viongozi hao katika makundi kutokana na mabara wanakotoka. Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili jana usiku tayari kuhudhuria Ibada ya Kitaifa ya Mandela ambayo imepangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa FNB (Soccer City).

Kabla ya Serikali kutoa orodha hiyo,Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane alisema wakuu wa nchi na Serikali 53 walikuwa wamethibitisha lakini jana mchana idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia 91. Kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka na kuzidi 100.

Msemaji wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Clayson Monyela aliwataja marais wengine kutoka Afrika kuwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC),Joseph Kabila, Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Mike Sall wa Senegal,Allessane Ouattara wa Cote d’Ivoire,Goodluck Jonathan wa Nigeria,Robert Mugabe wa Zimbabwe,Dennis Sassou-Nguesso wa Congo Brazaville, John Dramani wa Ghana na Ali Bongo wa Gabon.

Kutoka Amerika ya Kusini ni marais Nicolus Maduro Moros wa Venezuela na Dilma Rousseff wa Brazil ambaye ataambatana na marais wanne wastaafu wa nchini kwake.

Waziri Mkuu wa Bahamas, Perry Christie, Rais wa Guyana, Donad Ramotar, Rais wa Haiti, Michael Martelly na Rais wa Jamaica, Portia Miller, wakati kutoka Asia, kutakuwa na marais Pranab Mukherjee wa India na Hamid Karzai wa Afghanistan.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa,Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon Tayari Rais wa Marekani, Barrack Obama na mkewe Michelle walishathibitisha kushiriki, pia watangulizi wake, Bill Clinton,George W. Bush na Jimmy Carter wanatarajiwa kushiriki katika mazishi ya Mandela yatakayofanyika Qunu, Mthatha Jumapili.

Armando Guebuza wa Msumbiji, Abdelkader Bensalah wa Algeria,Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vicente, Rais wa Niger, IssoufouMahamdou, Kaimu Rais wa Agentina,Amado Boudou, Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key na Rais wa Bangladesh, Abdul Hamid MD Abdul.

Malkia Haakon wa Norway, Mfalme wa Philippe wa Ubelgiji, Rais wa Pakistan, Mamnoon Hussain, Rais wa Benin, Boni Yayi, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Rais wa Botswana,Seretse Ian Khama, Rais wa Ureno,Anibal Cavaco Silva na Mfalme wa Saudi Arabia, Muqrin bin Abdulaziz Al-Saud, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Rais wa Saharawi,Mohamed Abdelaziz, Waziri Mkuu wa Canada,Stephen Harper wa Chad, Idriss Deby Itno, Rais wa Serbia, Tomislav Nikolic,Makamu Rais wa China, Yuanchao,Rais wa Shelisheli, James Alix Michel,Rais wa Comores, Dr Ikiliou Dhoinine na Mfalme wa Hispania, Felipe de Borbon.

Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa,Makamu Rais wa Sudan, Hassan Salih,Rais wa Suriname, Desire Delano Bouterse, Rais wa Slovenia, Pahor,Rais wa Croatia, Josipovic Ivo, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kir Mayardit, Rais wa Cuba, Raul Castro Ruz, Rais waDjibouti, Ismail Omar Guelleh, WaziriMkuu wa Swaziland, Dr Sibusiso Dlamini, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Ato Hailemariam Dessalegn na Rais wa Equatorial Guinea, Obiang Mbasogo.

Rais wa Finland, Sauli Niinisto, Rais wa Tunisia, Mohamed Moncef Marzouki, Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago, Kamla Persad-Bissessar, Rais wa Gambia, Prof Alhaji Dr Yahya Jammeh, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa Ujerumani,Joachim Gauck, Rais wa Guyana,Donald Ramotar, Rais Michael Satta wa Zambia na Rais wa Guinea,Profesa Alpha Conde.

Mwanamuziki Bono, Mtangazaji,Oprah Winfrey na Mwanamitindo,Naomi Campbell na watoto kutoka Familia ya Malkia wa Uingereza,Prince Charles na Prince Harry.
 
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Messages
19,166
Likes
232
Points
160
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2011
19,166 232 160
Kwa hiyo jina likiwa la kwanza kwenye listi ndio kuongoza????!!!!!!

Watu wa protokali hebu tufafanulieni hapa!!!!!
 
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
12,446
Likes
5,218
Points
280
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
12,446 5,218 280
Kwa hiyo jina likiwa la kwanza kwenye listi ndio kuongoza????!!!!!!

Watu wa protokali hebu tufafanulieni hapa!!!!!
SA President Zuma ndiye atakaye ongoza mazishi na hii haiitaji hata uwe na elimu ya Mulugo kujua hii issue!

By the way President Obama na X Presidents Jimmy Carter;G W Bush;Bill Clinton wote watatua kwa pamoja Oliver Tambo International Airport na Airforce One bado kuna mtu anataka tuamini JK wetu atawaongoza hawa vingunge ugenini?
 
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined
Jul 29, 2010
Messages
11,192
Likes
433
Points
180
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined Jul 29, 2010
11,192 433 180
Hivi ni nani ana-update ziara za Kikwete nje ya nchi?
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
46,206
Likes
33,365
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
46,206 33,365 280
Wivu wa kike utakutoa meno.
Nyie vijana wa kichaga ni wa ajabu sana.
Nani mchaga?
Angalia heading na story yenyewe. Kwa nini unaanza matusi badala ya kujibu hoja? Ina maana kila anayeuliza swali ni mchaga? Kivipi? Kwanza ntake radhi kwa kuniita mchaga.
 
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Messages
19,166
Likes
232
Points
160
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2011
19,166 232 160
SA President Zuma ndiye atakaye ongoza mazishi na hii haiitaji hata uwe na elimu ya Mulugo kujua hii issue!
Elimu inaingiaje hapa; kama kuongoza in real sense itakuwa kiongozi wa kidini mkuu unless President Zuma is
 
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
12,446
Likes
5,218
Points
280
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
12,446 5,218 280
Hivi ni nani ana-update ziara za Kikwete nje ya nchi?
Kaisha vunja rekodi ya Rais Obasanjo;hii ni safari yake ya 361 dhidi ya 360 za Obasanjo(Nipo tayari kukosolewa nikikosea tarakimu)
 
habariyamujini

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Messages
3,095
Likes
44
Points
145
Age
39
habariyamujini

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined May 16, 2013
3,095 44 145
SA President Zuma ndiye atakaye ongoza mazishi na hii haiitaji hata uwe na elimu ya Mulugo kujua hii issue!

By the way President Obama na X Presidents Jimmy Carter;G W Bush;Bill Clinton wote watatua kwa pamoja Oliver Tambo National Airport na Airforce One bado kuna mtu anataka tuamini JK wetu atawaongoza hawa vingunge ugenini?
Ni Oliver Tambo International Airport na siyo National Airport!
 
Obama wa Bongo

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
5,138
Likes
3,618
Points
280
Obama wa Bongo

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
5,138 3,618 280
poor thread!
 
M

mchochoji

Member
Joined
Mar 15, 2013
Messages
20
Likes
1
Points
5
M

mchochoji

Member
Joined Mar 15, 2013
20 1 5
Kimbelembele wa kuzurura duniani,lazima ajiandikishe wa kwanza,Marais wengine wako bize kushughurikia masuala yao ya wananchi na kitaifa ndio maana walichelewa kujiandikisha..haina connection na kuongoza mazishi
 
omujubi

omujubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Messages
4,143
Likes
84
Points
145
omujubi

omujubi

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2011
4,143 84 145
Mhhhh! Najua kuna wanaotumia msiba huu kutafuta sifa baada ya kuona walizonazo haziwatoshi, ngoja tusubiri maana haya mambi yatakuwa 'live' na hapo tutajua ni nani 'ataiongoza' dunia kumuaga Mzee Mandela.
 

Forum statistics

Threads 1,273,231
Members 490,323
Posts 30,474,446