Jina la Dar es salaam ni CHAFU, DHAMBI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jina la Dar es salaam ni CHAFU, DHAMBI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pharaoh, Apr 30, 2011.

 1. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watanzania wenzangu wenye mawazo mapya na wasiokumbatia kwa itikadi, kwa nini huu mji uitwe jina la kutukuza Sultani wa Zanzibar aliyekuwa anavusha watumwa kutoka kijiji cha MZIZIMA, na kwa jinsi biashara ilivyokuwa laini akaamua kuiita BANDARI YA SALAMA, kwani wazaramo hawajampa upinzani wowote kuichukua watumwa.
  nchi ngapi Duniani zimebadili majina ya miji mikuu? au kwa sababu waliooongoza mji mkuu huu ni wazee wajinga wasiofikiri chochote bali ukubwa tu watukuzwe?
  au ndio LAANA ya mwafrika inaendelea? nawaombeni kwa Heshima ya Babu zetu walioteswa na kufa, Tubadilishe jina hili la Adui aliyewatesa Babu zetu.

  najua mtauliza, ndio, napendekeza turudishe jina lake la kale au tuchague haya:
  1 Mzizima, jina lake la mwanzo kabla ya uvamizi wa waarabu.
  2 Tanganyika, ili jina kubwa hili lisife, aminini Duniani linajulikana kuliko Tanzania.
  3 Bongo, ni jina ambao linamaanisha ubongo wa akili, ni zuri
  4 Tanzania, ili endapo muungano utavunjika hili jina lisipotee lishajulikana duniani.
  5 Zaramo, wenyeji wa asili.
  Naomba mashujaa wa Taifa wachangie.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri, naunga mkono hoja.
  Mji huu naona bora uitwe Mzizima kama hapo awali ulivyojulikana. Pia sio mbaya kama ukaitwa Azania
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naam, nilisahau, jina hilo nalo poa sana, ni jina la eneo lote hili katika enzi Issa ibn Marium au Yesu Kristo.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri but what is in the name? Vipi na wewe majina yako yote yana asili yako?
   
 5. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndo nyerere akaweka dodoma kuwa mji mkuu kwa akili zake mbovu kama zako pumbavu
   
 6. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sikuelewi ndugu, kwa hiyo hamna mabadiliko? au wewe unasemaje?
   
 7. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na. Tatu umechemka. Huwezi kusema Bongo wakati watanzania hawastahili. Mfano: 1. Wasomi wengi hufikiria magari tu wala sio namna ya kujenga mtazamo wa kutatua foleni kwanza. 2. Wanapenda sifa zilizojaa mipango dhaifu km kumiliki simu kali wakati huna pa kuishi. 3. Wanapuuzia umuhimu wa kuwa watafiti kwanza (uvivu). Ubongo wetu uko wapi? It is said that the level of social dev. is determined by level of knowledge of people of that society. Hadi hapo Sisi Wabongo na huu umasikini? Acha uvivu, fikiria kabla ya kujenga hoja.
   
 8. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  haya lete maoni yako, ndio kweli waafrika tuko hivi haswa kama unavyosema, lakini tufurukute wengine wachache kutafuta makosa yetu au tujichimbie kaburi? mi naona tusichoke kumbuka Rome was not build in a day!
   
 9. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mawazo yangu ni kuwa jina la dar-es-salaam liendelee kutumika na dsm uwe mji mkuu wa tz kama hamuutaki basi tupeni wenyewe wazenj huo dsm ni mji wetu mbona. Nyie kwenu ni arusha na iringa banaa.
   
 10. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  toa zaramo
   
 11. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye RED siamini kama ni sahihi vinginevyo tuamini hata wewe kuwa na mawazo tofauti na wazee hao basi wewe ni kijana mjinga unayedharau kila kitu cha wazee wako na kuwaza kubadiri kila kitu
   
 12. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza tuanze na kitu kinachoitwa "one's own proper place" yaani wasomi waipende nchi yao wala sio liwalo na liwe potelea mbali wanakimbia, hasa viongozi wapatikane watakaoleta kitu nachoweza kuita 'Trigger Theory' which can tap the potential energy of human labour ndipo tutafanikiwa kuitwa Wabongo.
   
 13. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sawa Kitumbo, tusifunge mlango na kupigana, mimi narudisha maneno mabaya juu ya wazee walioongoza jiji mpaka sasa, na nina heshima kubwa kwao kwani ni watangulizi, lakini sasa tukubali mabadiliko na mawazo mapya ya kuboresha nchi yetu, unajua Rome was not build in one day? sawa shekhe wangu Kitumbo? naomba radhi kwa maneno ya mwanzo.
   
 14. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  unakuwa vigumu hata kwa wanaotangaza nchi nje, kwani ukitaja jina tu la mji, watu wanajiuliza kwani ni arabuni? mbona jina la kiarabu? si nchi yenu iko africa? kidogo inakuwa aibu.
   
 15. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hoja iendelee mkuu
   
 16. S

  Sauti ya Uhuru Member

  #16
  May 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Miaka 1960s na 1970s wengi walitaka kubadilisha jina Dar es Salaam kuwa MZIZIMA. Dar es Salaam ilikuwa jina la Sultan Majid kutoka Zanzibar miaka 1860s, na Mzizima ilikuwa jina la Mashomvi na Zaramo kabla ya hii. Sifikiri jina la 'Dar es Salaam' ni chafu au dhambi -- Shomvi na Zaramo walikuwa na chafu na dhambi zao kabla ya Sultani!
   
 17. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Baba yenu nyerere alishawapelekeni dodoma sasa munaitakia nini Dar es salaam, DSM sio kwenu ndio maana hukudhamini kama ndio hivyo kila cha asili kirudishwe kwenye asili yake na nendeni kwanza mukabomoe yale makanisa yenu muliyoyajenga baada ya kuvunja misiskiti
   
 18. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sasa mbona ALEXANDRIA ipo Misri na jina lakizungu fikiri kabla hujaongea na kuandika
   
 19. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndio maana walibadilisha Dar es salaam Airport ili waweke jina la kikafiri, kama baba yenu alichemka mutaweza nyie bwana badilisheni majina yenu muliopewa na wazazi wenu ya kizungu kwanza
   
 20. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Welcome to The City of Mzizima - That's Hot
   
Loading...