Hivi ni kweli kijana ni taifa la kesho?

clion dismas

Senior Member
Aug 6, 2017
185
170
MUNGU HASEMI IVI, JE NANI ASEMA “KIJANA NI TAIFA LA KESHO”?

Habari zenu wapendwa, poleni na majukumu ya hapa na pale, naamini Mungu yu mwema kila leo. Naomba mnisaidie kuelewa kwa upana nadharia hii, "KIJANA NI TAIFA LA KESHO."
Tangu nikiwa mtoto mdogo hadi leo kijana nimekutana na msemo juu ya kijana( yumkini ni sera) usemao “KIJANA NI TAIFA LA KESHO”. Nimejiuliza maswali mengi juu ya kauli/msemo/sera hii, kama vile:-

1.KESHO NI SIKU GANI? KESHO ITAFIKA LINI?

2.KWANINI MSEMO HUU? NA KAMA KIJANA NI TAIFA LA KESHO, JE, TAIFA LA LEO NI NANI?

3.JE, MSEMO HUU UNAENDANA NA MAANDIKO MATAKATIFU? AU NI FUNDISHO LINALO ELEA ANGANI?

4.KWELI MSEMO HUU HAOUTOKUWA NA LENGO LA KUWATENGA VIJANA KATIKA SHUGHULI NYINGI NYETI KAMA VILE ZA KUTOA MAAMUZI MAZITO YENYE MASLAHI MAPANA KATIKA KADA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA?

Lakini sikuishia hapo, nimejaribu kuangalia hali ya vijana kiujumla na nimebaini yafuatayo:-

Kijana kiumri yuko kati ya miaka 15-35.( ni milioni 15.6 hapa nchini), ambao hawa ni sawa na 66.4% ya nguvu zalishi nchini.

Kijana ni mtu mwenye nguvu nyingi na ndiye mzalishaji mkuu kiuchumi

Vijana tegemezi, chini ya miaka 18 ni Zaidi ya asilimia 50% ya wakaazi wote wa taifa hili.

Vijana wasio na ajira(miaka 15-24) ni sawa na asilimia 13.4% ya nguvu kazi yote

Vijana wa kike wakiwa ni asilimia 14.3 na kiume 12.3 ya wasio na ajira

Vijana chini ya miaka 15 ni asilimia 47

Kiujumla, watu wasio na kazi, vijana ni 53.3% ya watu hao wote

Katika taifa lenye wakazi Zaidi ya milioni 50, Zaidi ya asilimia 50 ya wakazi hao ni vijana.

BADO SWALI LANGU LILIKUA PALEPALE, KWANINI VIJANA WAITWE TAIFA LA KESHO? NI KWA SABABU YA TAKWIMU HIZI ZA VIJANA NA AJIRA? IDADI YAO AU NINI?

Nimefatilia kwa umakini katika hali ya vijana kuajiriwa, mwaka 2014, nimegundua sekta rasmi ziliajiri vijana 230,515 ambapo nafasi 174,149 zilibaki wazi bila watu kuajiriwa kwasababu vijana hawakuwa na sifa.

JE, HIZI NI SABABU ZA VIJANA KUITWA TAIFA LA KESHO?

Sikuishia hapo, nikaamua kuangalia hali ya umri wa kupokezana vijiti katika kazi rasmi, nikafahamu ya kwamba:-

Umri wa kustaafu wa hiari ni miaka 55

Umri wa kustaafu wa lazima ni miaka 60 lakini pia watu wenye sifa maalum hawafungwi na kigezo hiki.

Nikawaza, je, wanaopitisha umri huu wa kustaafu ni vijana? Au hawa wa taifa la leo? Walioshika vijiti?

Bado, sikupata jibu

Nikaangalia nafasi walizonazo vijana zenye mamlaka, je wanafanya kazi za kutukuka? Sikupata taarifa kiujumla, lakini, pale mkoani mzizima kuna vijana, wenye dhamana, nimeona, wanafanya kazi pengine ukilinganisha na wazee wetu, kiufanisi wako mbali sana.

Nikaangalia maadili ya taifa kiujumla, nimebaini, vijana kwa upana, kwa sababu ni wengi sana nikaona maadili yao yanasuasua. Lakini hili ndilo labda vijana walifanywa kuwa taifa la kesho? Nikaoji, mchicha unaweza kuzaa Sukuma wiki? Sikupata jibu, nikabaini mmomonyoko wa maadili unachangiwa na walio wakuza au walio walea, yumkini, wao ndio taifa la leo.

Sikuishia hapo, nikaangalia sifa za kugombea nyadhifa kubwa sana, nikabaini kwamba, VIJANA wametupwa nje katika jambo hili pia. Nimejiuliza, sikupata jibu, nikawaza, jee hii sera kipindi inatolewa, ililenga kitu gani asa? Ilinuia kufanya nini? Na aliyeitoa alikua na mtazamo gani?

Nikaangalia athari ya msemo huu kwa vijana wenyewe, je, wanachukuliaje kuitwa taifa la kesho?

Kiupana katika utawala, linawaathiri vijana, kwa sababu watu wa taifa la leo wanaung`ang`ania mzinga uliojaa asali, na haifahamiki asali itaisha lini katika masega. Yumkini, asali ikikauka, vijana hawatongoja kuwezeshwa bali kutakuwa na njia sahihi za kuufuata mzinga wao wenyewe. Vijana wamekua kama nyuki, wanaruka huku na huko, wanafanya kazi ya kujenga masega, wanaruka misituni katika kila ua lililo juu ya ardhi na kutafuta majimaji ambayo ni malighafi ya kutengenezea asali lakini, kwa upana wake, bado hawaijua ladha ya asali ilivyo, hawawezi kutofautisha asali ya nyuki wakubwa na wadogo.

BADO SIKURIDHIKA, NIKAAMUA KUFUATA UKWELI USIO NA HILA YOYOTE, NIKAMUULIZA MUNGU, VIJANA NI TAIFA LA KESHO ?

MAJIBU NIKAPEWA HAYA:-

1. YOSIA ALIANZA KUTAWALA AKIWA NA MIAKA 8 TUU.( 2 wafalme 22)

Mungu akasema, hakika, HAYUKO NA HATOKUJA KUWEKO MFALME KAMA YOSIA KATIKA DUNIA HII. Aliifuata sharia yote na alimpendeza MUNGU.

YUSUFU ALIKUA WAZIRI MKUU AKIWA NA MIAKA 30 TUU.( mwanzo 41:46)

Nikazidi kupata somo, yusufu, mwana wa YAKOBO, alikua kijana, kijana aliyejazwa na roho wa MUNGU, kijana aliyeongoza taifa la misri kwa zamu yake.

2. BIKRA ESTA, BINTI MALKIA-MWOKOZI WA WAYAHUDI.( esta 2:2)

Wengi tunamfahamu malkia esta na kisa cha ukombozi wa wayahudi katika kipindi chake. Alikua binti yatima aliyelelewa na mjomba wake na alichukuliwa utumwani. Biblia yasema, ..ALIKUA NI MZURI NA WAKUPENDEKA..ESTA 2:7, PIA BIBLIA YASEMA, MUDA ANAKUA MALKIA, ALIKUA NI BINTI,… leteni mabinti bikra, wazuri… esta 2:2. Nikazidi kuelewa, mungu na vijana.

3. DANIELI,SHADRACK, MESHACK NA ABEDNEGO.( Danieli 1:14)

Ukisoma kitabu cha danieli utapata hadithi tamu ambayo yaelezea maisha na historia ya dunia hii hadi kuja YESU kwa mara ya 2. Hawa wana wa yuda wakiwa utumwani walifanywa kuwa wakuu katika nchi ya mfalme nebukadneza. Nikazidi kuunganisha visa hivi na nadharia ya kijana kuwa taifa la kesho.

4. KIJANA MUSA, kutoka 2

Musa alitumiwa na Mungu kuwatoa wana wa Israeli katika nchi ya utumwa ya Misri. Kwakweli, tangu kuzaliwa kwake, mafundisho aliyopewa na mama yake na hadi anaanza kazi ya kuwakomboa wa misri alikua ni kijana. Nilijaribu kujiuliza, hivi muda wote huu, mungu hakuona wazee wenye hekima kuwapa kazi hii takatifu ya kiutawala? Nikazidi kuelewa, MUNGU ameweka hazina kubwa ya utawala kwa vijana.

5. Kijana Daudi, Mwana wa Yese na GOLIATI( 1samuel 17:1-)

Kijana mdogo kabisa, mchunga kondoo, asiye na mafunzo ya kivita, asiye na ujuzi wa utawala bali kuwaongoza mifugo wake kwenda malishoni na kuwarudisha nyumbani anamaliza aibu ya taifa la ISRAELI lililodumu kwa Zaidi ya miaka 40 kwa kumuua jemedari wa vita, jitu kubwa la kifilisi, mnyama wa kutisha, GOLIATI.

Kipindi hiki Sauli akiwa mtawala, wafilisti walikuja kufanya vita na taifa la Israeli na walizoea kulishinda taifa hili katika vita, lakini, katika mji wa YESE, kupitia kwa mchunga kondoo.

GOLIATI AKASEMA, “SI MMESHUKA KUPIGANA NAMI…JICHAGULIENI MTU AJE APIGANE NAMI… AKINISHINDA NA KUNIUA MTATUFANYA WATUMWA, NAMI NIKIMSHINDA NA KUMUUA, MTAKUA WATUMWA WETU…( 8-10)”. SAULI NA JESHI LAKE WOTE WALITETEMEKA NA KUOGOPA SANA JUU YA MANENO YA GOLIATI NA KUNUIA KURUDI NYUMA.

Mfalme sauli alisikia maneno ya DAUDI kijana mdogo atakaye kwenda kupigana na mfilisti kwa maana sauli na majeshi yake yote walikwisha ogopa lile jitu na vita ile. Daudi akasema:- “usizimie moyo kwa ajili ya mfilisti huyu, mimi nitakwenda kupigana naye…”. SAULI hakumuelewa kabisa daudi na akamjibu, “huwezi wewe kwenda kupigana na mfilisti huyu, maana wewe hu kijana tu na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake”.

Hata leo ndivyo vijana wanavyodharauliwa na watu wengi, wakidhihakiwa na maneno ya namna hii, hebu tuone, Daudi alifanya nini.

DAUDI AKAMJIBU SAULI, “mtumishi wako nilikua nikichunga kondoo za baba…alipokuja simba au dubu akamkamata kondoo katika kundi, mimi hutoka na kumfuata na kumpiga na kumuua…, mtumishi wako nilimuua simba na dudu pia, na huyu mfilisti…kwa sababu ameyatukana majeshi ya MUNGU naye nitamuua…”(haya ya 32)

MFALME SAULI AKAMWAMBIA DAUDI, “ENENDA, BWANA ATAKUA PAMOJA NAWE”.( aya ya 37).

Nami kijana nakwambia, si kesho, si kesho kutwa wala si mwakani, ni sasa, kwa mamlaka ya neon la MUNGU, “enenda, MUNGU ATAKUA NAWE.” Wewe si wa kesho kijana wewe ni wa leo, tena si leo, wewe ni wa sasa, ENENDA. USIOGOPE, MUNGU YU NAWE.

SAULI AKAMVISHA NGUO ZA KIVITA DAUDI, DAUDI AKASEMA LA, SINA UZOEFU NA MAVAZI HAYA, AKAYAVUA. AKACHUKUA MAWE YAKE MALAINI 5 NA FIMBO YAKE YA KUCHUNGIA KONDOO NA KOMBEO, TAYARI KUKUTANA NA MFILISTI GOLIATI.

GOLIATI ALIPOONA YULE KIJANA MDOGO SANA, ALIMDHARAU NA KUCHEKA, GOLIATI AKAMWAMBIA DAUDI, “JE MIMI NI MBWA? HATA UNIJILIE NA FIMBO?”

Hata leo, twaonekana dhaifu katika hali ya nje, laiti goliati angekuwa na macho ya kiroho akaona ndani ya fimbo ile kuna kitu gani…. Angetubu na kuomba udugu.

Ni mara ngapi umekatishwa tamaa na adui aliye mbele yako kijana? Ukimtegemea mungu, yeye ni mkubwa kuliko adui huyo.

Daudi akafungua kinywa chake akasema, “wewe wanijilia na upanga na fumo na mkuki….lakini mimi naja kwako na JINA LA BWANA MUNGU…”

1SAMUELI 17:49

DAUDI AKATIA MKONO WAKE MFUKONI, AKATWAA JIWE MOJA, AKALIWEKA KWENYE KOMBEO, AKAMPIGA MFILISTI KATIKA PAJI LA USO, AKAANGUKA CHINI KIFUDIFUDI….50, AKAMUUA, INGAWAJE HAKUWA NA UPANGA MKONONI MWAKE.”

Kijana, unaponuia kwenda kokote pale, enenda kwa jina la bwana wa majeshi, MUNGU. AIJALISHI NI GOLIATI WA AINA GANI LEO UNAKUMBANA NAYE, RUSHWA, UTAWALA MBOVU, UOGA, KUTOJIAMINI, WIZI, DEMOKRASIA NA MENGINE MENGI YAMCHUKIZAYO MUNGU, UKIMTANGULIZA YEYE MUNGU, ATAKUSHINDIA, HILI NI AKIKA. ENENDA.

6. JESUS CHRIST/YESU KRISTO AKIWA NA MIAKA 27.( LUKA 3:30)

Naamini hapa duniani hakuna kiumbe mashuhuri na cha ajabu kuliko jina hili. Aliwekwa wakfu katika mwaka wa 27, tangu azaliwe kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu. Tangu utotoni alijawa hekima na maadili ya kutosha na hakika, wazee wenye busara walikili ilo.

MUNGU ALILETA UKOMBOZI KUPITIA KWA VIJANA, NA NI KWANINI SASA ULIMWENGU HUU UNASEMA VIJANA TAIFA LAKESHO? WAKATI MUNGU ANASEMA MSIISUMBUKIE KESHO NA MAMBO YAJAYO? MUNGU ASEMA, YEYE NDIYE ATOA KILA KITU KWA MTU AMTAKAYE, MWENYE HEKIMA, MUNGU NDIYE KAMKIRIMIA, MWENYE BUSARA NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU. MUNGU ACHAGUI AMPE NANI, AANGALII RIKA WALA RANGI. NI KWA NINI TAIFA HALIWATUMII VIJANA MAENEO NYETI KAMA MUNGU AFANYAVYO?

HAKIKA, MUNGU ASEMA, VIJANA NI JESHI KUBWA LA LEO. HAKUNA HABARI JUU YA TAIFA LA KESHO.

ILA KIJANA, MUNGU ATAKUTUMIA TUU, ENDAPO UTAISHIKA SHERIA NA AMRI YAKE PAMOJA NA KUITII.

NINAAMINI BILA SHAKA LOLOTE, KAMA JINSI MUNGU AISHIVYO, SIKU YAJA, MKUU WA TAIFA ATAKUA KIJANA. MTASHUHUDIA MAMBO MAKUU NA YAKUMPENDEZA MUNGU HAMJAWAHI KUONA. NAAMINI KATIKA NGUVU AMBAYO MUNGU AMEIWEKA KWA VIJANA, HEKIMA, BUSARA NA ROHO WAKE.

MWISHO KABISA, SHUKRANI ZIMUENDEE MKUU WA NCHI KWA KUAMUA KUWATUMIA VIJANA NA KUONESHA UWEZO WA VIJANA KWA DUNIA YOTE. ENDELEA IVYO IVYO NA MUNGU AKUFUNULIE MAMBO MAKUU ZAIDI.

“KIJANA NI TAIFA LA LEO”- namuamini MUNGU kuliko yeyote yule.

UZOEFU BINAFSI

NAOMBA NISEME KIDOGO JUU YA UZOEFU WANGU KAMA KIJANA, JUU YA MAMBO NINAYOYAPITIA NA JINSI MUNGU ANAVYOFANYA KAZI:-

KUHUSU UJENZI WA CHUO KIKUU MKOANI MARA

Naliandika barua( nimeiambatanisha hapa) kwa mkuu wa mkoa kwa ajili ya pendekezo langu katika mkoa. Barua niliikopi kwenye ofisi kubwa 3 nchini. Na ofisi moja kubwa iliiona barua na ilihoji mkoa juu ya barua yangu, je, wamenikubalia au wamenikatalia? Na kama wamefanya ivyo, wametumia sababu zipi? Hawakuwa na majibu kama mkoa. Waliamua kuniita kwa barua( ambatanishwa pia), nikaongea na ofisi ya mkuu wa mkoa. Nikaambiwa yote, name nikawaambia yote, nikaambiwa niandae mpango kazi jinsi itakavyofanyika, name nikauandaa na kuutuma.

Kama zama za daudi, bado kuna watu walio katika mfumo wanasema jambo hili haliwezekani na hakika wamelipinga kwa hali ya juu. Lakini sijawahi kukata tamaa, mwenye dhamana ya elimu katika eneo lile mkoani, alinipa ruhusa nizunguke mkoa mzima kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi juu ya jambo hili, kwa sababu mkoa una wilaya nyingi naliomba nishikwe mkono na mfuko wa elimu, lakini walidai hawana chochote kama hakiba. Sijachoka, kama kijana, najipanga,lazima chuo kikuu kijengwe eneo hilo.

Yapo mengi sana, lakini naomba niseme hilo kwa leo.

Mimi siyo mwanachama wa chama chochote.

Mimi sipo hapa kuwanadi wala kugombana na watu fulani

Mimi nipo hapa kuwaamsha vijana.

Vijana, MUNGU AWAAMBIA “enendeni”.

REJEA

BIBLIA- UNION VERSION

DATA FOR LOCAL IMPACT INNOVATION CHALLENGE

NATIONAL BUREAU OF STATISTICS

PMO-LYED

REPOA

ILO-TZ

WORLD BANK

PEPFAR

Clion o dismas
 
Attachments

  • RC MARA.pdf
    388.4 KB · Views: 33
  • OMBI LA KUFUNGUA CHUO KIKUU MKOANI MARA0001.pdf
    30.4 KB · Views: 24

Mkuu yote haya tusome sisi tu au ?
 
Mimi nadhani wahenga walimaanisha ya kwamba kijana kuwa ni taifa la kesho ni ile huyo kijana atakuwa mzee hvyo wazee kama wazee walitazamiwa kuwa na Busara na hekima nyingi hata ziwe na faida kwa taifa kama taifa katika nyanja mbalimbali ni mtazamo tu wakuu
 
Back
Top Bottom