Fahamu kuhusu shambulio la kigaidi Afrika Mashariki, Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998

Dec 23, 2016
31
69
Njia iliyotumika:
Malori yenye baruti vilipushi yalitumika kutekeleza mashambulio mbele ya balozi.

Idadi ya waathirika:
Zaidi ya watu 300 (Tanzania na Kenya) waliuwawa huku 4000 wakijeruhiwa.

Watekelezaji:
Azam (alie jitoa muhanga na kujilipua), Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali (mshambuliaji), Fazul Abdullah Mohammed (msuka mipango), Abdullah Ahmed Abdullah (Kamanda wa operesheni).

Al-Qaeda:
Intel CIA yabaini kua mtandao wa kundi la kigaidi al-Qaeda ulihusika ukishirikiana na kundi lingine kutoka Misri.

Osama Bin Laden:
Alitambulika rasmi kama mtu hatari katika uso wadunia hali iliyopelekea shirika la upelelezi la marekani FBI, kumuweka katika kitabu chake cha wahalifu 10 wakidunia waliohitajika zaidi.

Operation Infinite Reach:
Bill Clinton (1993-2001) aruhusu marekani kujibu mashambulizi kwakutupa makombora na kulipua ngome ya Al-Qaeda huko Khost Afghanistan na kiwanda kikubwa Khartoum Sudan ambacho mmiliki wake alisadikika kua na uhusiano na kumsaidia kifedha Bin Laden.

UN Security Council Resolution 1189:

Umoja wa mataifa kupitia baraza lake la usalama ulipitisha makubaliano (unanimously) yakulaani vikali shambulio la kigaidi Tanzania na Kenya.

Na;
Mfaume Hassani Hamadi.
Mwanafunzi Shahada ya Usimamizi wa Sheria UDSM.
Young Intelligence and Security Analyst.
.

Agosti 7, 1998 balozi mbili za marekani nchi za Afrika Mashariki, Tanzania na Kenya zililipuliwa kwa wakati mmoja katika shambulio lakigaidi lililo ratibiwa na kundi lakigaidi kutoka Misri ambalo ni katika mtandao wa Al Qaeda chini ya Osama Bin Laden.

Zaidi ya watu 213 walipoteza maisha, ikiwemo wafanyakazi na raia wa kawaida. Watu 44 walikua ni wafanyakazi na raia wamarekani (raia 12 wa marekani, na wafanyakazi 32)

Katika shambulio la Nairobi inakadiriwa kua raia 4000 walidhurika na shambulio.
Baada ya shambulio marekani ilikuja kutoa msaada wa kuokoa na pia kuwarudisha nyumbani raia wake walionusurika.

MODUS OPERANDI

Njia iliyotumika kufanikisha mashambulizi ilikua ni vilipushi vya baruti.
Malori aina ya yaliyokua yamejaa baruti yalitumika kusogeza vilipushi karibu na majengo ya balozi.
Jambo ambalo ni baya na lakuhuzunisha kabisa ni kwamba miongoni mwa magaidi waliotumika kutekeleza mashambulio haya walikua ni raia wa Tanzania na kenya, wakishirikiana na raia wengine kutoka nchi ya Somalia na nchi za uarabuni.

Dar es Salaam Tanzania

Ilikua ni siku ya ijumaa tarehe 7 Agosti, 1998, ambapo gari aina ya lori lililokua limebeba vilipushi baruti, lilijaribu kuingia katika eneo la ubalozi lakini likazuiliwa na walinzi getini.

Dereva baada yakuona hivi aliamua kulipusha mabomu yake palepale alipokua. Ilikua mbali kidogo na jengo hali iliyosaidia kupunguza madhara.

Bahati nzuri, shambulio la Dar es salaam halikuleta madhara makubwa ukilinganisha na kule Nairobi. Hii ni kutokana na sababu kua ubaluzi haukua katikati ya mji, na hapakua na makazi ya watu karibu na balozi. Balozi ilikua kando ya mtaa wa Bagamoyo. Watu 11 walikufa na Zaidi ya 80 walijeruhiwa.

Nairobi Kenya

Shambulio la Kenya lilikua ni kubwa Zaidi na lilileta maafa makubwa ukilinganisha na la Dar es Salaam. Hii ni kutokana na location ya ubalozi uliokua Kenya.

Huku mbinu iliyotumika ikiwa ni ileile ya lori, majira ya saa nne na nusu asubuhi watu wawili walikua ndani ya lori lililokua likisogea karibu na ubalozi wa marekani njia panda ya barabara za Moi na Haile Selassie karibu na kituo cha reli. Lilikua Lori dogo lililobeba kilogramu 700 za baruti.

Jitihada zakuingia katika gereji iliyokua chini ya balozi zilishindikana kwa sababu yakukataliwa na mlinzi bwana Benson Okuku Bwaku.

Ndipo gaidi Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali alipoamua kutupa kombora lamkono ambalo lilimkosa mlinzi na kumpa nafasi ya kukimbia.

Gaidi mmoja (Al-Owhali) alikimbia na mwingine alieitwa Azzam alianza kufyatua risasi hovyo na baadae akajitoa muhanga kwa kujilipua ndani ya lori. Mlipuko ulikua mkubwa kiasi chakusikika umbali wa kilometa 16. Ndani ya balozi walikua watu 44.

Mbali na kwamba jengo la ubalozi halikuanguka lote kutokana na uimara wake, vifo vingi vilitokana na mshtuko ulioingia ndani kupitia madirisha na kuangusha baadhi ya kuta za ndani.

Jengo dogo jirani la ufundi lilibomolewa na vifo vingi vilitokea katika jengo hili lililokua anguka kabisa. Raia wengi walikufa.

Hata baadhi ya magari na watu walikua barabarani waliathiriwa na mlipuko wa bomu hali iliyosababisha magari mengine kuchomwa kabisa na abiria wake waliokua ndani.

Operation Infinite Reach.

Baada ya tukio la Agosti 7, marekani haikuridhika kuwaacha magaidi salama na ilitaka kuwapa donda watakalokua wakiliponya kama walivyofanyiwa raia wa marekani na balozi zake.

Mapema ya Agosti 20, 1998, siku ya 13 baada ya shambulio Afrika mashariki, Makombora ya marekani yalielekea huko Sudan kwa Al bashir (raisi aliepinduliwa siku kadhaa zilizopita) na Afghanistan, katika operesheni iliyopewa jina la “Operation Infinite Reach”

Hii ilikua ni operesheni maalumu iliyolenga kumuua kiongozi wa Al-Qaeda Osama bin Laden na washirika wake kama Ayman Al-Zawahiri waliosadikika kuwepo katika kambi ya kundi hilo, katika mji wa Khost Afghanistan.

Operesheni hii pia ililenga kusambaratisha kiwanda cha madawa “Al-Shifa Plant” kilichokua Sudan ambacho kilisadikika kumtengenezea Osama Bin Laden kemikali aina ya “VX nerve” iliyotumika kutengeneza silaha zakikemikali na vilipushi.

Mmiliki wa kiwanda cha Al-Shifa alisemekana kua na ushirikiano na Bin Laden, kwa kumpa msaada wa kifedha.

Sampuli ya udongo uliochukuliwa katika kiwanda hicho ulionekana kua na kemikali ambayo ilitumika katika shambulizi la Afrika Mashariki.
Makombora yalisambaratisha kiwanda na kuua raia 11 wa Sudan.

Raisi wa marekani kwa wakati huo Bill Clinton aliuambia uma na dunia kua marekani isingeweza kuvumilia na ingefanya vyovyote iwezekanavyo kuhakikisha wahusika wa matukio ya kigaidi dhidi ya marekani na dunia kwa ujumla wanakamatwa na kupeleka mbele ya sheria.

Bin Laden Akoswa kuuwawa.

Shabaha kubwa ya marekani ilikua ni kumuua kiongozi wa Al-Qaeda, kitu ambacho hakikufanikiwa kutokana na ukweli kwamba intel iliyotolewa marekani kua Bin Laden alikua katika kambi huko Afghanistan haikua yakweli au kaikufika wakati sahihi.

Mbali na kumkosa Bin Laden, pia hakuuwawa gaidi mwingne yeyote zaidi raia ndio waliokua wameuwawa. Misheni ilienda bumbum.

Marekani Yakosolewa.

Baada ya kusambaratisha kiwanda cha Al-Shifa Plant, marekani ilikosolewa vikali na baadhi ya wasomi na nchi kadhaa, juu ya sababu ya kushambulia na ushahidi kwamba kiwanda hicho kilijihusisha na kutengeneza silaha zakikemikali. Wadau wengi walipinga kiwanda hicho kuhusika na madai ya marekani.

Marekani ilisababisha vifo vya raia wasiokua na hatia zaidi kutokana na kitendo chake chakurusha makombora Sudan na Afghanistan, huku ikiwakosa walengwa.

FUNZO DOGO KATIKA MAKALA HII.

i. Ugaidi unapaswa kupingwa vikali kwani unachangia kwa kiasi kikumbwa vifo vya raia wasio na hatia, kama tulivyoona ndugu zetu Dar es salaam lakini Zaidi Kenya waliopoteza maisha. Huku baadhi ya vyanzo vikionyesha kua Zaidi ya watu 300 walipoteza maisha ni raia 12 wa marekani, waliouwawa katika mashambulio haya.

ii. Vyombo vya usalama duniani kote vinapaswa kua makini sana katika ukusanyaji wa taarifa zinazotumika kufanya maamuzi yenye kuleta adhari kubwa endapo taarifa zitakua sio zakuaminika au vyanzo vyakuaminika.

The Eye That Never Sleeps
mfaumehassan@gmail.com
+255 745 624 754
 
Attachments

  • IMG_20190421_194040_088.jpeg
    IMG_20190421_194040_088.jpeg
    191 KB · Views: 95
  • IMG_20190421_193909_008.jpeg
    IMG_20190421_193909_008.jpeg
    67.4 KB · Views: 95
Kila mashambulizi yamepangwa na Marekani, 9/11, Dar and Nairobi Embassy bombings to justify the fight against terrorism.
Kulingana na makala nyingi zilizolikishwa na WiKiLeaks na Jasusi Edward Swoden. Kwamba gaidi Osama Katengenezwa na Marekani ili kufanikisha kampeni ya vita dhidi ya Ugaidi.
Kulingana na shahidi mbalimbali zilizotolewa na Jasusi mbobevu aliyehasi wa Marekani Bw. Edward Swoden Osama bado yupo hakuuwawa na Obama kama inavyoripotiwa kwny vyombo mbalimbali vya habari na yupo kwny payroll ya CIA na anaishi maisha ya kifahari Sana.
Mwisho: matukio mengi yanapangwa ili kutimiza ajenda fulani Kwa maslahi ya muda mrefu ya nchi husika. Uharibifu unaotarajiwa katika matukio hayo unalinganishwa na faida za ajenda hiyo ikionekana faida inayotarajiwa ni kubwa kuliko uhalibifu, basi ajenda inatekelezwa.
 
Muslamu na mwartabu ni mtu hatari sana
Ni kweli kabisa, ila US na UK ni watu hatari zaidi, wanatumia unmanned drone , F-22 raptor na AC-130 gunship kusambaratisha karibu nchi nzima uko Afghanistan,Syria,Myanmar, na ukiripoti habari izo unaswekwa ndani mvua za maana
 
Swali la kujiuliza, Hivi kuna barozi hata mmoja alifariki katika hayo mashambulizi? Kama hakuna je imetokea kwa bahati nzuri au walikuwa na taarifa.
 
Ile bomu nalikumbuka ilitikisa kweli
Mpk majirani na hapo laibon street waliathirika ila serikali ya marekani iliwa compensate

Ova
 
Kama hakuna balozi aliekufa katika hayo mashambulizi, basi hatuna haja ya kujua mchawi ni nani.

Kama hatujawahi kuona hata damu ya Osama, basi hatuna haja ya kujadili ugaidi wakati waongoza ugaidi ndo wahisani wa Dunia
 
Njia iliyotumika:
Malori yenye baruti vilipushi yalitumika kutekeleza mashambulio mbele ya balozi.

Idadi ya waathirika:
Zaidi ya watu 300 (Tanzania na Kenya) waliuwawa huku 4000 wakijeruhiwa.

Watekelezaji:
Azam (alie jitoa muhanga na kujilipua), Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali (mshambuliaji), Fazul Abdullah Mohammed (msuka mipango), Abdullah Ahmed Abdullah (Kamanda wa operesheni).

Al-Qaeda:
Intel CIA yabaini kua mtandao wa kundi la kigaidi al-Qaeda ulihusika ukishirikiana na kundi lingine kutoka Misri.

Osama Bin Laden:
Alitambulika rasmi kama mtu hatari katika uso wadunia hali iliyopelekea shirika la ndani lakijasusi la marekani FBI, kumuweka katika kitabu chake cha wahalifu 10 wakidunia waliohitajika zaidi.

Operation Infinite Reach:
Bill Clinton (1993-2001) aruhusu marekani kujibu mashambulizi kwakutupa makombora na kulipua ngome ya Al-Qaeda huko Khost Afghanistan na kiwanda kikubwa Khartoum Sudan ambacho mmiliki wake alisadikika kua na uhusiano na kumsaidia kifedha Bin Laden.

UN Security Council Resolution 1189:

Umoja wa mataifa kupitia baraza lake la usalama ulipitisha makubaliano (unanimously) yakulaani vikali shambulio la kigaidi Tanzania na Kenya.

Na;
Mfaume Hassani Hamadi.
Mwanafunzi Shahada ya Usimamizi wa Sheria UDSM.
Young Intelligence and Security Analyst.
.

Agosti 7, 1998 balozi mbili za marekani nchi za Afrika Mashariki, Tanzania na Kenya zililipuliwa kwa wakati mmoja katika shambulio lakigaidi lililo ratibiwa na kundi lakigaidi kutoka Misri ambalo ni katika mtandao wa Al Qaeda chini ya Osama Bin Laden.

Zaidi ya watu 213 walipoteza maisha, ikiwemo wafanyakazi na raia wa kawaida. Watu 44 walikua ni wafanyakazi na raia wamarekani (raia 12 wa marekani, na wafanyakazi 32)

Katika shambulio la Nairobi inakadiriwa kua raia 4000 walidhurika na shambulio.
Baada ya shambulio marekani ilikuja kutoa msaada wa kuokoa na pia kuwarudisha nyumbani raia wake walionusurika.

MODUS OPERANDI

Njia iliyotumika kufanikisha mashambulizi ilikua ni vilipushi vya baruti.
Malori aina ya yaliyokua yamejaa baruti yalitumika kusogeza vilipushi karibu na majengo ya balozi.
Jambo ambalo ni baya na lakuhuzunisha kabisa ni kwamba miongoni mwa magaidi waliotumika kutekeleza mashambulio haya walikua ni raia wa Tanzania na kenya, wakishirikiana na raia wengine kutoka nchi ya Somalia na nchi za uarabuni.

Dar es Salaam Tanzania

Ilikua ni siku ya ijumaa tarehe 7 Agosti, 1998, ambapo gari aina ya lori lililokua limebeba vilipushi baruti, lilijaribu kuingia katika eneo la ubalozi lakini likazuiliwa na walinzi getini.

Dereva baada yakuona hivi aliamua kulipusha mabomu yake palepale alipokua. Ilikua mbali kidogo na jengo hali iliyosaidia kupunguza madhara.

Bahati nzuri, shambulio la Dar es salaam halikuleta madhara makubwa ukilinganisha na kule Nairobi. Hii ni kutokana na sababu kua ubaluzi haukua katikati ya mji, na hapakua na makazi ya watu karibu na balozi. Balozi ilikua kando ya mtaa wa Bagamoyo. Watu 11 walikufa na Zaidi ya 80 walijeruhiwa.

Nairobi Kenya

Shambulio la Kenya lilikua ni kubwa Zaidi na lilileta maafa makubwa ukilinganisha na la Dar es Salaam. Hii ni kutokana na location ya ubalozi uliokua Kenya.

Huku mbinu iliyotumika ikiwa ni ileile ya lori, majira ya saa nne na nusu asubuhi watu wawili walikua ndani ya lori lililokua likisogea karibu na ubalozi wa marekani njia panda ya barabara za Moi na Haile Selassie karibu na kituo cha reli. Lilikua Lori dogo lililobeba kilogramu 700 za baruti.

Jitihada zakuingia katika gereji iliyokua chini ya balozi zilishindikana kwa sababu yakukataliwa na mlinzi bwana Benson Okuku Bwaku.

Ndipo gaidi Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali alipoamua kutupa kombora lamkono ambalo lilimkosa mlinzi na kumpa nafasi ya kukimbia.

Gaidi mmoja (Al-Owhali) alikimbia na mwingine alieitwa Azzam alianza kufyatua risasi hovyo na baadae akajitoa muhanga kwa kujilipua ndani ya lori. Mlipuko ulikua mkubwa kiasi chakusikika umbali wa kilometa 16. Ndani ya balozi walikua watu 44.

Mbali na kwamba jengo la ubalozi halikuanguka lote kutokana na uimara wake, vifo vingi vilitokana na mshtuko ulioingia ndani kupitia madirisha na kuangusha baadhi ya kuta za ndani.

Jengo dogo jirani la ufundi lilibomolewa na vifo vingi vilitokea katika jengo hili lililokua anguka kabisa. Raia wengi walikufa.

Hata baadhi ya magari na watu walikua barabarani waliathiriwa na mlipuko wa bomu hali iliyosababisha magari mengine kuchomwa kabisa na abiria wake waliokua ndani.

Operation Infinite Reach.

Baada ya tukio la Agosti 7, marekani haikuridhika kuwaacha magaidi salama na ilitaka kuwapa donda watakalokua wakiliponya kama walivyofanyiwa raia wa marekani na balozi zake.

Mapema ya Agosti 20, 1998, siku ya 13 baada ya shambulio Afrika mashariki, Makombora ya marekani yalielekea huko Sudan kwa Al bashir (raisi aliepinduliwa siku kadhaa zilizopita) na Afghanistan, katika operesheni iliyopewa jina la “Operation Infinite Reach”

Hii ilikua ni operesheni maalumu iliyolenga kumuua kiongozi wa Al-Qaeda Osama bin Laden na washirika wake kama Ayman Al-Zawahiri waliosadikika kuwepo katika kambi ya kundi hilo, katika mji wa Khost Afghanistan.

Operesheni hii pia ililenga kusambaratisha kiwanda cha madawa “Al-Shifa Plant” kilichokua Sudan ambacho kilisadikika kumtengenezea Osama Bin Laden kemikali aina ya “VX nerve” iliyotumika kutengeneza silaha zakikemikali na vilipushi.

Mmiliki wa kiwanda cha Al-Shifa alisemekana kua na ushirikiano na Bin Laden, kwa kumpa msaada wa kifedha.

Sampuli ya udongo uliochukuliwa katika kiwanda hicho ulionekana kua na kemikali ambayo ilitumika katika shambulizi la Afrika Mashariki.
Makombora yalisambaratisha kiwanda na kuua raia 11 wa Sudan.

Raisi wa marekani kwa wakati huo Bill Clinton aliuambia uma na dunia kua marekani isingeweza kuvumilia na ingefanya vyovyote iwezekanavyo kuhakikisha wahusika wa matukio ya kigaidi dhidi ya marekani na dunia kwa ujumla wanakamatwa na kupeleka mbele ya sheria.

Bin Laden Akoswa kuuwawa.

Shabaha kubwa ya marekani ilikua ni kumuua kiongozi wa Al-Qaeda, kitu ambacho hakikufanikiwa kutokana na ukweli kwamba intel iliyotolewa marekani kua Bin Laden alikua katika kambi huko Afghanistan haikua yakweli au kaikufika wakati sahihi.

Mbali na kumkosa Bin Laden, pia hakuuwawa gaidi mwingne yeyote zaidi raia ndio waliokua wameuwawa. Misheni ilienda bumbum.

Marekani Yakosolewa.

Baada ya kusambaratisha kiwanda cha Al-Shifa Plant, marekani ilikosolewa vikali na baadhi ya wasomi na nchi kadhaa, juu ya sababu ya kushambulia na ushahidi kwamba kiwanda hicho kilijihusisha na kutengeneza silaha zakikemikali. Wadau wengi walipinga kiwanda hicho kuhusika na madai ya marekani.

Marekani ilisababisha vifo vya raia wasiokua na hatia zaidi kutokana na kitendo chake chakurusha makombora Sudan na Afghanistan, huku ikiwakosa walengwa.

FUNZO DOGO KATIKA MAKALA HII.

i. Ugaidi unapaswa kupingwa vikali kwani unachangia kwa kiasi kikumbwa vifo vya raia wasio na hatia, kama tulivyoona ndugu zetu Dar es salaam lakini Zaidi Kenya waliopoteza maisha. Huku baadhi ya vyanzo vikionyesha kua Zaidi ya watu 300 walipoteza maisha ni raia 12 wa marekani, waliouwawa katika mashambulio haya.

ii. Vyombo vya usalama duniani kote vinapaswa kua makini sana katika ukusanyaji wa taarifa zinazotumika kufanya maamuzi yenye kuleta adhari kubwa endapo taarifa zitakua sio zakuaminika au vyanzo vyakuaminika.

The Eye That Never Sleeps
mfaumehassan@gmail.com
+255 745 624 754

Sasa hapa umefanya utafiti au umeandika yale yale anayotuhadhithia marekani kila siku? .. kijana kama hii ndio area of interest kwenye career yako basi una safari ndefu!! .. yaani uko shule unasoma lkn bado hutaki kuumiza kichwa? .. huna references wala facts and figures za kueleweka .. aagh haya ndio wasomi wetu nyie tutafanyaje sasa
 
Mm nikukosoe tu kuwa FBI sio shirika la ndani la kijasusi bali ni shirika na upelelezi wa makosa ya jinai
 
Kama hakuna balozi aliekufa katika hayo mashambulizi, basi hatuna haja ya kujua mchawi ni nani.

Kama hatujawahi kuona hata damu ya Osama, basi hatuna haja ya kujadili ugaidi wakati waongoza ugaidi ndo wahisani wa Dunia
Naunha mkono hoja. Hawa ni waongo kama muvu za kina Rambo na vandame. Wanaweza wakaudanganya ulimwengu na kila mtu akakubali uwongo wao.
 
Back
Top Bottom