SEGUZO
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 280
- 196
wakuu kama mnavo fahamu jiji la Dar lilikuwepo kapla mabeberu(wazungu na waarabu) kuingia tanganyika na wenyeji wake ni wazaramo wakati huo mji wao ulikua ukiitwa MZIZIMA, lakini kama kwaida ya mabeberu kwa kuwazarau watu weusi wakaona badala ya jina la kizaramo jiji walipe jina la kiarabu DARUSALAMU na jambo kama hili halikutokea tz peke yake, kuna nchi nyingine matatizo kama haya yalitokea lakini baada ya wakoloni kuondoka, wakarudia majina yao ya asili mfano:HARARE ilikuwa ikiitwa SOLISBARY, MAPUTU ilikua ikiitwa LORENSOMARCUS. kwa hivo basi imefika wakati na sisi kuachana na jina hili lenye mandhari ya kikoloni la daresalaam na kurudi kwenye jina la mwanzo MZIZIMA linalo wakilisha u asilia wetu wa kibantu na kufanya hivyo ni kuwaenzi waasisi wa jiji la dar, ambaye ni nduguzetu WAZARAMO