Jina la ccm lilimaanisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jina la ccm lilimaanisha nini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mfamaji, Oct 19, 2010.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,383
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  CCM ni chama cha ''mapinduzi." Hivi ni mapinduzi gani walikuwa wanamaanisha mwaka 1977? Could CCM be literally meaning REVOLUTIONARY PARTY ?

  Walitarajia kufanya mapinduzi gani?

  Mwenye kufahamu zaidi atujuze wakuu otherwise naona hilo jina hali- represent vision au mision yoyote nikilinganisha na majina mengine kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo. chama cha wanachi , n.k
   
 2. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa nchi yetu ilikuwa ikikabiliwa na maadui wakubwa watatu kama vile; UMASIKINI, MARADHI, na UJINGA, then mwasisi wake, J. K. Nyerere alimaanisha kuyapindua hali hiyo kwa kutangaza vita dhidi ya maadui hao. Lakini badala yake MAPINDUZI hayo yakabadilishwa falsafa hiyo namatokeo yake wakaipindua nchi mithili ya "MIGUU JUU, KICHWA CHINI".
   
 3. S

  So Perfect Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ninavyofahamu hizo CC, zina uhusiano na Catholic na Church, nyerere alikua Genius!
   
 4. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi nawe hapo umeongea, watu wengine wanaongea kama chekechea. Umeambiwa kuna kigezo cha dini kuingia CCM. Tueleze sehemu gani ya katiba ya CCM inasema u-puuzi huu unafyatuka. Halafu toa mchanganuo wa wanachama wa CCM kuthibitisha utoto wako. Kwa maandishi yako haya ukiitwa gaidi utakataa?
   
 5. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo lilikuwa katika kuviunganisha vyama vya TANU na ASP. Na tatizo kubwa lilikuwa likitokea Zanzibar, wakati Nyerere akihitaji umoja zaidi katika utawala ili kutekeleza falsafa yake ya chama kushika hatamu, wazanzibari wao waliogopa kumezwa kwa historia yao na ya chama chao, hivyo viongozi wa ASP walishinikiza ili kuilinda historia ya chama chao lazima tarehe ya kuanzisha chama kipya iwe tarehe 5 mwezi wa 2 ambayo pia ni tarehe ya kuanzishwa ASP, na pia walishinikiza lazima neno "mapinduzi" lionekane katika jina la chama kipya ili kushabihiana na historia yao ya mapinduzi ya Unguja, hivyo kuzaliwa CCM=chama cha mapinduzi.
   
 6. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHAMA CHA MAFISADI...au CHAMA CHA MAJAMBAZI.........!
   
 7. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mapinduzi yana maana nyingi tena yanategemeana na sehemu yanaoyalenga kufanyika.

  UPANDA WA KWANZA
  Nijuavyo mimi mapinduzi ni mageuzi juu ya mfumo,Muhimili, Desturi au kitu fulani na kuweka kitu kingine tofauti. Mapinduzi ni lazima yawe na mwisho. Hapa ninamaanisha lazima kitu kifanyike na kisha kuweka kitu kipya ilikukamilisha ile dhana ya mabadiliko iliyokusudiwa kisha jambo hilo huisha tu mara ile dhana husika inapofanikiwa. Kwa maantiki hiyo ndio ile dhana halisi ya mapinduzi inashika hatamu. Si hivyo tu mapinduzi ni lazima yawe ya lazima, hii ina maana kwamba mapinduzi ni kitu cha kutumia nguvu. Lazima nguvu itumike ili kupindua kile kilicho na nguvu au kile chenye mtazamo tofauti ya kile kinachokusudiwa kuwekwa.

  Kwa maana hiyo, toka CCM ilipoundwa au kuzaliwa baada ya muungano wa TANU na ASP hivyo kufanya yale mawazo yote ya pande hizo mbili yawe wazo moja kuu la kimapinduzi iliisha pale tu walipofanikiwa kuubadili ule mfumo wa kikoloni. Lakini kwa sasa neno MAPINDUZI halina hoja wala maantiki tena.

  UPANDE WA PILI
  Kwa kuwa Tanzania kwa sasa inatangaza kujenga Demokrasia, na mfumo uliopo ndio uleule uliojengwa na hiyo hiyo CCM, basi lengo la MAPINDUZI halipo tena maana huwezi kupindua kitu kilicho chako mwenyewe bali huwa tunabadili kitu kilicho chako au chini yako. Dhana ya MAPINDUZI kwa sasa inalenga zaidi juu ya haki na Mali za raia. Inalenga zaidi juu ya mifumo ya kiraia ambayo ipo na zaidi ya yote ni juu ya rasilimali za kitaifa.

  Ninalazimika kusema hivyo kwa sababu ya haya yote yanayotokea na yanayoendelea kutokea katika nchi yetu tukufu ya Tanzania. Sisemi wabadili la hasha! Malengo na dhana nzima ya MAPINDUZI waliyoyalenga wanajua wao, Ila kwa mtazamo wa nje hilo ndilo linaloonekana, Maana juhudi ya mabadiliko na dhana ya maisha BORA haitokani kwa watu kukaa majukwaani na kupaza sauti zao bila tija .Dhana ya maisha BORA na mabadiliko inatokana na watu kukaa chini na kutengeneza mifumo madhubuti juu ya jambo linalowasumbua. Pia linatokana na nia sahihi juu ya kuwaelimisha watu wote ili washiriki katika kuleta maendeleo yao wenyewe.

  Hapo ndipo tunapata mabadiliko juu ya maisha ya watanzania na si mapinduzi juu ya maisha ya watanzania.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  we ndo ma........... kweli wewe!
   
 9. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  viiii
   
 10. k

  kigulu kimoko Member

  #10
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  badala yake maadui wameongezeka badala ya kupungua,sasa hivi kuna UMASKINI,MARADHI,UJINGA na UFISADI
   
 11. M

  Manyema Senior Member

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Chama Cha Majambazi (CCM)
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,810
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Chama Cha Mafia
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,222
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Complete Corrupted Members

  Imenibidi niseme hivyo kwani Mafisadi wanakipeleka chama kubaya na ndio hiyo maana yake
   
 14. L

  Limbwata Member

  #14
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nahisi ni Chama Cha Mipango.....
   
Loading...