Jimboni Kalenga: CCM wamsimamisha Geodfrey Mgimwa kugombea ubunge

Tume ya uchaguzi KIMYAAAAAA,
Nnape na ccm ndio wanatoa maelekezo eti hawatavulia vurugu!!!!!!

TANZANIA vituko vimezidi.
 
sipendi sipendi sipendi hii tabia ya kutoa watoto msibani na kuwapeleka kwenye meza za siasa. Mgimwa kafa January, week chache mtoto anaogombea kiti chake! Huu ni uchuro.Inakuwa kama walisubiri baba afe ili wamuweke huyo mtoto!
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimempitisha rasmi Godfrey
Mgimwa (32) kuwa mgombea wa uchaguzi katika Jimbo la Kalenga
mkoani Iringa huku kikivitaka
vyama vingine kutanguliza
ustaarabu mara kampeni
zitakapoanza.

Akimtambulisha mgombea huyo
mbele ya waandishi wa habari Dar
es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa chama hicho, Nape
Nnauye alisema CCM imejipanga
kuchukua jimbo hilo kwa kishindo, kama ilivyofanya katika uchaguzi
mdogo wa madiwani, uliofanyika
hivi karibuni, ambapo chama hicho
kimeshinda viti 24 kati ya 27
vilivyokuwa vikigombaniwa.

Aidha Nape alisema pia CCM
imemteua Makamu Mwenyekiti wa
Chama hicho upande wa Tanzania
Bara, Phillip Mangula kuwa Mratibu
wa shughuli zote za kampeni za
chama hicho katika jimbo hilo, lililoachwa wazi kutokana na kifo
cha aliyekuwa Mbunge na Waziri wa
Fedha na Uchumi, Dk William
Mgimwa.

Nape alisema wamepanga kamati ya
siasa ya Wilaya ya Iringa Vijijini na
kamati ya siasa ya mkoa, kuwa
ndizo zitakazosimamia kampeni za
mgombea huyo, zinazotarajiwa
kuanza Februari 19 na baadae uchaguzi utakaofanyika Mach 16
mwaka huu.

“CCM haitavumilia vurugu za aina
yoyote, kama ilivyojitokeza katika
uchaguzi wa madiwani sehemu
mbalimbali, matarajio wenzetu
watakuja na ustaarabu wenye lengo
la kufanikisha uchaguzi ufanyike salama,” alisema Nape.

Aidha, alisema CCM itashinda
uchaguzi huo kwa asilimia kubwa,
kama ilivyofanya mwaka 2010
iliposhinda kwa asilimia 85 ya kura
zote zilizopigwa.

Source: Habari leo

Picha ikwapi tumuone Chifu mtoto anafananaje.
 
ccm mnaharibu chama cha nyerere, hakupenda upuuzi wenu mnaofanya wa kurithisha madaraka kiukoo,
yeye angefanya hivyo mngefurahi?
Acheni mambo hayo, hata kama kakeki ni kadogo acha tukagawane!
 
ccm mnaharibu chama cha nyerere, hakupenda upuuzi wenu mnaofanya wa kurithisha madaraka kiukoo,
yeye angefanya hivyo mngefurahi?
Acheni mambo hayo, hata kama kakeki ni kadogo acha tukagawane!

Kaka huku ni Iringa, haiitwi keki.

Ulitakiwa useme hata kama kambwa ni kadogo acha tugawane !!!!! just a mere joke!!!
 
ingekuwa CDM, tungeambiwa ni ya ukoo, kwa CCM kufa baba kuweka mtoto ni chama cha UKOO AU FAMILIA???
 
Wapenda maendeleo wa kalenga hatumfaham huyu kijana,wetu mgimwa, tunaomba cv yake ili tuwe na uhuru wa kumuongelea. Ukimya sio mzuri .
 
Wapenda maendeleo wa kalenga hatumfaham huyu kijana,wetu mgimwa, tunaomba cv yake ili tuwe na uhuru wa kumuongelea. Ukimya sio mzuri .

CV yake ni mtoto wa marehemu , kama kawaida Mbunge akifa CCM lazima mwanae achukue .Ndiyo CV kubwa na kigezo hicho .
 
Waliompitisha wamemrithisha na CV ya baba yake. Kwahiyo wewe tazama ya Marehemu Dr. Mgimwa ndiyo hiyohiyo waliyoitumia kwenye uteuzi.
 
Ni mrithi wa mgimwa hapo kalenga, nasikia jimbo hilo ni la kina mgimwa tu, wengine kazi yao ni kuwapigia kura tu ili wakale maposho pale mjengoni!
 
Ina Maana mwanamke Pekee aliyezaa mbunge ni wa kwa Mgimwa tu?hawa Wamama wengine Wazaa wapiga kura tu yaani wapnga floe ni ya kura na kwa Mgimwa au wan awake wengine wamezaa jiwe siyo!!!!!!!!!!Kama sumari Kama sioyi Arumeru .Nasari peleka ushuhuda wanakalenga wakuelewe
 
Back
Top Bottom