Jimbo moja tu salama Njombe na Iringa

Jimbo moja tu salama Njombe na Iringa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ni Jimbo la Ludewa la Deo Filikunjombe. Mengine ni utata mtupu. Kuanzia Njombe Kusini na Njombe Kaskazini, Kilolo, Iringa Mjini na mengineyo katika mikoa hii, hali ya CCM si ile ya zamani. Sikuziona dalili za kulirejesha Jimbo la Iringa Mjini mikononimwa CCM.Wananchi wanataka kutuacha mkono. Mchungaji Msigwa bado ananguvu,ushawishi na mizizi.

Wanadai wametuchoka na kutaka kubadili chama cha kuwaongoza. Hatua za harakazapaswa kuchukuliwa. Wananchi wanadai kuwa walihudhuria mikutano ya timu ya KatibuMkuu Kinana ili kusikilizajipya.Hawakulisikia.Hawaoni chochote.Wamebaki kamazamani. Wamechoka yale yale. Wale wa Kalenga,hawajaona tumaini la Mbungempya-Mgimwa.

Kwa Deo Filikujombe, upinzani hauna nguvu kutokana na kukubalika kwa kijanahuyu. Filikujombe anapedwa na wana-CCM na hata wapinzani. Yuko salama na Jimbolake liko salama kwa CCM kulitetea mwaka 2015. Majimbo mengine humu Njombe naIringa ni utata kwelikweli.

Hali halisi humu mikoani ni 'tumbo-joto' kwa CCM yetu. Tusonge mbele tukitekeleza Ilani ili kurudisha matumaini ya wana-Njombe na Iringa kusalia madarakani 2015.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Njombe naIringa)
 
Na iwe kweli mpaka mwisho. Na siku ya kupiga kura mpaka kuhesabu hatutoki maeneo na kura zitalindwa kuliko 2010. Nawashauri CCM waongeze Policcm.
 
Raia akishtuka,fisadi mashakani,wamechoka kuburuzwa!!
 
Mzee Tupatupa hali hiyo ni nchi nzima. Kumbuka kuwa Mkoa huo wakati huo ukiwa Iringa bila ya Njombe mliufanyia sherehe kwa kuwapa kura nyingi ninyi mwaka 2005? Wananchi wanabadilika ila cha ajabu ni hao viongozi wako hawaoni, hawasikii na wala hawataki kupapasa ili kujua. Andika hiyo ripoti ikakae hapo Lumumba bila kufanyiwa kazi hivyo mtakuwa mmechezea pesa za chama bure. Hakika kuna siku kina Elizabon, simiyu yao na wenzao watakuja kukukumbuka watakapokuja kujikuta hawana tena ID za hapa JF
 
Leo nijitambulisha rasimi. Natoka wilaya ya Njombe jimbo LA Njombe kusini na natarajia kuwania Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA.
Jina langu ntafunguka Novemba mosi siku rasimi ya kuongea name wana habari kuweka wazi nia Yang, dhamira, malengo, sababu na CV yangu kwa ujumla.
Ahsanteni.
 
Baada ya kushinda udiwani nadhani CCM imekufa kabisa hapo...

Msalimie sana SAGASAGA
 
Daah ile njombe sijui ndo kusini ile sijui kaskazini aisee nawaaminia
 
Kwa ludewa ni kweli ccm ina nguvu, ila kwa upande wa kata zake kwa kweli ni utata mtupu.
Mlangali iliyokuwa ikiongozwa na chama chenu sasa ipo mikononi mwa chadema baada ya yule diwani wenu kunywa sumu na kufa ili kukimbia madeni.
 
Watanzania tumeshaichoka ccm, hatuna hamu nayo. Tunatamani tuongozwe angalau na chama kingine!
 
Filikunjombe anapigwa vita ndani ya ccm kwa misimamo yake, hatapitishwa na chama chake kugombea.
 
Ni Jimbo la Ludewa la Deo Filikunjombe. Mengine ni utata mtupu. Kuanzia Njombe Kusini na Njombe Kaskazini, Kilolo, Iringa Mjini na mengineyo katika mikoa hii, hali ya CCM si ile ya zamani. Sikuziona dalili za kulirejesha Jimbo la Iringa Mjini mikononimwa CCM.Wananchi wanataka kutuacha mkono. Mchungaji Msigwa bado ananguvu,ushawishi na mizizi.

Wanadai wametuchoka na kutaka kubadili chama cha kuwaongoza. Hatua za harakazapaswa kuchukuliwa. Wananchi wanadai kuwa walihudhuria mikutano ya timu ya KatibuMkuu Kinana ili kusikilizajipya.Hawakulisikia.Hawaoni chochote.Wamebaki kamazamani. Wamechoka yale yale. Wale wa Kalenga,hawajaona tumaini la Mbungempya-Mgimwa.

Kwa Deo Filikujombe, upinzani hauna nguvu kutokana na kukubalika kwa kijanahuyu. Filikujombe anapedwa na wana-CCM na hata wapinzani. Yuko salama na Jimbolake liko salama kwa CCM kulitetea mwaka 2015. Majimbo mengine humu Njombe naIringa ni utata kwelikweli.

Hali halisi humu mikoani ni 'tumbo-joto' kwa CCM yetu. Tusonge mbele tukitekeleza Ilani ili kurudisha matumaini ya wana-Njombe na Iringa kusalia madarakani 2015.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Njombe naIringa)

Kwa research yako hii inamaana Mwenyekiti wetu amedanganywa tena?
 
Daah ile njombe sijui ndo kusini ile sijui kaskazini aisee nawaaminia

Taja kijiji nikudadavulie...

Ila Makinda anapiga makombora ya Scud wapinzani wake ndani na nje ya chama chake na lazima atagombea tena
 
Hata Mwanza hapa sioni dalili za CCM kukomboa majimbo haya, ni vizuri TCD ikakutana na Serikali ili kukubaliana kuwa kila jimbo lazima atangazwe yule aliyeshinda tu ili kuepuka nguvu kubwa kutumika, eti hadi waone wananchi wamechachamaa ndo wamtangaze mshindi kutoka upinzani, hili litafutiwe ufumbuzi mapema kabla ya 2015.
 
Akina Lizaboni, Msalani, Simiyu Yetu na kaka yenu MwanaDiwani njooni huku majimbo yanawaka moto.
 
Back
Top Bottom