Jiko la gesi kuwaka moto

DIBAJI

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
391
Reaction score
513
Habari wadau, Leo asubuhi nimepatwa na mshangao baada ya kuona jiko langu la gesi likiwaka moto na kupelekea kioo cha juu kuvunjika vipande vipande, ikumbukwe kuwa hili jiko lina kama miezi miwili tu toka nimelinunua dukani. Nimejaribu kuwaita mafundi nao wameshindwa kuelewa tatizo ni nini! Nimeamua kuleta uzi kwenu nikiamini JF ni kisima cha maarifa na pia kupata angalizo juu ya vitu vya kuwanavyo makini pindi nitakaponunua jiko jingine. Unaweza angalia picha hapo chini ili angalau nipate msaada wa mawazo.
 
Pole, mwenyewe hiyo kitu imewahi kunitokea, jiko la kioo ni zuri kwa muonekano na upate original, ukipata fake matokeo yake ndio hayo
 
Tatizo mnanunua majiko ya bei rahisi..... Nunua jiko la westpoint original..... Apo ni mkataba.... Mi ninalo mwaka wa tatu Sasa Na bado jipyaaa.... Ila chunga usinunue fake..... Ikiwezekana kanunue kwenye maduka yao ya westpoint
 
Utakuwa hukukaza clamp vizuri gesi ikawa inavuja. Ila gesi imechanganywa na harufu flani hivi, ikivuja tu utaisikia hiyo harufu. Eitther kulikuwa na leakage kwenye piping ya hilo jiko
 
Tatizo mnanunua majiko ya bei rahisi..... Nunua jiko la westpoint original..... Apo ni mkataba.... Mi ninalo mwaka wa tatu Sasa Na bado jipyaaa.... Ila chunga usinunue fake..... Ikiwezekana kanunue kwenye maduka yao ya westpoint
West point ninalo mwaka wa tatu pia, liko vizuri halijawahi sumbua
 
Tena kawaida shukuru Mungu, hivyo vioo vinapasuka na kuruka yaani ni hatari utapoteza Macho.
Sifa ya kioo kinaposhika moto unajuwa? Una Bahati kweli huo moto ungeshika mpira unaopitisha gas ingekuwa hadithi nyingine nyumba nzima
 
Hivi vifaa vya kiwango duni vitatugharimu! Kuna extension nazo inaweza kuungua tu kamakaratasi!
 
Brand ya ZEC/BOSS nayo mruuua zaid ya Westpoint wakuu.
 
nilipokuwa nanunua jiko bahati nzuri nilipata kumuona fundi majiko yupo pale bigbon kko anauza vifaa/spaire za majiko alinishauri nisinunue jiko lenye kioo....hakuwa na sababu ya msingi ....ni fundi wa kujifunza kwenye kazi (on job training) so nilimsikiliza....though nilitamani muonekano wa jiko la kioo
 
Hicho kioo kinakaa wapi na kazi yake nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…