Jiji la Mbeya kama kijiji

Jiji la Mbeya kama kijiji

mbeya ni shidaaa yaani washamba mpaka kero utawakuta airport kwa mamia mpaka leo kushangaa fastjet
 
Ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwepa fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua)

We kilaza Songwe mpaka mbeya town naamini ni zaidi ya 20km unashangaa kulipa 10000 ilihali Dsm airport to city centre tunalipa tax 25000 halafu unalialia kwani ulikuwa na sh?

Jambo la pili yawezekana mbeya ikawa na mapungufu yake ila sio kwa kiwango hicho kwani miji mingi ya tanzania ni kituko kila mkoa unamapungufu yake ila kwakuwa mkataa kwao mchawi basi kila mtu hapa atajikweza oohh mkoa fulani uko hivi na kwakuwa ni ngumu kupata jazba ya mawazo ya wengi kwakuwa nature ya maisha yetu bongo haitupi fursa kutembelea mikoa mbali mbali kama utalii wa ndani ila kwa wenye kazi ambazo zimetusaidia tembelea mikoa mingi nadiriki kusema tofauti ya maendeleo katika mjiji yetu ndogo sana,Dar yetu hii mji wa kukopa ndio hovyooo kabisa sema tu kazi ndio zinatuweka hapa na fursa ya mzunguko mkubwa wa pesa.
 
Iv lile soko la mwanjelwa halijamalizika tu maana huu mwaka kama wa tano nahis tok 2010, mara ya mwisho mwaka jana 2014 mwez wa 7 nilipokuwa huko lilikuw kwenye hatua za mwisho japo naona limecheleweshwa sana
 
Jiji sio hotel. Kuna vigezo ving vinaangalia mpaka sehemu ikaitwa jiji. Usha jiuliza kwabin waliamua kuita jiji despite ya kuto kuwa na hotel nzur?
 
Uache ushamba mtoa mada kisafari kimoja tu hapo mbeya unapiga kelele je siku ukipewa assignment katavi si utalia usiku kucha! kwani kwako ni nyumba ya hadhi ya nyota tano tv mpk chooni? kwa mbeya varieties ya chakula usipime hakuna mikoa mitamu kama mfano wa mbeya,mwanza na arusha kwa uzuri wa vyakula na hata ukaribu wa wenyeji.
 
kama mnaona wamelala kwanini msiitumie hiyo fursa kufungua HOTEL NA PUB za hadhi muitakayo?
Kama vp mtuache watu wa mbeya ,tumeridhika na mji wetu
uliyesema sisi wachawi , ni UCHAWI gani unaozungumzia hapa?..maana unafki kama wa mtoa thread nao ni UCHAWI pia!
Karibuni MBEYA muwekeze, ili iwe vile mnavyoiwazia
Mleta thread anamaanisha UCHAWI wa kuwanga yaani kuloga
 
andreakalima,
kwanza we panya kabila gani,walikupiga kipapai kabla hujafika kwasababu ulikua unaenda na nongwa.jaribu kwenda ukiwa free minded then utajua uzuri wa mbeya.
tulobwike ndagha kikulu
 
Japkas,
Uchawi ndio abusive language? mbona aliyosema mleta thread ni ya kweli au unajitoa ufahamu bosi.
 
mbeya muone na aibu kutetea upuuuuzzz. tembeen hata arusha mjifunze
 
Bora Mbeya ni jiji.

Moshi ni manispaa lkn watu wake wamejaa misifa kibao
 
Mbeya sijui tatizo ni nini hasa, maana ni kama HIROSHIMA-NAGASAKI baada ya kupigwa bomu na marekani vita vya 2 ya dunia kuisha. Sasa Kazi tu mpunguze ULOZI!!!
 
Ukiwa nje ya Dar majiji ni Arusha na Mwanza tu.................Arusha na Mwanza hutoboreka.....kumechangamka......sehemu classic na kisasa kutembelea zipo kibao.....si mji unaitwa jiji unaomba kupelekwa hotel 1st class unapelekwa hotel za Temeke stereo nafuu..........:der:
Hata Dodoma , Moshi na tanga kuna hotel nzuri bomba
 
Mbeya sijui tatizo ni nini hasa, maana ni kama HIROSHIMA-NAGASAKI baada ya kupigwa bomu na marekani vita vya 2 ya dunia kuisha. Sasa Kazi tu mpunguze ULOZI!!!
Kweli Mbeya Kwa sasa ni makao makuu ya Ndumba za kila aina .
 
ULOZI ni mambo yote ya UCHAWI (ikiwemo uki-gagula, kupaa angani na ungo, misukule na ufirauni)
 
Hata Dodoma , Moshi na tanga kuna hotel nzuri bomba
Kiuhalisia huwezi kuifananisha Moshi na Mbeya kwa Uzuri wa mji na majengo hata mandhari yake...kamwe hiyo nakataa

Dar es Salaam kuna sehemu umejengwa vibaya sana but sehemu ulipojengwa vema unausababisha uvutie ila kwa Mbeya I can say ni mkoa wa mwisho kabisa hapa Tabzania kwa kuvutia..Umejengwa vibaya sana na yale matofali yao yasiyochomwa unaonekana umechoka sana but nafikiri ni mkoa ambao kama ungejengwa angalau vizuri kidogo na nyumba za hadhi ungekuwa mkoa unaovutia sana kutokana na geographical yake ya miinuko miinuko
 
Last edited:
Back
Top Bottom