Jiji la Mbeya kama kijiji

Jiji la Mbeya kama kijiji

sijui ni vigezo gani vinatumika kuupandisha mji kuwa jiji lakini kwa Mbeya na Tanga TAMISEMI walichemsha, hii miji inashindwa hata na mji wa Dodoma kwa kweli...kipindi cha Pasaka nilikuwa Dodoma yaani pale pako bize sana na mzunguuko wa pesa ni mkubwa labda kutokana na shughuli iliyonipeleka pale sijui kwa seckta zingine...pale Arusha napo ni padogo mno yaani kamji kamejibana sehemu moja tuu, ukiitembea mwendo wa kilometa 5 tuu upo nje ya mji....Mwanza ni nyumbani naomba nitoe pongezi kwa Wasukuma wenzangu mlioamua kubaki na kuuendeleza mji, ndiyo sehemu pekee ambayo nikiwa nje ya Dar bado najiona nipo mjini nikiwa Mwanza, ni pazuri sana.

Mkuu G.Jacob unataka kunambia Dodoma unaizid Mbeya kwa mzunguko wa Pesa,you must be mada..very mad..
 
Last edited by a moderator:
"Mbeya ni kijiji kikubwa"......By Olenjolay...

Kwi kwi kwi kwi kwi.....Teh teh teh teh teh....Ha ha ha ha
 
Ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwepa fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua) nikafika hoteli ambayo ndio wanaisifia ni classic (Mbeya hotel) duuh ni kama nyumba ya makumbusho nikamuambia dereva nipeleke nyingine tukaenda Paradise Hotel (nayo ya kipuuzi pia) nikaenda nyingine (GR City) daah ndo nikajua kumbe zile sifa za wanyakyusa hapo Dar kwao hamna lolote sasa sehemu ya kula ndo ishu yaani labda uende CITY PUB hakuna sehemu nzuri ya kupata varieties.

Poor Mbeya inastahili kuitwa KIJIJI CHA MBEYA si JIJI LA MBEYA mmekalia UCHAWI tu.

kwanza mweshimiwa ujatuambia unatokea wapi?pili ninauwakika hujui vigezo vinafyo zingatiwa sehemu kuitwa jiji,tatu unamatatizo binafsi na nina wasisi wewe(ni nsukule)jibu ninalo taka nikujibu niambie unatokea wapi? bana usije ukaniambia undokea dar mara mlio wengi ni washamba mkifika dar mnataka hadi mikoa hiwe hn mlimani city(unamental disorder)
 
Ukisikia jiji la mbeya utafikiri bonge la jiji kumbe upuuzi mtupu. sasa hapa kati nilipata safari ya mbeya nikakwepa fastjet ile kutua kwa kweli uwanja wa songwe ni mzuri kiasi (pengine kwa sababu ya upya) sasa tukapanda shuttle kwenda mjini 10,000/= (bei ya kulangua) nikafika hoteli ambayo ndio wanaisifia ni classic (Mbeya hotel) duuh ni kama nyumba ya makumbusho nikamuambia dereva nipeleke nyingine tukaenda Paradise Hotel (nayo ya kipuuzi pia) nikaenda nyingine (GR City) daah ndo nikajua kumbe zile sifa za wanyakyusa hapo Dar kwao hamna lolote sasa sehemu ya kula ndo ishu yaani labda uende CITY PUB hakuna sehemu nzuri ya kupata varieties.

Poor Mbeya inastahili kuitwa KIJIJI CHA MBEYA si JIJI LA MBEYA mmekalia UCHAWI tu.

Wewe sema tu ulikuwa unataka wana jf wajue kuwa ulienda kwa Fastjet.
Inaonekana hujui hata ni vigezo gani huwa vinatumika sehemu fulani kuitwa jiji nk.
Ila usijali tumejua ulipanda fastjet
 
khaaa umechukia sana aisee, sikujui mbeya, so sina comment. Ila suala la uchawi kwani limeingiaje hapo? au wameku-mbeya?
 
Mi ninachokumbuka nimeacha watoto wawili huko dume na jike enzi hizo kutoka mafiati to uyole ghorofa refu"mbili" lilikua mwanjelwa la jamaa mmoja anaitwa mfikemo ila juzi kati naona wamejitahidi kuanzia pale njia panda ya air port/mafiati/uyole wamejenga viota. Mwanjelwa/kabwe/soweto/tunaruka hadi Ilomba na uyole hapa ndio jiji linatakiwa kuonyesha taswira.
 
Mkuu Bateko kama umetumia saa tatu toka Nyakato hadi Liberty lazima ulikuwa unatumia baiskeli zile za walemavu za wheelchair. Nyakato hadi Liberty kwa miguu hardly nusu saa, kwa gali wakati WA foleni ya asubuhi dk 25, mida mingine isiyo na foleni Ni dakika 10 tu. Msiwe mnatupia uongo humu as if wasomaji ni watoto wadogo.
Mkuu huyu ni wa kuhurumia tu! Atakuwa anaizungumzia Mwanza ya Madaso na siyo Mwanza tunayoifahamu!
 
Last edited by a moderator:
Tanzania yote kwa ujumla miji yake haijapangwa vizuri, hakuna anayejali...watu wako busy maofisini wanakimbizana na Posho za vikao, per diem, na dili za viwanja vya makazi. Maeneo ambayo hajaendelezwa wanapima viwanja vya makazi wanapeana ili waje kulangua baadaye.

Kuna haja ya kuwapeleka maafisa mipago miji wetu kwenye miji ya watu iliyopangwa ikapangika vizuri wawe exposed.
Nimepata fursa ya kutembelea mikoa mikubwa kwa midogo ya Tanganyika hali ni mbaya, na hapo nchi ya jirani Zanzibar ni yale yale.

Unapotua Dsm unajiuliza kama unachokiona ndo kinachoonwa na wanaotunga sera za adhi na kuzisimamia yani ni shidaaa!

Mji wa mbeya ndo tumefeli ingawa tunanafasi kubwa ya kujirekebisha, wana mby kama mtakumbuka kulikuwa na msitu mkubwa pale forest kati kati ya mji, nini kimetokea pale kumejaa nyumba za makazi hakuna maeneo yalioachwa wazi kupendezesha mji kwa bustani za kupumzikia. Ilikuwa ni kuuza viwanja kwa kwenda mbele... jiji lingewachukua hawa jamaa liwapeleke hata China, au Singapore tu wakaone miji inavyopangwa, naona makosa yanaendelea wamepima Iwambi, Tazara watu wako busy na deal za viwanja. Mbalizi mpaka songwe hamna kitu, Uyole, Ituha ni holela....
Mji wetu unakuwa sasa tutumie vizuri maeneo ambayo hayajaendelezwa...
 
Back
Top Bottom