Hii Mada ni Nzuri sana,
Tatizo la msingi hapa ni wizara ya aridhi, na sio kila kitu tulaumu serikali kuu.
Tatizo la aridhi linaanzia kwenye serikali za mitaa na kufikia wizarani, upimaji wa viwanja imekuwa ni tatizo kubwa sana hapa tanzania, na kama tungeliangalia hili tungeondoa matatizo mengi sana, kwa kweli hakuna sehemu yenye ubabaishaji mkubwa kama wizara ya aridhi na wababaishaji wala sio wanasiasa bali ni watendaji wa wizara, watu wanafikiria pesa tu na sio kufanya kazi. Ukienda serikali za mitaa kwa maswala ya aridhi ubabaishaji, ukija wilayani kitengo cha aridhi ubabaishaji ukienda wizarani ndio kabisaaa….. watu wanakuangalia tu, waziri husika yupo!, naibu yupo!, Katibu na wakurugenzi wapo tu wanatafuna pesa za Kodi zetu na hasa lipa kama unavyopata.
Kwenye miradi ya upimaji Viwanja ndio balaa kabisaa, kama kunaeneo linapimwa viwanja ni maafa, habari sahihi hazitolewi, wanachi hawaelezwi nini cha kufanya na wala hawaambiwi haki zao, tunaoharibu nchi hii wa kwanza ni sisi wanachi hasa watendaji wa ngazi za chinina pili ni viongozi wa juu kushindwa kuwawajibisha watendaji wabovu.
kwa mfano; hivi kunaubaya gani kuwaeleza wakazi wa kigamboni ukweli na kuchukua hatua haraka kuliko kuwababaisha mara kuna mradi, mara hakuna, uongo mtupu, ifikie mahala watu wajifunze kusema ukweli ili kurahisisha mipango ya nchi, ni busara kuwaeleza wanachi kuwa eneo hili litajengwa barabara na wote waishio hapo wanatakiwa kufanya A,B,C na kama unamaswali Uliza office Z na wakifika huko Office Z wamwone office Y na Officer Y ajue cha kuongea na Wanachi na ukweli tu, hata kama kitawauma wanchi lakini ikiwa ni kwa mujibu wa sheria nafikiri wataelewa cha msingi ni kuangalia haki na maslahi ya pande zote mbili, na sio maslahi ya watendaji ambao wanalipwa mishahara kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Pia hakuna mawasiliano kati ya wizara moja na nyingine, kwa mfano kukiwa na mradi wa upimaji viwanja wizara ya aridhi inatakiwa iwasiliane na wizara nyingine husika ili wawe na mpango kazi wa pamoja na ndipo utaona , upimaji utaenda sambamba na upimaji wa barabara, tanesco nao watafika, maji nao pia, Afya,Elimu nk. Na tutaepusha mpangilio mbovu wa makazi na bomoa bomoa zisizo za lazima na zinazo umiza wanchi hasa wa kipato cha chini, wewe unafikiri nani atasubiri kwa miaka 10 mpango wa kupima viwanja na ilihali anakaa nyumba ya kupanga! Hapa inaatkiwa wanachi wapimiwe viwanja kwa haraka na kuwapa plan ya jinsi ya kujenga Simple!
Tatizo kubwa la Watz ni ubinafsi wa kutaka kujilimbikizia mali, kwa mfano utaambiwa mkubwa flani ana hekari 500, pwani, 300 MZA, 80 Lindi, 200 Kigoma zote hizo za nini? mapori Tu! na ukija mradi kigamboni wakubwa wanataka viwanja Vyote, Tamaaa ya nini, mwisho wa siku utahitaji 6x4 sq metres and 6 ft down, Tubadilike kwa maendeleo ya nchi hii.