Jihadharini na Matapeli wa Mtandaoni!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jihadharini na Matapeli wa Mtandaoni!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Jul 5, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu alipost kwenye hii website ya watanzania Tanzania | About Tanzania, Tanzania Information, Tanzania Directory > ZoomTanzania.com tangazo la kuuza gari. Akapokea simu jamaa wanaitaka gari toka mkoani alieyongea ni mtu mzima, jamaa aliyempigia akadai atamtuma mtu wawasiliane ili aje kuiona gari na kuikagua kwa kesho yake kwa kuwa yeye yupo mbali. Siku iliyofuata akapokea simu nyingine toka kwa jamaa aliyejitambulisha kuwa ametumwa na Baba yake ili kuona gari. Ndugu yangu akaenda kuonana nae pale waliposema waonane, bahati nzuri ndugu yangu alikuwa na mwezake kwenye. Wakamkuta yule alijifanya ni mteja pale walipopanga kukutana, akaikagua gari, adai ipo njema na kutaka waongee bei vizuri. Baadae akajifanya anataka kulipa cash kama wataafikiana, waonane tena sehemu nyingine waandikishane kwa wakili ili alipe, ndugu yangu akakataa kupokea cash, basi yule jamaa akamweleza kuwa itabidi waende Benki ili ikiwezekana jamaa aondoke na ile gari siku hiyo hiyo kwa kuwa inatakiwa mkoani.

  Ndugu yangu akaanza kuingiwa na shaka, lakini moyo ukamsukuma akubalia waende Benki, lakini jamaa akadai waende kwanza Benki ambayo Baba yake atatumia ili achukue hela kisha waende wakaweke kwenye Benki ya Ndugu yangu baadae waandkishane kwa wakili.

  Wallipokaribia kwenye Benki ambayo huyo jamaa alidai waende kuchukua hela, akaomba wasiamame kidogo, wakiwa bado kwenye gari, jamaa akajifanya anataka kupiga simu kuuliza kama Baba yake ametuma fedha katika ile Benki, akamwomba ndugu yangu ampe simu aitumie kwa kuwa yake imeisha vocha.. kwa kuwa walikuwa katika gari, ndugu yangu hakuona shida, akampa..jamaa alipokea tu akafungua mlango fasta na kutokomea mtaani...
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  aiseee poleni sana ndo bongo dar es salaam..
   
 3. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuh bongo bana dah uckute cm yenyewe ya kichina.
   
Loading...