jihadhari na vikundi vya jogging vya alfajiri (saa 11-12 asubuhi)

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,698
1,396
Ndugu zangu, kuna hivi vikundi vya jogging vinavyoibuka kila uchao.Kiukweli hivi vikundi kiafya vina faida mno na mara nyingi vikundi hivi hukimbia siku za Jumapili.

ILA SASA KUMEIBUKA WIMBI LA WEZI/VIBAKA NA WANYANG'ANYI KUPITIA MWAMVULI WA JOGGING "tena hawa utawaona hadi siku za kaz".

Ikitokea umedamka asubuhi sana barabarani (saa11-12 asubuhi) kwa shughuli zako za mihangaiko ya siku na ukaona vikundi vidogovidogo vya joggers(obvious watu 4-5) vinakuja uelekeo wako hebu jitahidi ukae mbali aidha kwa kukimbia au kujificha.

HIZI NJEMBA HUKUVAMIA GHAFLA NA KUKUPORA NA KUKUVUA KILA WAWEZACHO "wanakuwa na vibegi mgongoni" this happened kwa jamaa yangu mmoja hapa mtaani na aliporwa wallet na smart phone.

BE WARNED
 
Mimi nikienda mazoezi muda huo wa asubuhi sana au jioni sana kwenye viwanja vya wazi huwa naacha simu na hela.

kuna wale wanaodamka asubuhi kwenda makazini.nyumba za ibada....kuna wale ndugu zetu wa kutia mtungi hadi alfajiri wawapo wanarudi majumbani..
MUHIMU NI KUCHUKUA TAHADHARI JUST IN CASE IKITOKEA. Zion Daughter
 
Last edited by a moderator:

Yes I agree with you.Kwa upande mwingine wanaweza hata kukudhuru hawanaga huruma hasa wakikosa wanachotaka.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo mbinu ipo tangu kitambo, sema hukuijua tu, tuulize wakazi wa Mwananyamala komakoma, ujiji na kwa mama Zakaria tukujuze na mbinu nyingine za makundi kama Yakuza, akina Mashukurumbwe......... stay tuned.

tupe uzoefu kaka nasisi tujipange mkuu...maana wengine haya mambo huku kwetu mapya kwa kweli mkuu
 
hata kariakoo tu haishauriwi kwenda saa 12, 1 au 2 asubuhi, huwa wanakaba sana ukikaa vibaya mida hiyo coz maduka mengi yanakuwa yamefungwa
 
Hiyo mbinu ipo tangu kitambo, sema hukuijua tu, tuulize wakazi wa Mwananyamala komakoma, ujiji na kwa mama Zakaria tukujuze na mbinu nyingine za makundi kama Yakuza, akina Mashukurumbwe......... stay tuned.
kuna jamaa yangu mmoja anakaa m/nyamala ujiji. miaka kadhaa iliyopita nlienda kumtembelea sikuwa napajua kwao..yeye ananiambia ukishuka hapo stand(msikiti) nsubiri nakuja..aliniweka kama 20 minutes nabung'aa pale...KILA NKICHEKI MATEJA KIBAAOOO HALAFU MAWASILIANO NA JAMAA YANGU NI KWA SIMU..aaisee hadi anafika alinikuta nimenuna vibaya mno..na kama sio kuheshimiana ningemchapa makonde.. na nikaapa kwao siendi tena...wale jamaa/junkies unawasikia kabisa wanakupigia hesabu.."SHIKAMOO MWANANYAMALA UJIJI".. ila nlichoka zaidi nlikuta wahuni wanacheza kamari ya penalti~penalti/matuta..unaweka hela mnapigiana penati wawili wawili ukipigwa umeliwa...ahahahah daah
 
hata kariakoo tu haishauriwi kwenda saa 12, 1 au 2 asubuhi, huwa wanakaba sana ukikaa vibaya mida hiyo coz maduka mengi yanakuwa yamefungwa

thanks for the infos..nakubaliana nawewe back in the days wakati nasoma benja mkapa in the early 2000's .nlishuhudia hilo mitaa ya mchikichini..thank god walituachaga na viuniform vyetu..
 
thanks for the infos..nakubaliana nawewe back in the days wakati nasoma benja mkapa in the early 2000's .nlishuhudia hilo mitaa ya mchikichini..thank god walituachaga na viuniform vyetu..

nina ndugu yangu maisha yalishamchosha, huwa anashinda kariakoo kazi yake ni deiwaka na wale wanaoweka vitu chini. huwa tunamhisi kuwa kibaka japo anakataa. huyu ndio alinionya akaniambia kariakoo ufike kuanzia saa 3 au 4 ila kabla ya hapo usilaumu. kama imelazimu uwe hapo muda huo basi usiende na vitu vya gharama au hela
 
Back
Top Bottom