Jihadhari na tapeli wa mabwawa ya samaki

Jihadhari na tapeli wa mabwawa ya samaki

TENGEFU

Senior Member
Joined
Jan 25, 2017
Posts
138
Reaction score
206
Kuna kampuni inaitwa Positive Eye yenye ofisi zake ndani ya viwanja vya nanenane Arusha. Hawa wanajitangaza wanatengezeza mabwawa ya samaki ya kuhamishika nk. Mkurugenzi (anajulikana kama "Atukuzwe")wake anatuma watu kukagua eneo lakini yeye hafiki zaidi ya kukwambia umwekee hela kwenye akaunti.

Ukishamwekea hela mchezo unaanzia hapo. Atawatuma watu walete vifaa kama nguzo nk kama kama ushahidi na hapo utawaona hadi uwatafute wakwambie tutakuja na itaendelea kwa namna hiyo huku akichukua fedha sehemu nyingine kwa mtindo huo huo.

Huyu Mkurugenzi huwa hafiki site zaidi ya kuchukua hela na kuanza kutoa maelekezo ya uongo na hivi ndivyo anavyoendesha maisha.

Natoa tahadhari kwa wale mlioko Arusha na mnaotamani kutengenezewa mabwawa ya samaki ni vema mkatafuta makampuni mengine yanayoeleweka na siyo Positive Eye la sivyo utajikuta na wewe unatapeliwa.

Mimi na marafiki zangu watatu ni waathirika kwenye huu utapeli ambao unakuwa very soft kiasi cha kutoushtukia.
 
Sio bure mtoa wataibuka matapeli wa kila namna kinachotakiwa ni serikali kuwakazia buti
 
Nimeshasikia watu kadhaa wakiilalamikia hii kampuni na sijui kwa isingechukuliwa hatua wakalipa hela za watu
 
Mbaya zaidi target yao ni vikundi vya wajasiriamali haswa akina mama kwa hiyo natoa wito kwa wale wenye passion na ufugaji wa samaki msiingizwe mkenge makajutia kupoteza mitaji yenu mliyokopa VICOBA
 
Wanajua sana kujieleza na hiyo ndiyo sifa kubwa ya matapeli
 
Maelezo yaliyotolewa yanatosha kuwatia hatiani kwani kilichobaki ni polisi kufanya kazi yake ili watu wasiendelee kutapeliwa. hela n ngumu sana kipindi hii
 
Sasa mkurugenzi aje site, office haimishie kwenye mradi wako??? Au labda wewe ndiyo mteja pekee?? Ama twambie anatuma watu wasiofaa kwa kazi yako?? Au labda unamhitaji site mkafanyeje linashindwa kufanyika hapo ofisi kwake ukimfuata?? Pia usishangae mkurugenzi hajui kabisa hizo mambo za mabwawa, kikubwa fuatilia vizuri kama hujaridhika na huduma.
 
Sasa mkurugenzi aje site, office haimishie kwenye mradi wako??? Au labda wewe ndiyo mteja pekee?? Ama twambie anatuma watu wasiofaa kwa kazi yako?? Au labda unamhitaji site mkafanyeje linashindwa kufanyika hapo ofisi kwake ukimfuata?? Pia usishangae mkurugenzi hajui kabisa hizo mambo za mabwawa, kikubwa fuatilia vizuri kama hujaridhika na huduma.
HUWEZI KUCHUKUA CONTRACT HATA HUJUI HIYO KAZI INAFANYIKA WAPI; SUALA LA KUFANYA MONITORING NI KAWAIDA KABISA HAJASEMA MKURUGENZI AHAMISHIE OFISI HUKO. Mkurugenzi responsible lazima awakague wafanyakazi aliowapa majukumu kuona kama kazi inakwenda au kuna uchakachuaji. mawaziri wanakahua barabara sembuse huyu ?
 
Huyu ni tapeli na anafahamika. kwanza TRA wafuatilia pia wachukue kodi yao kwani inawezekana anatengeneza hela nyingi chafu
 
Sasa mkurugenzi aje site, office haimishie kwenye mradi wako??? Au labda wewe ndiyo mteja pekee?? Ama twambie anatuma watu wasiofaa kwa kazi yako?? Au labda unamhitaji site mkafanyeje linashindwa kufanyika hapo ofisi kwake ukimfuata?? Pia usishangae mkurugenzi hajui kabisa hizo mambo za mabwawa, kikubwa fuatilia vizuri kama hujaridhika na huduma.
Ndio wewe nini mkuu?
 
Niliona tangazo lao zoom wakitafuta mtaalamu wa samaki nikatuma maombi yangu .....

Baada ya siku kama tatu hivi wakanitumia SMS kuwa watanitafuta siku yoyote kwa ajili ya kufanya usaili wa mwanzo mpaka leo naona kimya....

Nashawishika kuwa nahisi vyuma vitakuwa vimewakazia kwelikweli mpaka kufikia hatua ya kutaka kutapeli watu.....
 
IMG_20161118_182603.jpg


KWA ENEO NA GHARAMA KIDOGO FUGA SAMAKI WENGI NA BILA KULAZIMIKA KUCHIMBA ARDHI



1.Tunaelimisha jamii kuhusu teknolojia mpya za ufugaji samaki kisasa


2.Tunawajengea wateja wetu mabwawa yakisasa ya ufugaji samaki yanayojengwa kutumia mabanzi au yale ya kuhamishika ambayo mara nyingi tunatumia chuma na turubali maalum



3.Tunawauzia wafugaji wa samaki kila wanachohitaji kufanikisha ufugaji wa samaki kisasa, ikiwemo vyakula, na mabwawa yaliyotayari na mbegu bora ya samaki kwa gharama nafuu.


4.Tunatoa huduma za ushauri wa kitaalam zaidi kwa wale wafugaji walioanza ufugaji samaki kisasa kwa kujengewa nasi kwa teknolojia tunazowajengea au kuwauzia.



5.Tunatoa ushauri wa kuhusiana na upatikanaji wa soko la samaki haswa kwa wafugaji walioanza kufuga kwa msaada wetu.


6.Malengo yetu nikufanya ufugaji samaki kuwa rahisi kadiri iwezekanavyo, utumie eneo dogo kwa uzalishaji mkubwa, hii tunafanya kwa kutumia ubunifu na kuchanganya teknolojia yetu na ya ufugaji samaki kwenye mataifa yaliyoendelea iwe rahisi kufanyika kwa mazingira yetu.



7.Tuna malengo yakuzalisha minofu ya samaki na na bidhaa nyingine zitokanazo na samaki kwa soko la ndani na la nje, hivyo mbeleni tutafanya ufugaji wa kimkataba na wafugaji wa samaki waliokwishabobea kwenye ufugaji huu wa kisasa chini ya uangalizi wetu nakuwaakikishia soko la samaki watakaozalisha.


UFUGAJI SAMAKI

Kwa miaka mingi imekuwa kawaida kwa watu wanapotajiwa ufugaji wa samaki moja kwa moja hupata picha au kuanza kufikiria mchakato wakupata makatapila au mtaji mkubwa kuchimba mabwawa.

Positive eye Co. Ltd inakuwa kampuni ya kwanza kabisa kutambulisha Tanzania ufugaji wa samaki kisasa na kibiashara katika mabwawa yasiyochimbwa ardhini ambayo yamekuwa yakitumika katika nchi nyingine mbalimbali ikiwemo Kenya kwa kitambo sasa, na hata sasa kampuni hii imeweza kubuni na inaendelea na tafiti zakibunifu za aina nyingine ya mabwawa ambayo hufaa kuamishika kwa wafugaji wanaokaa eneo lisilokuwa lakudumu au nyumba yakupangishwa kunufaika na ufugaji samaki.

Katika teknolojia hii ya ufugaji samaki kisasa, tofauti na inavyofaamika kitaalamu na ilivyosomwa na wataalam wetu wa kilimo kwa miaka mingi kuwa utaweza kufuga samaki 3-4 tu kwa eneo la mita moja mraba. Kwenye ufugaji huu teknolojia na uwezo wakuthubutu kujiongeza kijasiriamali vimebadilisha mambo, kwani utahitaji eneo la mita 4 urefu, mita 2 upana na mita 1 kina kuwezakufuga samaki 1000 aina ya kambale au wastani wa tilapia 300-400 na kulazimika kubadili maji nusu ya ujazo mara moja tu kwa wiki.

Kutengenezewa mabwawa haya utahitaji kuwa na mirunda kidogo na mabanzi ambayo yatatumika kutengeneza umbo la bwawa la samaki kwa kuinua juu bila kulazimika kuchimba chini na baada ya hapo yatawekewa karatasi maaalum yakuhifadhi maji(tazama picha hapo chini kwa uelewa zaidi). Karatasi hizi ziko za aina tofauti zikitofautiana kwa ubora na muda wakudumu, Japo wengi huanza mradi huu kulingana na uwezo wakimtaji wa mhusika lakini sisi tunashauri aina bora ya karatasi ambayo ni gharama juu kidogo kuinunua lakini inawezakudumu kwa wastani wa miaka hadi 30 endapo itatunzwa vyema

Katika ufugaji huu wa samaki kisasa samaki aina ya kambale watawezakufikia kuvunwa yaani uzito wa kati ya 1-1.5kg ndani ya kipindi cha miezi 6-8 tu, kutegemeana na sababu mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula bora ,hali joto ya wastani mzuri ambavyo huchangia ukuaji wa haraka wa samaki na maji.

TATHMINI YA UZALISHAJI, SOKO/UHITAJI WA SAMAKI DUNIANI

Imethibitika upatikanaji wa samaki kwenye vyanzo vya asili umekuwa ukiendelea kuporomoka kutokana na uvuvi haramu, uchafuzi wa maji na kemikali toka viwandani, n.k,huku uhitaji wa nyama nyeupe umekuwa ukiendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku. Tathmini inaonyesha miaka ya 1970 ni wastani wa 5% tu ya samaki walioliwa duniani walitoka kufugwa, Hivi leo nusu ya kiwango cha samaki wanaoliwa duniani ni wakufugwa, na baadhi ya wanasayansi wametabiri hadi ifikapo mwaka 2048 hazina ya samaki wote wapatikanao kwenye vyanzo vya asili itakuwa imekwisha hivyo kulazimisha uhitaji wote wa samaki duniani kutoshelezwa kwa samaki wafugwao kibiashara mashambani mwetu, hivyo kuthibitisha fursa ya kuzalisha samaki kulisha dunia na idadi kubwa ya watu inayoongezeka kwa kasi kuliko uzalishaji wa chakula kinachohitajika mwanadamu kuishi vyema.

Tembelea: All seafood will run out in 2050, say scientists

Kanuni ya uhitaji na uzalishaji (demand & supply principle)

Kanuni ya kiuchumi ya uzalishaji na uhitaji inasema “mara zote kunapokuwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa yeyote sokoni kuliko kiwango cha uzalishaji au upatikanaji wake basi bei itakuwa juu” na vivyo hivyo uzalishaji ukiwa mkubwa kuliko uhitaji bei ya bidhaa hiyo itakuwa chini. Kwa kutumia kanuni hiyo fanya ufuatiliaji utagundua nyama ya samaki inauzwa ghali kiasi cha watu wengi wa kipato cha chini na kati kutomudu kuitumia kadiri wapendavyo. Na hiyo ni ishara yakuwa soko lake lipo ni kubwa.

KWA UJUMLA BISHARA YAKUZALISHA CHAKULA NI BISHARA AMBAYO SOKO LAKE LIPO SIKU ZOTE AU KAMA NI LAKUTAFUATA AU KULITENGENEZA NI RAHISI SANA SABABU MWANADAMU KABLA YA MAMBO MENGINE YOTE KULA NI SUALA LA LAZIMA ILI AWEZE KUISHI.


GHARAMA ZA KUANZA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KISASA



S/N

MAELEZO

KIASI

MARADI WA BWAWA 1

KIASI

MRADI WA MABWAWA 2

1

Ujenzi wa shamba kitalu (green house) la kufugia samaki na bwawa bora ndani yake,Malighafi zake zote zenye ubora unaoshauriwa na kampuni,gharama za ufundi na utaalamu wa teknologia hii, na ushauri wa kitaalam pamoja nakutembelewa mara moja kwa mwezi wa kwanza wa mradi kuanza.


1,193,700


2,048,700

2

Mbegu bora ya samaki aina ya kambale(Hybrid Catfish -mono sex)

1000

450,000

2,000

900,000

3

Chakula bora cha samaki


400,000



800,000



Jumla kuu gharama yakuanza mradi kisasa



2,043,700



3,748,700













S/N

MAUZO KADIRIWA/SALES FORECAST

KIASI

MARADI WA BWAWA 1

KIASI

MRADI WA MABWAWA 2

1

Mauzo kwa makisio ya bei chini Tshs 5,000/= kwa 1kg

1000

5,000,000

2000

10,000,000

Toa (-)






1

Ngarama za ulishaji hadi kuuza


(400,000)


(800,000)

2

Maji upatikanaji kama unalipia ya bomba makisio ya juu


(600,000)


(1,200,000)

3

Mbegu ya samaki


(400,000)


(800,000)

4

Dharura nyingine yeyote ile inayowezakujitokeza


(1,000,000)


(2,000,000)









FAIDA (BAADA YAKUTOA GHARAMA ZAUENDESHAJI)



2,600,000



5,200,000



ndo hawa? maelezo mazuuri kumbe ni matapeli asante ngoja nikamtie mabovu hukohuko kwenye kablog kake
 
Back
Top Bottom