Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,229
- 44,239
Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na ndugu yangu mmoja mitaa ya Aggrey tukitafuta simu aina ya galaxy Note 4 mpya, huwezi kuamini tulizunguka maduka yanaweza kufika hata 100 lakini hatukupata hata note 4 moja ambayo ni ya kimataifa (Africa pia) zote zilikuwa ni simu ambazo wamezitoa kwenye mitandao ya simu ya Kimarekani, Korea na China pamoja na nchi nyengine kubwa kubwa. Simu hizi nyingi zilikuwa zimelokiwa na jamaa wamezi unlock na pia ni mbaya kwa matumizi yetu ya kitanzania, leo hii nimeona niandike thread hii kuelezea madhara ya hizi simu na pia tuelezane njia za kupunguza hayo madhara kwa wenye nazo.
Hupati updates, warranty wala support yoyote
Unaponunua simu hizi usitegemee kupata updates badala yake ukitaka update inabidi udownload manual, vile vile hata kama simu ni mpya ikiharibika inabidi urudishe ilipotoka. mfano una galaxy s7 ya kikorea ukiwapelekea samsung Tanzania hawatakutengenezea sababu haiwahusu. Hata mwenye duka akikwambia anakupa warranty ni muongo tu labda airudishe alipoitoa kama atakua tayari.
Zinasumbua ussd
Umeshanunua simu ukaona ukiuliza salio *102# inakubali lakini mpesa, tigopesa na vyengine vinakataa? ukiona hivyo ujue tayari upo mkumbo huu umeuziwa simu za kikorea na wenzie
Muda wote zinaandika 4g au kutoshika kabisa 3g
Watu wengi hufikiri simu zao zina 4g kumbe hazina, mitandao mingi ya kimarekani na baadhi ya nchi wanaitwa hspa+ kama 4g kitu ambacho sio sahihi, hivyo simu hizo zikija hapa kwetu huandika 4g hata kama mtandao ni wa 3g, ukiona simu yako ipo hivi ujue umeshauziwa hizi simu, pia kuna mitandao kama T-mobile band yao ni 1700mhz hivyo simu zao zinaweza zisishike kabisa 3g huku kwetu
Simu za CDMA na band tofauti
Pia simu hizi zipo za CDMA zinaweza kuja Tanzania zisishike kabisa network ukapata pengine 4g tu, na hio 4g inaweza iwe ni band ambazo hazikubali kwetu, mtandao pekee wa Tanzania wenye band za kichina china ni smart band 2300mhz hivyo ukiwa na simu ya namna hii angalia mtandao wa smart.
Zinakuja bila google play store
Nchi kama China playstore kwao sio maarufu, hivyo simu zao zikija huku kwetu zinasumbua unakuta haina playstore wala app yoyote ya google hivyo kuanza kukuhangaisha kuweka hizo app sometime inabidi hadi uflash simu
SMA charachter sio 160
Kikawaida sms moja huwa na herufi 160 (pamoja na space na namba) lakini simu hizi huwa na herufi chini ya 160 hivyo utakatwa hela nyingi zaidi pamoja na kuharibu mfumo mzima wa kutumiwa mfano mtu akituma msg ya 160 kwako itakuwa kama msg 2. kwa wale wanaotuma msg ni muhimu hii.
mfano hii ina charachter 70 tu hivyo msg ya 160 itahesabika kama sms 3
Dialer ya kikorea au kichina
Pia inaweza tokea dialer (ya kupigia simu) ikawa mfumo wa kikorea
Support ndogo ya developers
Pia simu hizi huwa na custom rom chache au usipate kabisa, njia za kuroot wakati mwengine zinakuwa ngumu, nyengine zinalokiwa bootloader etc kama wewe ni power user simu hizi zinakuwa pasua kichwa.
Hayo ni baadhi ya madhara ya simu za kikorea, kama kuna mengine nimeyasahau mutaniambia.
Namna ya kujua kama simu ni ya kikorea au international
Kusema simu inaitwa lg g2 au galaxy s5 haitoshi kila simu inakuwa na model zake, simu moja kama galaxy s5 inaweza kuwa na model tofauti tofauti hata 10, hivyo kujua simu yako fanya hivi
-Nenda setting halafu about utaona model number ya simu
Ukiipata hio model number angalia online ni ya wapi, site kama gsmarena kwenye specs za simu hueka model na maeneo zinapotoka unatakiwa uwe na model international, au just google simu yako na neno international version kwa mbele, mfano galaxy s5 international version utapata model ya international kama huna hio ujue kuna uwezekano kupata madhara ya hapo juu
-Njia nyengine ni kuregister na warranty ya samsung sema njia hii ni kwa simu mpya zilizotoka chini ya miaka miwili iliopita.. utaandika neno REG*imei# halafu tuma kwenda 15685 utajibiwa, badili neno imei na imei halisi ya simu
jinsi ya kupunguza madhara ya simu za kichina
1.Badili app husika
Mfano dialer ina maneno ya kikorea nenda playstore install dialer nyengine tumia
2. Badili rom
Unaweza ukaeka custom rom kama cyanogen hii itasolve matatizo mengi tu
3. Mods mbali mbali
Kuna simu zinakubali kubadili bands zake na kueka bands za nchi yako, kuna mods za bootloader kwa wale ambao rom za international zinakataa etc
Una tatizo la simu za Kikorea? Usisite kulitaja hapo chini.