JIHADHARI NA MATAPELI PROMOTION YA tIGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JIHADHARI NA MATAPELI PROMOTION YA tIGO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ESCO, Feb 6, 2012.

 1. E

  ESCO Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Kuna utapeli mpya umezuka wakati huu wa Promotion za tIGO.
  Nimetumiwa sms toka +255652165304 inasomeka hivi " PATA OFA KABAMBE KUTOKA tiGO WEKA SH,5000 KATIKA AKAUNTI YAKO KISHA TUPIGIE SIMU NAMBA *101*652165304*4848#OK UTAKUWA NA SH,10000 PAPO HAPO tiGO"

  NIMEJARIBU NIKALIZWA , NAKATUMIWA UJUMBE TOKA 100, Sh 4848.00 imetumwa kwenda 652165304. Kisha matapeli wakinipigia simu na kuuliza kama nina salio na fedha kwenye tiGO PESA. Kisha wakazima simu. Nimewapigia tiGO customer care kwa namba 100 bila mafanikio. Nimejaribu kupiga jioni hii ile namba ya matapeli inaitwa bila majibu.

  NIMEANDIKA KUWATAHADHARISHA NA MSAADA WA KOMESHA UTAPELI HUU
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  pole sana!

  Tusipende vya bure! Vya bure gharama!
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Mimi ningekuwa hakimu ukiniletea malalamiko kama hayo nakuhukumu kuchapwa vikobo 12.... yes.... kwa ujinga uliopitiliza
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata mimi majuzi imeingia sms inasema "Tigo inakuarifu kwamba mtumiaji wa namba 657161354 amekutumia ujumbe. Andika OK kukubali kulipia gharama za ujumbe huu"
  Nikiangalia namba iliotuma ujumbe ni 25555740657161354, ambayo ni hii hii.
  Nikawaona ovyoooo wanadhani mie wa kuibiwa kijinga, nikawakumria mbali.
   
 5. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,724
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  kwa kweli kwanza ningeanza kukupa adhabu wewe.unatumia tigo halafu hujui no ya kuhamisha salio ni *101*? Ndio maana mmeambiwa na mwana Fa msije mjini.hii ndo bongo bana!
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,724
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Yaani huyu ni kilaza haswa,inaonekana akikutana na zile za wanaijeria kutoka yahoo, au window live atapagawa kabisa huyu akifikiri kashautoa umaskini. Acha ujinga wewe,no gain without pain.shtuka machale kundesa jamaa angu.
   
 7. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  hawa tigo sasa wataanza kula tigo
   
 8. BABU CHONDO

  BABU CHONDO JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  We ndo kilaza kweli.
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  In fwakt hata mie
  sijui hiyo process
  ya huhamisha hela
  Natumiaga ile
  ya huduma za tgo
  aisee

  ila hawa tigo
  hawapokeagi
  hiyo no ya
  customer care
  si waiondoe
  na watuambie
  hyo service
  is no more!
  Aghrrrr
   
 10. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Huu ni WIZI! Hiyo namba inaweza kuwa, ama imesajiliwa au la, haijasajiliwa. Jaribu bahati yako. Chukua ushahidi wako, nenda Polisi, lakini sidhani kama TiGo watakupa ushirikiano. Hawapendi kuhusishwa na utapeli unaotumika kupitia mtandao wao. Jibu? ISUSIENI TIGO! Kwani kuna ulazima wa kutumia mtandao huo wa MAFISADI? MUMEROGWA?


   
 11. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana mtu wangu! Hao jamaa walishanitumiaga msg kama hiyo takribani kama miezi miwili iliyopita. Ila niliwazidi ujanja zaidi hivyo hawakufanikiwa kabisa. Siku nyingine mkuu kuwa makini na vitu kama hivyo umefanya jambo la maana sana kuwajulisha wana jamii ili na wao wasije kuingia kwa huwo mtego.
   
 12. D

  Developer JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 285
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  halafu tuupe shavu mtandao gani usiokua wa mafisadi?
   
 13. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  kuna akina dada walimliza mwenye duka la boutique 682,000/-
  walifika dukani kwa kujiamini mashamsham kibaao.. Wakaanza kujaribu na kisha wakaomba wafungiwe mzigo wao,maana walikuwa wanawahi airport..

  Walichukua handbags,viatu pea kadhaa,na makorokoro mengine.. Baadaye wakamuuliza mwenye duka kama kajiunga na tiGO pesa,mwenye duka akasema hajajiunga,akamuuliza mfanyakazi wake,akasema kajiunga.

  Wale wadada wakaomba namba walipe pesa.. Huku wanapiga stori nyingi,na kusema wamepata duka lina collection kubwa,hawatashop maduka mengine..
  Mmojawao akamuuliza yule dada wa kazi kama hela imeingia,akajibu haijaingia bado..Basi akamwambia yule dada wa kazi pale dukani ampe simu yake kisha akaichezea kama dakika mbili,kisha akasema ujumbe si huo hapo hela imeingia tayari... Wale wakasoma ujumbe,na wakaagana..

  Baada ya muda kidogo waliamua kuangalia salio na kukuta hamna kitu! Wakaja kugundua kuwa wameibiwa! Je mwajua waliibiwaje? Ni kwamba mwizi yule alisave namba yake kwenye simu ya yule dada wa kazi pale dukani kwa jina la TIGO PESA. Kisha akatuma ujumbe kama unavyoandikwa na wenyewe wenye huduma kuwa UMEPOKEA Sh....

  Mpo hapo?
   
 14. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ingawa tangazo lao dada Shirima kupata mchumba kupitia facebook ni zuri sana...nimeliona kupitia TBC..
   
 15. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  la tiGO
   
 16. dwight

  dwight JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ha ha! Pole,kwani hukujua kuwa *101* ni namba ya kuhamisha salio?
  Shida ya kupenda mteremko!
   
 17. E

  ESCO Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Asante ndugu. Mtandao huu nautumia kama ziada tu (kupiga na kupokea simu tu) . Hivyo sikujua kuhamisha salio, na sasa najua.
  Hoja yangu kuwahadharisha na huyu Tapeli. Hii namba (0652165304) ninaipiga inaita bila kupokelewa (hata wewe jaribu). Huyu anaendelea na utapeli wake. Naomba mwenye namba ya watu wa customer care -tiGO wanipe. Nataka kutoa ushahidi ili tapeli huyu adhibitiwe. Asante
   
Loading...