Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 26,097
- 34,036
TIGO Tanzania ni kampuni kubwa ya simu na nimetumia huduma zenu kwa muda kiasi kabla ya hapo nimekuwa Active Customer wa Vodacom kwa miaka mingi.
Nimeamua kuhamia TIGO kwasababu namba kubwa ya watu ninaowasiliana nao kwasasa ni wa Tigo. Pamoja na kuvumilia kupata messages nyingi za advertisements za tigo kila mara, nimekuwa nikijiunga na bundle la mwezi mara chache lakini zaidi ni la wiki, yaani kila wiki najiunga na kifurushi na wanasema ukitaka kujua umebakiwa na kiasi gani cha data click *102*00# utaona.
Nimejaribu mwezi mzima sasa na pia nimewasiliana na namba zao za huduma kwa wateja 0714 100100, mpaka na kuwa tumia message za Whatsapp kama wanavyotangaza lakini HAWAFANYI CHOCHOTE zaidi ya kunipa matumaini kuwa ndani ya masaa 24 tatizo litakuwa limeisha lakini wapi.
PILI, kuna Utapeli ulifanyika ni mwezi mzima umepita sasa na niliripoti namba iliyofanya utapeli kutoka kwenye A/C ya benki lakini sipati feedback yoyote ile, na mbaya zaidi mwanzoni namba iliyofanya Utapeli ilikuwa imesajiliwa kabisa na nina majina kamili yaliyotumika katika usajili lakini baadae mhusika akaenda kufuta usajili ilihali nilisharipoti TIGO kupitia customer care wao.
Sanasana ujumbe wanaotuma ni kuripoti Utapeli kwenda 15040 na kuishia hapo.
Sasa najiuliza Efficiency ya kampuni kubwa kama Tigo iko wapi? Au kuna staff wa Tigo anaekula njama na Matapeli?