Jihadhari kukopesha ndugu fedha

Sikopeshi zaidi ya 20,000/=

Tena hapo lazima uifatilie haswa
 
Hapana mkuu nilikua nina laki 8 tu akanikopa laki 6 .mwingine akaja nikamkopesha laki 2 hivyo akiba yangu ikaisha na ndoto za kudunduliza 1M zikapotea.
 
Ni kweli mkuu tabia ya kukopesha sio nzuri hasa unapomkopesha mtu pesa nyingi kama 5M kuendelea.

Ukimdai sana na kutishia kumshtaki hakawii kukuendea kwa mganga na kukuondoa duniani.

Kuna bwana mmoja wa iringa aliwapatia wakulima wa tumbaku mtaji halafu wakivuna mazao wanamrudishia na riba. Ilipofika msimu wa mavuno baadhi ya wakulima wakagoma kurudisha na akaamua kuwashtaki mahakamani.

Haikupita wiki alianza kuugua ugonjwa wa ajabu hatimaye akafariki.
 
Wengine waaminifu... Mpe tu!!
Daah mkuu me sijui ntamuaminije maana jamaa alianza job mwezi uliopita ninapofanya, sasa sijazoeana naye kivile na sijui huko alikotoka yupoje, halafu kwenye job huwa jamaa ana tabia ya kuchomoka chomoka na siku nyingine haji tena hata taarifa hatoi! Sasa aliambia juzi hadi leo ananikomalia kama yake, kafuata wengine wakamtolea nje...
 
Nilimkopesha jirani yangu laki nne, akaahidi kulipa ndani ya mwezi mmoja. sas ni mwaka wa pili hajalipa. kweli mfadhili mbuzi, utakula mchuzi na sio binadamu maana wana maudhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…