Jihadhari kukopesha ndugu fedha

Jihadhari kukopesha ndugu fedha

Sikopeshi zaidi ya 20,000/=

Tena hapo lazima uifatilie haswa
 
Dah, Ni ndugu umemsaidia.... Potezea bwana.... Sio ndugu wote wako hivyo.... Mi mtu akichelewa nilipa lakini anaonyesha concern namwelewa, mambo yanakuwaga tight wakati mwingine tunasaidiana. Dah ulikuwa una 8m, hiyo laki Sita Ni Fanya Ni malumbuko ukilalama hivi utakosa pesa na baraka
Hapana mkuu nilikua nina laki 8 tu akanikopa laki 6 .mwingine akaja nikamkopesha laki 2 hivyo akiba yangu ikaisha na ndoto za kudunduliza 1M zikapotea.
 
Jamaa yangu alikwenda kudai pesa zake na hakupewa na aliporudi nyumbani akaugua ugwanjwa wa ajabu na akafa watu wakaseama amelogwa. Kuna mwandishi mmoja alikuwa anatafuta habari na akaenda kwa mganga kujifanya ana shida na akakutana na watu wamekuja kwa mganga kwa ajili ya kuloga watu waliowakopesha pesa zao. Nimeshawakopesha wengi na cha kusikitisha ni mmoja alikuwa akijiita mchungaji na ameishia na pesa zangu. Inakuwa vigumu saa nyingine kumnyima maana anakuwa ni rafiki yako lakini akishapata anaishia. Kwa ujumla ukikopesha jiambie mwenyewe umemsaidia.
Ni kweli mkuu tabia ya kukopesha sio nzuri hasa unapomkopesha mtu pesa nyingi kama 5M kuendelea.

Ukimdai sana na kutishia kumshtaki hakawii kukuendea kwa mganga na kukuondoa duniani.

Kuna bwana mmoja wa iringa aliwapatia wakulima wa tumbaku mtaji halafu wakivuna mazao wanamrudishia na riba. Ilipofika msimu wa mavuno baadhi ya wakulima wakagoma kurudisha na akaamua kuwashtaki mahakamani.

Haikupita wiki alianza kuugua ugonjwa wa ajabu hatimaye akafariki.
 
Wengine waaminifu... Mpe tu!!
Daah mkuu me sijui ntamuaminije maana jamaa alianza job mwezi uliopita ninapofanya, sasa sijazoeana naye kivile na sijui huko alikotoka yupoje, halafu kwenye job huwa jamaa ana tabia ya kuchomoka chomoka na siku nyingine haji tena hata taarifa hatoi! Sasa aliambia juzi hadi leo ananikomalia kama yake, kafuata wengine wakamtolea nje...
 
Nilimkopesha jirani yangu laki nne, akaahidi kulipa ndani ya mwezi mmoja. sas ni mwaka wa pili hajalipa. kweli mfadhili mbuzi, utakula mchuzi na sio binadamu maana wana maudhi
 
Back
Top Bottom