Tape measure
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,980
- 3,577
Habarini wanajukwaa natumaini mpo salama,
Najua wengi watajiuliza kwanini nasema ujihadhari kukopesha ndugu fedha! Wengine watahisi kuwa mimi nina roho mbaya na kuanza kunipa majina lukuki mara nitakua mangi, msambaa mpare na kadhalika.
Mpaka naandika huu uzi nimepitia mengi sana. Kwanza kabisa kuna siku rafiki yangu alikuja getto kwangu jioni na kunieleza kuwa amepata kazi katika ofisi mpya hivyo basi anaomba nimkopeshe Tsh 600,000. Ili aweze kuhama nyumbani kwa wazazi wake alipokua anaishi na kuweza kupangisha chumba maeneo jirani na sehemu ya kazi alikopata.Aliahidi mwisho wa mwezi angenirejeshea fedha zangu sikua na hiyana kwani zilikua zimebakia siku chache tu mwisho wa mwezi kufika.
Nilikua nina akiba ya Tsh 8,000,000. Nikampatia laki 6 akaanza maandalizi ya kuhama nyumbani. Mwezi ukaisha nikamuuliza vipi deni langu jamaa ananiambia nisubiri tarehe 15 ya mwezi mwingine atanipa, tarehe 15 nayo ikapita nikamuuliza tena ndugu vipi nahitaji 600,000 yangu nimekwama.
Jamaa akazidi kunipiga tarehe Mara nivumilie mwezi ujao nitakupa angalau nusu, nikaendelea kua mvumilivu Mara mwezi wa 3 ukaisha hela yangu sipewi nazidi kupewa story mpya kila kukichaa.
Ikafikia kipindi nikimpigia simu hapokei wala message hajibu, Mara aniambie nitakutumia siku fulani then siku hiyo ikifika anazima simu hata siku 2 mfululizo.
Ikawa mchezo ndio huo nikimfuata kwake basi ni story tu za matatizo ananisimulia yanii mpaka nikashindwa kumuelewa kwani inafika kipindi naona kama tunashindana kuelezeana shida kwani na mimi nilikua nina shida tena nyingi na kubwa kuliko yeye.
Kiukweli alinikwamisha sana kwani malengo yangu yalikua ni kudunduliza Tsh 1,000,000. Ili niweze kuanza kufanya biashara na ilikua imekasoro Tsh laki 2 tu malengo yangu yatimie.
Tukio jingine alikuja jamaa mmoja ambaye pia ni mpangaji wa nyumba tuliokua tunaishi, yeye alikua ni mtumishi wa serikali pia anajihusisha na kilimo, Hivyo aliniomba nimkopeshe Tsh laki 3 ili akanunue mbegu na kuahidi atanirejeshea mwisho wa mwezi. Nilimjibu hiko kiasi sina ila ninaweza kumkopesha laki 2, ambayo ndio ilibaki nilipomkopesha jamaa wa kwanza laki 6.
Sikua na wasiwasi naye kwani tupo nyumba 1. Mwisho wa mwezi ukafika deni langu hakunilipa. Mbaya zaidi huyu jamaa akaanza kuwa na life style ya tofauti yaani anadamka sa 11 asubuhi kwenda kazini na akawa anarud usiku mnene kusudi tu tusionane. Kiukweli nilishindwa kuelewa kuwa tatizo ni deni langu tu?? Kufua akawa anafua usiku asubuhi mnakuta kaanika nguo kwenye kamba.
Dunia ina mengi kwani nikawa naambiwa nikisafiri tu kwenda mikoani jamaa ndio huwa anaonekana nyumbani kwani ata siku za wkend ilikua haonekani na haikua kawaida yake, siku akirud sa 7 usiku ukimgongea mlango haitiki anajidai hakusikii.
Tisa kumi hii ndio ilikua kituko ambacho sitokaa nisahau kwani nilimuekea mtego. Hiyo siku nikaamua kukaa jikoni nimsubirie mpaka atakaporudi nimkamate anilipe pesa zangu.
Maajabu ya mtume ilipofika sa 5 usiku nikaona mtu anakuja kwa kunyata nikashtuka kulikoni huyu atakua ni kibaka ama! Alipokaribia karibu kumbe ndio yule mdeni wangu, nikaendelea kujibanza alipokua anakaribia kwa mlango wake ile anaanza kufungua tu kufuli la mlango wake basi nikatokea nikamwita kwa jina..mambo vipi jamaa kugeuka na kukuta ni mimi huwezi amini alifungua kufuli kwa kasi akaingia ndani upesi alafu akajifungia kumwita haitiki utazani kazimia nilitamani nikeshe mlangoni mpaka sa 11 amke nipambane naye nikaona mbu watanifaidi tu nitulize hasira nikalale yaishe.
Huu ni mwaka wa 3 sijalimpwa hata senti na wote 2 niliowakopesha. Ulifika pahali nikahisi ni majaribu kulikoni mtaji wangu umetoweka katika mazingira ya kutatanisha hivyo.
Nilichojifunza;
1. Kamwe usimkopeshe mtu fedha ambayo una mpango wa kuitumia hata kama ni miezi 3 baadae.
Yaani hata aje mtu akuambie ATM sijui Tigo pesa imegoma nitakurudishia baadae usimwamini kabisa ata kama ni boss wako.
2. Kutoa ni moyo sio utajiri lakini kamwe usimsaidie yeyote fedha yako uliotenga kwa ajili ya dharura ama matumizi mengine.
3. Kukopesha watu sio zambi lakini usijijengee tabia ya kukopesha watu fedha wakati mwingine deni lako laweza kuwa sababu tosha ya wewe kupoteza uhai wako.
4. Ni vema mtu anaetaka kukopa ukamwelekeza kwenye vikundi au mashirika yanayotoa mkopo kwa riba kuliko kumzamini wewe.
5. Kopesha mtu kiasi ambacho hata asipokirudisha hakitaweza kuharibu mipango yako ya maisha.
Nikikumbukaga huwa nacheka sana.