Jifunze zaidi kuhusu leseni/programu za bure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jifunze zaidi kuhusu leseni/programu za bure

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jul 9, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  JIFUNZE ZAIDI KUHUSU LESENI/PROGRAMU ZA BURE

  Inasemekana kwamba moja ya sababu ya Uhalifu wa Leseni za Programu haswa kwa nchi za dunia ya tatu ni Bei kubwa za programu kadhaa ambazo watu wengi wanapenda kutumia kwenye shuguli zao za kila siku na sababu nyingine ni uimara wa programu hizo zenye leseni za bure .

  Unatakiwa ujue kuna tofauti kubwa kati ya Programu ya bure ambayo unaweza kubadilisha baadhi ya vitu ili iweze kukidhi mahitaji yako na ile ya bure ambayo hutakiwi kubadilisha chochote zaidi ya kutumia tu kwa taarifa zaidi ya jinsi unavyoweza kutumia program hizi na leseni zake unatakiwa kusoma maelezo ya program hiyo au leseni yake .

  Napenda kuwajulisha watu kwamba hii sio sababu ya kweli kwa sababu ukiangalia bidhaa anazozalisha mtu huyo kwa kutumia leseni bandia za programu Fulani zina dhamani na gharama kubwa angepeza kununua leseni angekuwa salama zaidi kuliko ambapo angepoteza bidhaa hiyo kwa kutokuwa na leseni ambayo sio yake .

  Lakini pia kuna programu nyingi sana zenye leseni za bure ambazo unaweza kushusha kwa njia ya mtandao ukatumia kama zingine tu ila zinakosa baadhi ya vitu ingawa ila hilo halihusiani na programu zote kuna aina na aina tunaweza kuona chache hapa .

  Zipo programu zinazokupa muda wa siku 90 au 30 yaani unatakiwa uwe umenunua leseni yake ndani ya siku hizo ulizopewa , kuna ambazo hazikupi muda wa kikomo zaidi ya mwaka mmoja lakini hizi huwa zinakosa baadhi ya vitu lakini zinafanya kazi vizuri hazina usumbufu tembelea www.filehippo.com unaweza kuona aina mbalimbali za programu .

  Kwa wale ambao wako kwenye taasisi kama mashule wanatakiwa wajue kwamba kuna baadhi ya kampuni zinazotengeneza baadhi ya programu zinakuwa na mikataba na taasisi hizi kuhusu kutoa programu kwenye taasisi na shule hizi kama unatafuta programu na uko kwenye taasisi ni vizuri ukaangalia kwenye tovuti ya kampuni husika uone kuhusu mpango wao wa leseni kwa mashule , vyuo na sehemu zingine za elimu .

  Kama mtu ni mchoraji wa majengo na aina nyingine ya michoro anapofanya kazi yake moja anapata shilingi ngapi na programu hiyo bei yake ni shilingi ngapi ? hizo kazi huyo mtu anakuwa anafanya mara kwa mara kwa mwaka kama angekuwa na leseni yake sahihi anakuwa amepoteza nini ?

  Huyo mtu wa juu niliyemtaja hapo akiamua kutumia leseni bandia au ambayo sio yake ina maana kuna vitu anaweza kukosa kwa njia ya mtandao ambavyo vingeweza kufanya programu yake bora zaidi kwa kuongezewa pindi anapojiunga kwenye mtandao ( updates ) na kuna uwezekano mkubwa akashindwa kufanya kazi kwa ufasaha kutumia programu hiyo .

  Mtu huyo anapoamua kutumia leseni bandia au ambazo sio zake anatakiwa ajue leseni hizo na programu hiyo inatengenezwa na watu ambao wameajiriwa au wamejiajiri wenyewe na wanaotafuta maendeleo kama yeye anavyoyatafuta kwa njia ya kutengeneza programu hiyo .

  Huu utumiaji wa leseni bandia umechangia kwa kiasi kikubwa kwa maendeleo ya programu kwenye masuala ya kiulinzi kwa kiasi Fulani lakini kwa kiasi hicho hicho umesaidia katika kudidimiza baadhi ya kampuni au watu ambao waliwekeza kwenye sekta hiyo kwa kutumia gharama kubwa na kasha programu zao au leseni zao kuja kuibiwa haki zake kama hizo leseni , usisahau kupoteza nafasi nyingi sana za ajira kutokana na kushuka soko .

  Mfano mzuri uko hapa hapa nchini kwetu jinsi utumiaji wa leseni bandia unavyoathiri sekta kadhaa haswa hii ya teknohama , tunahitaji sana maendeleo ya watu wetu haswa wanaotengeneza programu hizo au wale wanaotakiwa kuja kuziendeleza mbeleni , ukiiba una nyima wengine fursa za kujiendelea , fursa za ajira , kodi na nyingine nyingi sana .


  Kwahiyo ndugu zangu tutumie nafasi tulizonazo katika kuelimisha umma kuhusu programu na leseni bandia tuhimize matumizi ya leseni halali haswa kwa njia ya kununua kwenye masoko ambayo yanaaminika au kutoka kwenye maduka au tovuti zinazoaminika lakini hii pia haimaanishi lazima uuziwe programu yenye leseni halali .

  Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu Programu/Leseni za Bure Tembelea

  www.gnu.org/philosophy/free-sw.html
  www.en.wikipedia.org/wiki/Free_software
  www.freeware.intrastar.net/education.htm
  www.download.cnet.com/windows/educational-software/
  www.yourchildlearns.com
  How educators and students can save on Microsoft software
  www.adobe.com/education/students/
  AutoDesSys | formZ
  Autodesk Education Community
  Free software movement - Wikipedia, the free encyclopedia


  YONA F MARO
  WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
   
Loading...