Jifunze mambo muhimu ya kuzingatia katika usalama wa barua pepe (Email)

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1598264394065.png


Maana ya Usalama wa Barua Pepe (Email Security)

Usalama wa Barua pepe ni hatua zote muhimu ambazo zinatumia kulinda mawasiliano na taarifa zinazokuja au kutumwa kutoka kwa Mtu mmoja hadi mwingine. Ulinzi huu unahakikisha hakuna Mtu asiyemlengwa au kuhusika / mdukuzi anayepata fursa au nafasi ya kuingilia mawasiliano ya barua pepe.

Baadhi ya hatua muhimu za ulinzi wa barua pepe ni pamoja na;
  • Chagua mtoa huduma anayetoa kipaumbele cha usalama kwenye barua pepe zake (Unashauriwa kutumia ProtonMail, Tutanota, Hushmail au Mailvelope kwenye Gmail)
  • Kuwa na Neno la Siri/Nywila (Password) imara
  • Kuhakikusha barua pepe imewezeshwa na mfumo wa Encryption
  • Lakini kifaa kinachotumika pia lazima kiwe salama (Kimewekewa Ant-Virus, Firewall)
  • Lakini lazima email iwe inaweza kuchuja maudhui na kutambua Spam Emails

1598264323067.png

Jifunze na uyaelewe baadhi ya mashambulizi yanayoweza kutekelezwa kwenye Barua pepe yako
  • Malware: kama vile virusi vya mtandaoni, minyoo wa mtandaoni, program za udukuzi. Hizi ni baadhi ya hatari zinazoweza kuingia kwenye kifaa cha mtumiaji na kuathiri usalama wa Email yake na mawasiliano yake kwa ujumla
  • Spam: Hii pia ni hatari nyingine na hasa pale ambapo mtoa huduma anapokuwa hajaweka hatua au chujio la kuchuja uhalali wa email zinazoingia. Spam inaweza kutumika kusambaza virusi kwenye email
  • Phishing: Hii ni hatari nyingine kwani mdukuzi hufanya uvuvi wa taarifa za siri za mtumiaji wa mtandao kwa kutumia ulaghai wa mtandaoni na wakati mwingine anaweza kuigiza kama anafahamiana vyema na mtumiaji wa Email
Hatua za usalama wa Barua pepe zinazopendekezwa na wataalam wa usalama wa kidigitali:

Password (Neno la siri / nywila): Unashauriwa kutumia neno la siri lililo imara zaidi na uliloliandaa kwa kufuata vigezo vyote (tumia herufi kubwa na ndogo, namba, alama, urefu wa hadi character 16 na zaidi, nk). Unapaswa kubadili neno la siri kila baada ya miezi 3 na uhakikishe linabaki kuwa siri.

Wezesha Two Factor Authentication au Multifactor Authentication kwenye email yako: Hii itakusaidia kujua kama kuna jaribio la kuingilia barua pepe yako. Ukitaka kuwezesha hii nenda kwenye mpangilio/settings kisha tafuta sehemu ya security utaona sehemu ya Two Factor Authentication au Multifactor Authentication.

Spam Filtering: Hii ni hatua muhimu kwasababu itakusaidia kujua kama kuna emails zisizostahili zilizotumwa kwako. Unashauriwa kutumia ProtonMail, Tutanota, Hushmail au kuweka mailvelope kwenye Gmail

Spyware Protection: Hii ni progamu maalumu itakayokusaidia kutambua kama kuna program hatari iliyotumwa kwako. Na itakusaidia kuidhibiti

Email Encryption: Huu ni mfumo wa usalama kwenye email utakaokusaidia kulinda email zako unapozituma na kuzipoke. Encryption inasaidia kuzuia mtu anayetaka kuingilia na kusoma kitu kinachotumwa kupitia email

NAOMBA TUSHIRIKISHANE YAFUATAYO;
  1. Ukiwa kama mtumiaji wa mawasiliano kwa njia ya email unafikiri ni njia gani nyingine unaweza kuitumia kuongeza ama kuimrisha ulinzi wa mawasiliano ya barua pepe?
  2. Je, kutokana na uzi hapo juu ni kitu gani unahitaji ufafanuzi wa kina?
 
Kwenye picha umezungumzia .bat files ambazo sidhani kama siku hizi wadau wanatengeneza...vingi vinakuwa embedded kwenye files tulizozea kama .pdf, .doc, .mp3 nk Je! Mtu anawezaje kujikinga na wadudu wa hivyo

Piani namna gani mtu anaweza kuverify addresses, ikiwa address nyingi zinakuwa shortened i.e kama zile wanazotumia watu kuziweka twitter, na kwa phish kubwa mtu ukigusa tu, taarifa zinakwenda ikiwemo IP address ambayo mtu anaweza kuifanyia port scanning na akaweza kucompromise system je na hapo inakuwaje
 
Asante kwa somo zuri. Kwa nyongeza tuu ni vizuri kila mtu anayetumia email akawa makini hasa kwa wale wenye emails za kampuni ambazo mara nyingi huwa zipo linked kwenye saver 1.

Tambua mtu 1 tuu anaweza kusababisha gharama au hasara kubwa kwa kampuni kupoteza taarifa au mambo ya siri kuvujishwa kwa wasio husika
 
Nashauri watu watumie kapsersky, hawa jamaa wapo vizuri mno.

Kuna kirusi kilishawahi kupiga ktk pc ya ofisini, nikahaha saaana.

Kirusi kila wakati kinawasha browserz, mafile ya microsoft office na nyimbo na video kikawa kimekata vyote.

Na hii ilitokea baada ya kuizima ili nidownload application.

Kile kirusi kilinisumbua mno, finally nikaiwasha kapsersky internet security.

Bhana weeee, ndani ya dakika kadhaa mwanaume akaondoa ule uchafu.

Toka ile siku mpaka sasa, japo sijatumia product zingine ila hawa jamaa naweza nikasema security ipo juu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom