Jifunze kupendwa ndani ya dakika chache

shadownet

Senior Member
Aug 4, 2015
133
1,000
Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na watu wengi, Watu hawa ndio mzizi wa hii dunia, Kutokuelewana / Kupuuzwa / kuchukiwa na watu ni kitu ambacho hakitakuletea faida maishani mwako, Kupendwa na watu ni moja kati ya vitu vinavyoweza kukufanya ujihisi faraja na kuishi bila hofu, Ukipendwa na mtu kwa dakika chache za kwanza mlizokutana basi kuna uwezekano mkawa marafiki, Wapenzi na hata kuwa best friends. Katika maada hii tutajifunza mambo ya kuzingatia ili tuweze kupendwa ndani ya dakika chache za mwanzo tunapokutana na watu.

JUANA NA WATU WENGI

Kama unajuana na watu wachache kusikufanye ujifungie kwenye hio circle, Ongeza networks kwa kujuana na watu zaidi, Jenga tabia ya kujuana na watu wapya, Watu wanaokutana na kujuana na watu wengi wanazungumziwa na watu wengi so unakua umejijengea kama umaarufu flani hivi kama wa msanii ambao utakusaidia kupendwa haraka maana kuna uwezekano mkubwa mtu ambae humjui tayari anakujua kwa vile unajuana na watu wengi.

SALAMU YAKO NDIO SILAHA KUU

Dakika zile za mwanzo unapotaka kutengeneza connection na mtu ni muhimu sana uziheshimu, Kutengeneza urafiki / Mapenzi huanza kabla hata hujafunua kinywa chako.

Vitu ambavyo vitainfluence wewe kuendwa ni kama Body language, macho yako na expression ya uso wako unapomkaribia mtu, Unapoonyesha interest ya kuwa interested na mtu Fulani jaribu kuposition mwili wako na moyo wako umlenge moja kwa moja mtu ambae upo interested nae, hii itakufanya uonekane ni mwaminifu na unajiamini, Kinachofata lengesha macho yako kwa muhusika na ndipo inapobidi utabasamu dizaini flani hivi kitu kitachomfanya mlengwa ajue automatically wewe ni sincere na muwazi.

Baada ya hapo mfate mlengwa na kitu cha kwanza ni kumoa salamu kama “Hi”, “mambo vp” katika tone nzuri na ikibidi ongezea na “Ninaitwa Fulani” ili na wao waweze kujitambulisha, Wakishajitambulisha hapo hapo na wewe dakia jina lao walilojitambulisha mfano””Oww , Agness nice to meet you” Ili waone wewe ni msikivu.

Hapo umefanikiwa kupendwa kwa asilimia 40 na kinachofata mfate karibu zaidi msalimie kwa mkono au kama ni sehemu za starehe mshike bega.

JARIBU KUWA NAO KITABIA NA KIMATENDO

Kila mtu anampenda mtu ambae kwa namna moja au nyingine wanafanana tabia au matendo, Katika dakika chache za mwanzo jaribu kuwa sambamba na mlengwa, Kama mlengwa naongea sauti ya chini nawe ongea kwa sauti ya chini, Kama mlengwa anafatilia habari nawe onyesha upo interested na habari, Badilisha tabia yako, expression ya uso na voice tone iendane na mlengwa, Kwa kufanya hivyo kutaleta natural connection.

USISIMAME KAMA MGOMBA UNAOONGEA, TUMIA BODY LANGUAGE,

Simama / kaa katika pozi ambalo linaonyesha wewe ni mkakamavu , Uso wako uonyeshe umechangamka, Macho yako yalenge kwa mlengwa, n.k. Katika body language zuia vitu kama kukunja mikono maana hii inainyesha kama hupo interested, Maneno unayoyanzungumza na body language yako hakikisha vinaendana.

ULIZA MASWALI ENDELEZI NA KUWA MSIKIVU

Usiulize maswali ambayo mtu anajibu ndio au hapana, Uliza maswali ambayo yanendeleza mazungumzo , Njia rahisi yah ii mbinu anza na neon kama Nani, Lini, Nini, Wapi, Inakuaje, Kwanini? Nakuhakikishia mazungumzo yatakuwa marefu, Hakikisha unakuwa msikivu kwa kile kinachozungumziwa, Mfano ongezea kauli kama “sawasawa”” ehee endelea” ili mlengwa ajue upi interested


MY OTHER POSTS

Funzo: Mapenzi imara yatakayodumu muda mrefu
Jifunze kupendwa ndani ya dakika chache
Jifunze mbinu za kujitegemea kiuchumi na kuwa tajiri
Jinsi ya kupata marafiki na kuwafanya wafanye unachotaka
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,102
2,000
Mkuu haya yanafanya kazi ktk jamii iliyojaa ustaarabu na imeelimika. Siyo hapa kwetu ambapo watu ni washamba na wajinga. Trust me hayafanyi kazi. Labda huko maeneo ya Posta Mpya Dar, kwa kuwa kuna ikulu
 

Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,921
2,000
Kunamtoto mmoja hapaofisini kanitupia tabasamu mpaka nikasisimka mwenyewe.

Ila yule atakuwani wale waliofundishwa maadili ya kuwa charming tu na si kitu kingine.

Namimi nina Bi. Zuhra.

Ingekuwa enzi zangu maneno mengine saa hizi.
 

lulu za uru

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
1,286
2,000
Wazungu ukikutana nao anakuchekea kidogo hata kama Kwenye daladala kitendo cha kukutanisha macho tu mzungu ana smile huku kwetu smile kwa mtu usiyemjua kiukwel utaonekana mwehu wa ukwl unaweza ukapewa makavu live wewe unanichekea mi shangazi yako!..
 

shadownet

Senior Member
Aug 4, 2015
133
1,000
Wazungu ukikutana nao anakuchekea kidogo hata kama Kwenye daladala kitendo cha kukutanisha macho tu mzungu ana smile huku kwetu smile kwa mtu usiyemjua kiukwel utaonekana mwehu wa ukwl unaweza ukapewa makavu live wewe unanichekea mi shangazi yako!..
Elekeza mwili na moyo wako wote, mlenge macho mlengwa (usimkazie sana), ukiona yupo vulnerable ndo utoe smile (sio kutabasamu kule kwa kukenua)
 

Neybright

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
5,673
2,000
Wazungu ukikutana nao anakuchekea kidogo hata kama Kwenye daladala kitendo cha kukutanisha macho tu mzungu ana smile huku kwetu smile kwa mtu usiyemjua kiukwel utaonekana mwehu wa ukwl unaweza ukapewa makavu live wewe unanichekea mi shangazi yako!..
 

cyrustheruler

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
2,049
2,000
f2fb18a48c8111921bd8cd493082f537.jpg
hivi vitabu ni vizuri sana ila hapa tandale haviapply kabisa they just don't work here.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom