Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,640
1. Epuka kununua vitu vya rejareja kwa "Mangi". Ukinunua nusu nusu kwa Mangi unauziwa bei ya juu japo utaona ni hela ndogo!
2. Weka daftari la matumizi nyumbani. Kila kinachotumika kiandikwe iwe ni pesa au kiasi cha unga, mchele kilichotumika: itasaidia kudhibiti matumizi
3. Dhibiti pesa za "chenji" zinazorudi dukani hasa sarafu kwa kuziweka mahali maalum. Hizi wengi "huzipotezea" na ukipata dada wa kazi mjanja, basi hizi hizi mpaka mwisho wa mwezi anajikuta amekusanya nusu ya mshahara wake bila wewe kujua!
Ndio unashangaa unakaa nae miaka na miaka, Wewe unajisifu "nimeishi nae mwaka wa 7 huu tunaishi kama ndugu"..lol ndugu my foot!! Ndugu zake wako kijijini huko, hapo yeye anapiga hela wewe kaa tu unashangaa shangaa, kashangae kigamboni daraja jipya ila wezi wa zamani!
4. Nunua mizani ndogo ya kupimia uzito(bei rahisi) ili kupimia vitu nyumbani.Kuna wakati unapika chakula kingi kwa kukosa kipimo sahihi
5. Kuwa mbunifu kwa kupendelea mapishi yanayobana matumizi mf: badala ya chips kuku, unaweza kupika viazi rosti utakuwa umefidia mafuta! utajiuliza ukipika rosti si nyanya, vitunguu vitahitajika? Hata chips kuku utahitaji tomato source/kachumbari
6. Usinunue soda, tengeneza juice "simpo" mfano juice ya ukwaju. Watu10 ukiwanunulia soda utakuwa umetumia gharama zaidi kuliko ukitengeneza juice ya ukwaju
7. Mgeni asikulazimishe uharibu bajeti yako, Usijivimbishe kiduva kama alama ya kuuliza kwa kuleta ufahari na kulijaza friji ndiii! yani mpaka mgeni akiondoka una madeni kwa mangi ya mishahara miwili! Simaanishi usimkirimu mgeni ila "cheza kwa step"
8. Usinunue maandazi au mkate kwa jirani, pika hata chapati za maji asubuhi,utabana matumizi kuliko kununua vitafunwa nje.
9. Usizoeshe watoto tabia ya kuwapa hela hovyo!Kuwa na utaratibu maalumu,sio huyu amekuja anasema umpe mia ya pipi huyu anataka miatano ya chip. Hata kama unazo jifunze kuwapa kwa utaratibu na hakikisha unaandika.
10.Kama nyumbani nyote mnaondoka asubuhi, mwambie dada wa kazi azime umeme na awashe tu pale anapohitaji!Mara nyingi kuna kuwa na "lose connections" ambazo wakati mwingine zinakula umeme bila kujua