Jifunze kubana matumizi nyumbani

Jifunze kubana matumizi nyumbani

1.Epuka kununua vitu vya rejareja kwa "Mangi".Ukinunua nusu nusu kwa Mangi unauziwa bei ya juu japo utaona ni hela ndogo!

2.Weka daftari la matumizi nyumbani📒. kila kinachotumika kiandikwe iwe ni pesa au kiasi cha unga, mchele kilichotumika: itasaidia kudhibiti matumizi

3.Dhibiti pesa za "chenji" zinazorudi dukani hasa sarafu kwa kuziweka mahali maalum.Hizi wengi "huzipotezea" na ukipata dada wa kazi mjanja😜 basi hizi hizi mpaka mwisho wa mwezi anajikuta amekusanya nusu ya mshahara 💰wake bila wewe kujua! Ndio unashangaa😳 unakaa nae miaka na miaka,Wewe unajisifu"nimeishi nae mwaka wa 7 huu,tunaishi kama ndugu👩‍❤‍👩"..lol ndugu my foot😏!! ndugu zake wako kijijini huko, hapo yeye anapiga hela wewe kaa tu unashangaa shangaa, kashangae kigamboni daraja jipya ila wezi wa zamani!

4.Nunua mizani ndogo⚖ ya kupimia uzito(bei rahisi) ili kupimia vitu nyumbani.Kuna wakati unapika chakula kingi kwa kukosa kipimo sahihi

5.Kuwa mbunifu kwa kupendelea mapishi yanayobana matumizi mf: badala ya chips kuku🍟🍗, unaweza kupika viazi rosti, utakuwa umefidia mafuta! utajiuliza ukipika rosti si nyanya, vitunguu vitahitajika? hata chips kuku utahitaji tomato source/kachumbari

6.Usinunue soda🍾, tengeneza juice "simpo" mfano juice ya ukwaju🍹. Watu10 ukiwanunulia soda utakuwa umetumia gharama zaidi kuliko ukitengeneza juice ya ukwaju

7.Mgeni asikulazimishe uharibu bajeti yako, Usijivimbishe kiduva kama alama ya kuuliza kwa kuleta ufahari na kulijaza friji ndiii! yani mpaka mgeni akiondoka una madeni kwa mangi ya mishahara miwili😳!.Simaanishi usimkirimu mgeni ila "cheza kwa step"

8.Usinunue maandazi au mkate🍞 kwa jirani, pika hata chapati za maji asubuhi,utabana matumizi kuliko kununua vitafunwa nje.

9.Usizoeshe watoto tabia ya kuwapa hela hovyo!Kuwa na utaratibu maalumu,sio huyu amekuja anasema umpe mia ya pipi huyu anataka miatano ya chips🍟..Hata kama unazo jifunze kuwapa kwa utaratibu na hakikisha unaandika✍.

10.Kama nyumbani nyote mnaondoka asubuhi🚗,mwambie dada wa kazi azime umeme💡 na awashe tu pale anapohitaji!Mara nyingi kuna kuwa na "lose connections" ambazo wakati mwingine zinakula umeme bila kujua
Ubarikiwe mkuu, namba 3 ina nihusu
 
Kama siyo uchoyo basi tuna haki ya kununua grisi ya kurainisha vyuma.
....
2.Weka daftari la matumizi nyumbani📒. kila kinachotumika kiandikwe iwe ni pesa au kiasi cha unga, mchele kilichotumika: itasaidia kudhibiti matumizi
Mzani home haki ya nani...
4.Nunua mizani ndogo⚖ ya kupimia uzito(bei rahisi) ili kupimia vitu nyumbani.Kuna wakati unapika chakula kingi kwa kukosa kipimo sahihi
Waafrika wengi kula (mfano) kiporo cha ubwabwa ni haki yetu, sasa upike ubwabwa kwa kipimo 😂 hahaaaa...
 
Mzee haya Mambo sioni umuhimu...wewe tafta pesa, miliki pesa hizo zingine ni uoga wa maisha
Hapana, unakosea, mimi nadhani Utofauti wa mtu mmoja na mwingine haupo kwenye kipato, bali unatokana na matumizi ya hicho kipato. Hapa namaanisha, kama wapo watu 2, wote wanapata kipato kinachofanana, ila wanatofautiana kwenye matumizi yao, ndani ya kipindi kirefu kutakua kuna utofauti wa maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, unakosea, mimi nadhani Utofauti wa mtu mmoja na mwingine haupo kwenye kipato, bali unatokana na matumizi ya hicho kipato. Hapa namaanisha, kama wapo watu 2, wote wanapata kipato kinachofanana, ila wanatofautiana kwenye matumizi yao, ndani ya kipindi kirefu kutakua kuna utofauti wa maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo zinafaa kwa waoga wa maisha.Sijawahi na Wala sitakaa nifikirie kuzitumia.. natumia pesa kila panapohitajika na nazitafta but still nimefanya maendeleo makubwa tu
 
Hayo siyo maisha ni upumbavu.

Jiue tu kama vipi ili upunguze kabisa matumizi usiwepo.
 
Mtu katoa ushauri mzuri watu wanajibu upuuzi,kua na kabajaji sijui kaduka hayo sio maendeleo ni uganga njaa maana wiki tu ukiugua kila kitu kinaporomoka kiss wewe ndo boss ndio mfanyakazi
Inamaana Kuna watu wako radhi kumwaga chakula au kipolo daily kisa wanatafuta pesa wenyewe,nidhamu ya kila kitu ni muhimu maana inatukumbusha kua na kiasi na utaratibu kwenye maisha Kama tu dini zinavyosema
 
Ukitaka laana ya maisha anza kujihesabia au kuwahesabia familia yako matumizi haswa yanayoingia tumboni ni laana unaikaribisha ndiyo maana muda mwengine mungu huleta baraka kwenye familia mtaona mnakula mnatumia nyumbani ukikaa kufikri unaona siyo uhalisia wako wa mshahara au kipato chengine ni baraka.
Naomba nishauri wazungu ndiyo waenye kuweka madaftari nyumbani na kuhesabiana ndiyo sababu ya wingi wao kiwa na roho ya ubinafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bandiko zuri sana.haijalishi wangapi wanakushambulia in negative way matumizi yangu binafsi plus na kodi ya mezani ninaandika tena ni kwenye sim yangu.km kuna atakaekuona Bahiri sio neno.
Pesa lazima uiwekee nidham Sana kwa kupunguza kama si kuacha matumizi yasiyo na ulazima,mfano mm niliamua kuacha sigara na Mambo mengine ikiwa ni moja ya kubana matumizi.
kma unabana hakikisha unabana sana mpka watu wako wa karibu watoe mlio
 
mi naziachaga makusudu dada wa kazi atumie...hizo chenchi ndogo ndogo.waanasaidia sana hawa madada kuliko hata ndugu
 
Back
Top Bottom