Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 466
- 1,209
1.Kila zama huja na jambo lake lepesi usipolifanya basi kesho utalifanya likiwa ghari zaidi.
2.Bahati inaweza kurudi mara ya pili lakini inaweza kukuta haupo kwenye mazingira rahisi kama ulivyoipoteza awali hivyo utagharamika.
3.Usiamue kufuata mihemko ya wengine kwa sababu matokeo kila mmoja atayabeba peke yake.
4.Nyuma ya mtindo wa maisha ya mtu kuna mengi huyajui hivyo acha tabia za kuiga.
5.Wengi wanataka uamue maamuzi ambayo yatawafurahisha wao hata kama kwako yatakuumiza hilo hawatajali hivyo kuwa makini.
6.Kuwahi kupo na kuchelewa kupo hivyo sio mbaya kujua upo upande upi ili ujue namna gani uchukue hatua.
7.Usiwe mtu wa kujifariji sana kwa sababu utafunga mlango wa kuchunguza wapi ulikosea, utajiona sahihi mpaka kwenye makosa yako.
8.Unayemuona hafai wewe kuna sehemu atafaa hivyo ukifanya maamuzi ya kumkataa usimshindikize kwa MATUSI NA DHARAU.
9.Kama sio dharura basi jipe muda kabla ya kuamua.
1.Punguza washauri ila katika kupunguza usiwatoe wale wanaokwambia ukweli
#Mwanasayansi Saul Kalivubha
#Fikia Ndoto Zako