Jicho Langu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jicho Langu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by vivian, Jan 25, 2012.

 1. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Asalamu Aleikum JF Members,

  Nafikiri nianze nakuwatakia Heri ya Mwaka mpya, Bado ni January na Bado tunatakiana Heri.

  Jicho langu linaangazia Tanzania na Ukimwi, ninajiuliza Mengi sana kuhusu Takwimu za Maambukizo ya Virusi vya Ukimwi Tanzania.

  Nina imani wengi wetu ni waadhirika wasiojijua! kwa maana nyingine tumeambukizwa virusi vya Ukimwi lakini hatujijui kwasababu bado hatujapima Afya zetu.

  Hii ni moja ya sababu kubwa ya ongezeko la maambukizi ya Ugonjwa huu. Ninaamini wengi wetu tungekua na ujasiri wa kupima na kujua afya zetu tungechukua tahadhari,

  Kwasababu mimi Vivian nilitembea na Invisble, na tayari invisible wameshaanza kumsema mtaani kuwa ni muadhirika, moja kwa moja na mimi najichukulia tayari ni Muadhirika, na kwasababu nina roho mbaya ninaamua kuondoka na watu pia. sitaki kufa peke yangu. atakayejipendekeza shauri yake, swala la condom ni yeye mwenyewe. akiwa nayo poa. asipokua nayo poa.

  This will finish Us!!!!.

  Kwanini m2 akijulikana ni muathirika anaonekana kama hastahili kuwa katika Jamii husika? amini msiamini muadhirika wa ukimwi katika Jamii ya kitanzania ni sawa na mtuhumiwa wa mauwaji. - kuna anayebisha hili?

  Tufanyeje??????
  Tupigane na ufisadi!!!

  Kama sio ufisadi, Tanzania ni moja ya Nchi Tajiri Africa. kwasababu ya Ufisadi Tanzania ipo kumi bora ya nchi maskini Africa.

  Kama Tungeweza kutumia rasilimali zetu katiaka njia isiyo ya kifisadi, Tungeweza kuwasaidia na kuwawezesha waathirika wa ukimwi.

  hivi ingekuwaje kama Serikali ingetoa incentives kwa watu ili wapime afya zao kwa hiari? na wakigundulika ni waathirika wakasaidiwa kwa namna fulani.

  Can we just Check what is SA doing about this?.
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Wasaidiwe vipi? allready mtu una ngwengwe hivi unafikiria serikali au jamii itakusaidiaje wewe ukiwa na ngoma? usiniambia masuala ya ushauri pls
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Vivian

  Kwanza nikurekebishe kidogo, ni muathirika na sio muadhirika. 'Athiririka' inatokana na neno 'athiri' linalomaanisha 'affect' kwa Kiingereza na neno 'adhirika' linatokana na neno 'adhiri' yaani 'kuaibisha' au kwa Kiingereza linaweza kuwa na maana sawa na 'to put to shame'

  Tukirudi kwenye mada, kupima afya ni jambo zuri lakini nadhani isiwe tu kwa ajili ya kupima VVU au UKIMWI.

  Nadhani ingekuwa jambo la msingi iwapo makampuni binafsi na ya serikali yangekuwa na sera ya msingi ya kupima afya ya wafanyakazi wao kila baada ya miezi sita, au mwaka mmoja. Na majibu ya VVU/UKIMWI upewe ukiyataka kwa khairi tu, japo kuwa utapimwa. Hii inafanyika kikawaida katika baadhi ya nchi za nje

  Itasaidia watu kuwa na afya njema kiujuma
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 180
  Vivian tatizo kubwa saana katika hili janga la Ukimwi ni Kila Mwadamu kujiona yupo Unique kana kwamba yeye Ungonjwa hauwezi mpata (ha hali anajihusisha na Sex); Kwa wale ambao wanaamini wanaweza kupata (ama wamesha pata) majority hua na Elimu ndogo saana kuhusu Ugonjwa. Naamini kua wengi twaogopa kifo saa ingine kuliko hata Ukimwi/Virusi vya Ukimwi.

  Na wengi saana wakisikia kua mwenye HIV anaweza ishi kwa mda mrefu – uhisi tu kua ni maneno ya Matumaini. Wanakua hawatambui kua ukiwa na HIV na ukaishi kwa vigezo na masharti you can live for a very long time. Hio inapelekea majority kuendelea kujihusisha na ngono isio salama na inevitable kusababisha hata alie kua anajihisi tu (na hana) aambukizwe, AMA yule ambae aliathirika kwa virus vya viwango vya chini viongezeke hadi a Critical Level....

  However nipo really interested as to why umegusia kua SA wanafanya nini....
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Vivian watu kupima huu ugonjwa imekuwa kama kuwapa hukumu ya Kifo..
  Sijui ni Elimu gani kwanza itumike ili kuwaconvice watu wajitokeze kwa wingi kupima afya.
   
 6. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,791
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Huwa wanatoa fulana FL1
   
 7. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dada Hongera kwanza kwa kuandika ujumbe mzito, lakini turekibishane kwenye mambo yafuatayo!


  Sentensi yako hapo juu na yenyewe ni sehemu ya kunyanyapaa. Kwanini, swala la kujikinga na maambukizi wapewe waathirika tu? Ama kwanini unadhani waathirika wote wanamalengo ya kuambukiza watu kwa makusudi tu! Yawezekana wapo lakini sio wote. Cha kukumbuka ni kitu kimoja tu - ukiwa na vijidudu/ukimwi sio kwamba matamanio ya mwili yanatokomea, la hasha, pia inajulikana ukijitangaza unatengwa - na basi kama ukibahatisha upate muathirika mwenzako! Sasa, Kijana mwenye miaka 30 kwanini abebe mzigo huo katika jamii ambayo haijali kujitokeza kwake? Kwahiyo, jukumu la kujilinda ni la wote - na haswa ambao sio waathirika kuelewa.

  Pia kunamifano mizuri ya waathirika ambao wamejitangaza na wanaendesha maisha yao kwa uwazi na makini sana. Pia lazima ujue, nijitangaze kwa nani? kwa faida ya nani? na wakati gani!
   
 8. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Tufanyeje??????
  Tupigane na ufisadi!!!

  Kama sio ufisadi, Tanzania ni moja ya Nchi Tajiri Africa. kwasababu ya Ufisadi Tanzania ipo kumi bora ya nchi maskini Africa.

  Kama Tungeweza kutumia rasilimali zetu katiaka njia isiyo ya kifisadi, Tungeweza kuwasaidia na kuwawezesha waathirika wa ukimwi.

  hivi ingekuwaje kama Serikali ingetoa incentives kwa watu ili wapime afya zao kwa hiari? na wakigundulika ni waathirika wakasaidiwa kwa namna fulani.

  Can we just Check what is SA doing about this?.[/QUOTE

  Inabidi tufikie mahali sasa tuache au tupunguze kuilaumu serikali yetu badala yake tujaribu kuwa wawazi kwa hatua iliyofikia na tuishauri jinsi ya kuboresha hicho ilichoanzaisha,
  Kwa nini nasema hivi :
  Nafahamu kabisa serikali kuna hatua imechukua katika suala hili la gonjwa la ukimwai ikiwa ni kwa ushirikiano wa mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi mbalimabali wamekuwa wakijitolea sana kuakisha kwanza huduma ya upimaji wa VVU iantolewa bure na hilo kweli wamejitahidi.
  Pili serikali pamoja na nchi rafiki pamoja na mashirika ya kidini yamekuwa yakijitahidi sana kuhakikisha afya ya waathirika ianangaliwa ikiwa ni pamoja na kuwapa dawa za kupunguza makali na pamoja vyakula vya kumsaidia muwathirika japo huduma hii imekuwa ikipigiwa makelele sana kwamba kumekuwa na upendeleo katika kupata huduma hii lakini serikali imejatahidi kwa kiasi fulani.
   
 9. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Yo yo! wewe ni mtoto mtukutu sana. why?
   
 10. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Umenena.

  kwanini Vivian aonekane kama kinyesi katika jamii kisa ana ukimwi?

  Hapa hatuilamu serikali. tunatoa maoni tu.

  Sipendi kuilamu serikali ya Jakaya, ila nitashauri pale inapobidi.

  Swala la upimaji wa VVU Tanzania Badooo!! takwimu zote ni Zero
   
 11. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kijitangaza?

  sipo tayari kutengwa na Jamii.
   
 12. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  we are now speaking the same Language.
   
 13. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Siz,

  SA. watu wanajitangaza coz kuna incentives.

  Tanzania Kungekua na Incetives Vivian angekua amejitangaza. Hapa Ifunda wasingekua wanapagawa naye tena. wangechukua tahadhari.

  Leo Vivian akijitangaza maisha yake Kwishen, vijiwe vyote ni story ya Ukimwi wa Vivian
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tanzania imekuwa ina-rely kwenye counselling practice only, i.e kubadilishana mawazo ya matumaini na wagongwa walio na cronic desease alone is not enough to convice them. Tunatakiwa kuimarisha au kuanzisha Palliative care services ili kuhakikisha kuwa wanaopima na kukutwa na incurable desease kuwa watapata huduma bora mpaka maisha yao yatakapofikia kikomo. Ila huduma bora maana yake ni gharama, na gharama maana yake ni uchumi kuwa unawezesha serikali kukusanya mapato ya kugharamia huduma hizo via tax.

  Kinachoiua Tanzania ni uongozi mbovu usio na kipaumbele na wenye kuangalia masilahi binafsi zaidi ya yale ya nchi. Watu hawagombei uongozi kuacha legacy bali wanagombea uongozi kuliibia Taifa na kujitajirisha wenyewe.

  Chanzo cha yote haya ni Uongozi, kama serikali inashindwa kujua kuwa madaktari ni muhimu zaidi ya wanasiasa basi hapo kuna tatizo la ubinafsi, na tutaendelea kufa kwa magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika. Tokea tumeanza chaguzi za vyama vingi ni nadra sana kusikia watu wakiweka kipaumbele katika sekta ya afya. Tumekuwa brainstormed kiasi kwamba kila kitu tunaishia kusema 'Kazi ya mungu'.
   
 15. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Need I say more?
   
 16. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Dah, niliovyosoma Title ya Thread, Jicho langu nikajua Jicho lile "jicho"
   
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,651
  Trophy Points: 280
  Ugonjwa huu ni wa "kiakili" zaidi,ni kweli unasambaa kwa ngono?Aliekua raisi wa africa ya kusini Thabo Mbeki aliwahi kukana kuwa virus wa HI haviambukizwi kwa ngono!**** raia mmoja wa venezuela aliwahi kusema alipona Ukimwi baada ya kuishinda akili yake!Hii maana yake nini?
   
 18. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kesho nitapima.
   
 19. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  basi tuanze kufight against stigmatisation kwanza then mapambano yaendelee.
  huu ugonjwa ukijua kama unao ndio unakumaliza kbs yan, bora kutojijua pia unless tuwe assured kuwa unyanyapaa utatokomezwa kidogo kunaweza kumotivate watu.
  kutengwa mama ni soo yan hapo tuu.
   
 20. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ujumbe umefika- Tatizo ukigundulika una Ukimwi unaonekana kama Muuwaji fulani hivi
   
Loading...