Jicho langu la tatu na biashara ya bodaboda

Jicho langu la tatu na biashara ya bodaboda

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
Hivi karibuni nilipata safari za kutembelea mikoa tofauti tofauti hapa nchini Tanzania, lakini pia nilipata fursa ya kubadilishana mawazo na watu wa kada na makundi mbalimbali, usafiri wangu wa kuniwahisha mahali mara nyingi nilitumia pikipiki ama jina maarufu boda boda, kitu kilichonifikirisha sana ilikuwa mawazo na mlengo wa taifa huko mbele miaka 15 hadi 20 ijayo, taifa tutakuwa wapi?

Biashara ya boda boda imekuwa mkombozi wa vijana wengi kwa sasa na imekuwa ni kama mtu akipunguza machaguzi kwenye maisha anatafuta boda anakuwa dreva boda na anaendelea na maisha, lakini nilichogundua boda boda ni mradi unao ua ubunifu na mipango ya maisha ya vijana wengi kwa sasa, vijana wengi wanaoendesha boda boda malengo yao yameishia kwenye bodaboda na hesabu zake. Ndoto zao nyingi zinakufa kwa sababu tu anaendesha bodaboda na inamruhusu kupata Tshs 5000 - 10,000/= ya kwake kwa sikuu basi anakuwa anabweteka na pia inakuwa rahisi sana kwake.

Asilimia kubwa ya wanaoendesha bodaboda ndoto zao hazikuwa kuendesha bodaboda lakini baada ya kupata upenyo mwepesi wa kuendesha maisha wanaua ndoto zao na kupambana na huu upenyo, nikapata swali kwa sasa nchi nzima biashara ya boda imeshamiri na inakuwa kwa kasi, kama nchi tunamipango ya kuendelea kuwa kwenye uchumi wa kati lakini kujivuta hadi uchumi wa juu hii lazima iende na nguvu kazi pamoja na kujituma, lakini hata mipango ya familia ni kuongeza kipato na kuwa kipato kilichosimama, sasa nikajiuliza kwa asili na muonekano wa biashara hii ya bodaboda baada ya miaka 15 au 20 nchi itakuwa wapi? iwapo biashara ya boda boda ikiendelea kuwa ndio kimbilio la vijana wakichelewa kupata ajira?

Sitaki kugusia sana kuhusu matendo na tabia zinazoonyeshwa na madreva boda, ambazo zinachangiwa na umri wao, mazingira na elimu duni ya matumizi ya fedha na mkumbo wa eneo ila nnachokiwazia ni tukiendelea kuua malengo na ndoto nyingi kila mwaka kwa kisingizio cha ajira kuwa ngumu ama kuchelewa tutakuwa na taifa gani miaka 20 ijayo na je, hizo ndoto zilizokufa nani atakuja kuzifanyia kazi? ama tunaawachia wageni ndio wazifanye na kisha wazawa tubaki tunawahudumia wageni kwa kazi zao?

Hili jambo limeniwazisha mambo mengi sana kwa mustakabali wa nchi na familia kwa ujumla, tunahitaji kubadilisha mawazo na fikra kuhusu biashara hii ni kweli inatusaidia kuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa haraka lakini tunapoteza nguvu kazi kubwa ambayo tunaihitaji kama taifa na familia, kutimiza malengo makubwa ukiwa na biashara ya bodaboda sio suala dogo lakini waajiriwa wake ndio nguvu kazi ya leo na kesho?

Bodaboda ni Dream killer ambae anaonekana mkombozi kwa sasa. Tuamke, njia bora nadhani hawa vijana waanze kupokea mafunzo ya kujitambua kabla ya kupewa hizi bodaboda ili tuanze kubadilisha vituo vya boda kutoka kuwa genge hadi kuwa VTC vijana wawe na uongozi ambao utasimamia mienendo na afya za akili zao ikiwa inamaanisha kuwa na semina na warsha za madreva boda nyingi za kuwajenga kihisia na akili ili wajitambue nafasi zao na uhusika wao kwenye jamii na familia kwa ujumla isiwe tu kwa sababu ya kukosa ajira bali iwe ni daraja la kijana na ndoto zake.

Elisha Chuma.
 
Una point ila ukumbuke hamna mtu anayependa kufanya kazi ambayo hakuwahi kuifikiria au kazi za mediocres wengi.

Ila kwa hali ya maisha ilivyo,na mfumo ambao vijana wengi tumekuzwa nao kwamba baada ya graduation ni kazi na kununua gari,kujenga na kuoa,,, itokee huna sh.10 mfukoni matatizo yatakayokupata ni makubwa kuliko ungeendesha hio boda boda ukawa na uhakika wa elfu 10 mpaka 15 kwa siku.

Hutakaa upate furaha katika maisha kabisa, utaachwa na mchumba, utatengwa na ndugu na jamaa ambao wana kazi zao na wanajikidhi. Watu tunaamua ku sacrifice tu sasa maana hata ukisema usiendeshe utafanya biashara kwa mtaji upi?

Biashara ya usafirishaji ni quick solution maana hamna gharama za promotion wala unaweza usiwe unamiliki hio pikipiki na ukapata zako hela freshi tu.
 
Bodaboda ni shughuli kama shughuli zingine ili mradi ni halali. Kusema kuwa ni dream-killer ni mtazamo hafifu maana kuna vijana wanatembea mjini na masters zao kwenye bahasha hata hiyo 10,000 kwa siku hawapati!
Jamaa anaongea kirahisi tu. Maisha yamekuwa magumu sana mkuu yani usiombe ukose shughuli yeyote rasmi ya kufanya mjini.

Graduates wasio na ajira ama wale waliowahi kufukuzwa kazi ghafla wakaonja utamu wa kushindwa kutimiza majukumu ya mjengoni baada ya hela zote kukata ndio wataelewa uzito wa kazi yeyote inayoweza kukupa hata 10K tu kwa siku! Hata ikiwa kuzoa mavi ilimradi inaingiza pesa.

Kuna nyimbo moja ya Zilipendwa sijui ni ya somebody Daudi kabaka inaimbwa:
"Ikiwa kama wewee ni kijanaa, ukikosa kazi tabu nyingi utazipata"
 
Absolutely mkuu. Mimi nafahamu vijana kama wawili ni mawakili kabisa Ila wameikosa kazi wanauza mitumba kwa whatsapp.. mwingine ni wakili Ila anaendesha Uber!

Wote hawa ukiwahoji wanakuambia taaluma zao haziwalipi ndo maana wanahustle kivyovyote vile ili mradi pesa ipatikane!

Mleta mada ana mshahara Kila mwezi hawazi chochote halafu anawaona vijana wa bodaboda wajinga huku yeye mwenyewe akitumia usafiri huo huo!

Hawa ndo "kigwangalla-type" wao wenyewe wameajiriwa halafu wanaambia vijana wajiajiri bila kufafanua wajiajiri vipi!
 
Jamaa anaongea kirahisi tu...Maisha yamekuwa magumu sana mkuu yani usiombe ukose shughuli yeyote rasmi ya kufanya mjini.

Graduates wasio na ajira ama wale waliowahi kufukuzwa kazi ghafla wakaonja utamu wa kushindwa kutimiza majukumu ya mjengoni baada ya hela zote kukata ndio wataelewa uzito wa kazi yeyote inayoweza kukupa hata 10K tu kwa siku! Hata ikiwa kuzoa mavi ilimradi inaingiza pesa.

Kuna nyimbo moja ya Zilipendwa sijui ni ya somebody Daudi kabaka inaimbwa:
"Ikiwa kama wewee ni kijanaa, ukikosa kazi tabu nyingi utazipata"
Ukitaka kujua msingi wa tatizo lenyewe anzia hapa:

- Soma sheria ya kodi na ya makampuni.

-- Angalia sera ya nchi kuhusu vijana na mahitaji kama ajira, mikopo

- Angalia namna nchi unavyotreat sekta binafsi.
- Angalia hata uanzishaji wa vitu vidogo tu kama Drones, youtube channel na blogs unavyokumbana na vikwazo.
- Then, njoo hapa:
+ Tanzania ina almost watu 60M.
+ Serikali imeajiri watu Laki 5 tu.
( Na bad enough imeshindwa kuwahudumia, wengi wana maisha magumu mno )
+ Maana yake watu wengine kila mmoja anajijua, bodaboda, vibanda barabarani, machinga etc
+ Na wakati huo huo watu wanahamasishwa kufyatuaaa

- Anyway sekta binafsi lia inapigwa vita: Ukianzisha biashara, unakutana na serikali yenyewe sokoni kupitia TANCOL, SUMA JKT, ATCK, ATCL, n.k

Yaani sijui unaelewa?

Okay, soma stori fupi:

Unamaliza chuo ukiwa na miaka 21 huku ukiwa na deni kama 10M la Loan board, ajira hakuna na deni linakuwa kwa 6% kila mwaka

Ukatafuta kikazi Fast Jet, mara ikapigwa vita ikafa mafao yako kupata NSSSF moaka ufikishe miaja 55.

Sasa unataka vijana waishi vipi ?
 
Mkuu mfumo wetu wa serikali dhidi ya uwekezaji uko complicated un-neccessarily tu!

Sometimes nawaza hata mtoto wangu akimaliza O-Level nimu enroll kwenye utafutaji mali tu ili akifika utu uzima awe tajiri. System za kibongo zinachosha sana.
 
Wengi wetu kazi tuzifanyazo hatuzipendi si bodaboda tu. Ni vile tu hatuna jinsi.
 
Absolutely mkuu. Mimi nafahamu vijana kama wawili ni mawakili kabisa Ila wameikosa kazi wanauza mitumba kwa whatsapp.. mwingine ni wakili Ila anaendesha Uber!

Wote hawa ukiwahoji wanakuambia taaluma zao haziwalipi ndo maana wanahustle kivyovyote vile ili mradi pesa ipatikane!

Mleta mada ana mshahara Kila mwezi hawazi chochote halafu anawaona vijana wa bodaboda wajinga huku yeye mwenyewe akitumia usafiri huo huo!

Hawa ndo "kigwangalla-type" wao wenyewe wameajiriwa halafu wanaambia vijana wajiajiri bila kufafanua wajiajiri vipi!
Jamaa anajifanya think out of the Box huku kakalisha ndeke TANAPA!

Game la mtaa ni gumu ila wanaokula chipsi mayai & kuku huko maofisini wanatuona wengine kama makatuni na hatuna akili. Katika maisha nimekuja kugundua elimu ya mtaa ndio real deal kuliko zile GPA tulizokuwa tunapiga chuo.
 
Wenzetu wana silicon valley sisi huku Africa tuna tuna bodaboda valley.
 
Bodaboda ni suluhisho la ajira kwa vijana (kisiasa ni mtaji)

Tatizo hatuangalii athari zake
- Matatizo ya ulemavu kwa vijana kutokana na ajali
- Gharama za kutibu na kuhudumia walemavu hao kwa Serikali na Jamii kwa ujumla
- tatizo la maumivu ya mgongo kutokana na vibration ya muda mrefu
- tatizo la uraibu wa pombe na ngono zembe (vijana hawana nidhamu ya matumizi ya fedha)
- kero za ajali za mara kwa mara
- Tatizo la kumaliza nguvu kazi (vijana wanakimbia kazi zinazotumia nguvu nyingi)
 
Ukitaka kujua msingi wa tatizo lenyewe anzia hapa:

- Soma sheria ya kodi na ya makampuni.

-- Angalia sera ya nchi kuhusu vijana na mahitaji kama ajira, mikopo

- Angalia namna nchi unavyotreat sekta binafsi.
- Angalia hata uanzishaji wa vitu vidogo tu kama Drones, youtube channel na blogs unavyokumbana na vikwazo.
- Then, njoo hapa:
+ Tanzania ina almost watu 60M.
+ Serikali imeajiri watu Laki 5 tu.
( Na bad enough imeshindwa kuwahudumia, wengi wana maisha magumu mno )
+ Maana yake watu wengine kila mmoja anajijua, bodaboda, vibanda barabarani, machinga etc
+ Na wakati huo huo watu wanahamasishwa kufyatuaaa

- Anyway sekta binafsi lia inapigwa vita: Ukianzisha biashara, unakutana na serikali yenyewe sokoni kupitia TANCOL, SUMA JKT, ATCK, ATCL, n.k

Yaani sijui unaelewa?

Okay, soma stori fupi:

Unamaliza chuo ukiwa na miaka 21 huku ukiwa na deni kama 10M la Loan board, ajira hakuna na deni linakuwa kwa 6% kila mwaka

Ukatafuta kikazi Fast Jet, mara ikapigwa vita ikafa mafao yako kupata NSSSF moaka ufikishe miaja 55.

Sasa unataka vijana waishi vipi ?
Asante chief kwa ufafanuzi makini, bado tuna safari ndefu sana.
 
Mleta mada una hoja ila haitaeleweka kwa uraisi.

Kwa mimi nilivyokuelewa ni unahoji kwamba hawa vijana wote wanaingia katika biashara ya bodaboda, it means wanaingia katika industry moja na kuacha ndoto zao kaajiri ya bodaboda.

Its true hili ni tatizo, sababu wengine walikuwa na ndoto za kuwa madaktari, mawakili au wanasheria, mainjinia, mapilot ila kutokana na haki ya sintofahamu ya kiuchumi kuwakuta wamejipata wapo katika sekta ya usafiri department ya bodaboda.

Si hao tu.... Wapo wengi sana katika industry zingine. Wapo ninaowafahamu ambao wapo katika upishi wa chipsi, wengine wamekuwa vinyozi, wengine wamekuwa madereva tax, wengine wamekuwa wauza magenge ya matunda na mboga mboga na kadhalika.

Unachosema ni kitu cha msingi sana ingawa haujakiweka vema sana kueleweka kuwa serikali na jamii kwa ujumla wamechagua kuwa sacrifice vijana na ndoto zao.

Yaani viongozi wa serikali wanaoteuliwa na kuchaguliwa wameshindwa kuja na mikakati, sera na mbindu shawishi, elekezi na saidizi za kumuinua kijana kuwa katika platform za uongozi wa jamii yake.

Pia jamii kama jamii tunafeli kwa namna ya ushiriki wetu kwenye michakato ya ujenzi wa taifa kwa maana ya uundaji wa sera, elimu ya mazingira yetu ya kiuchumi, kijamii na kisiasa zinavyokwenda, ni mambo gani tunayatumia kama platform za kuzungumzia matatizo yetu (eg. imagine kuna mtu anaamini dini ndio kikwazo cha yeye kutokuwa na maendeleo au ndio sababu mtu mwingine kumzidi au kumpita kimaendeleo).

Namna gani tunapata viongozi, nani anakuwa katika platform ya thinking na influences katika jamii pia inaathiri sana maendeleo yetu. Kwa mfano tazama ni nani wanawekwa kama role models na ni nini wanafanya. Kwa hapa tz tuna watu wa ajabu ajabu sana ndio wapo kwenye media, wapo kwenye social media, wapo kwenye matukio ya kiserikali. Yaani sifuri kabisa.

Kuna mambo mengi mkaranganyiko wake unampelekea kijana especially mtoto wakiume kupata wakati mgumu kufanya maendeleo.
 
Mkuu umeongea mengi yamsingi, lkn unasahau nchi yetu kama inamatatizo mengi yakujiajiri na ajira.

Kama Serikali tu inataka wahandisi wakawe walimu wa secondary au msingi huoni kama tatizo letu nikubwa, kuanzia huko maofisini hasa kwa wapanga sera?.

Hapo nahakika zaidi ya wahandisi 78% wakipata hio nafasi hawatokua wanapenda kazi wazifanyazo. Serikali inachangia kuua ndoto za vijana walio wengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom